Tafuta

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mazungumzo ya kidini, huko Berlin Ujerumani kuanzia 10-12 Septemba 2023. Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mazungumzo ya kidini, huko Berlin Ujerumani kuanzia 10-12 Septemba 2023.  (ANSA)

Papa Francisko:Vita vimesambaa katika sayari,amani inahitajika!

Hatuwezi kujikabidhi.Inahitaji kufanya kitu zaidi.Inahitaji shauku ya amani ambayo iko kwenye kitovu cha mkutano wenu.Uhalisia hautoshi,mazingatio ya kisiasa hayatoshi,vipengele vya kimkakati vinavyotekelezwa hadi sasa havitoshiNi katika Ujumbe wa Papa kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa sala ya amani,ulioandaliwa na Jumuiya ya Mt.Egidio huko Berlin,Ujerumani.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko  Jumanne tarehe 12 Septemba 2023 ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa maombi kwa ajili ya amani, ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuanzia tarehe 10 hadi 12 Septemba 2023 jijini Berlin, Ujerumani.  Katika ujumbe huo Papa amewaeleza kuwa wanakusanyika pamoja Berlin katika Mlango  wa Brandeburg, Wakuu wa Makanisa na Viongozi wa dini za kidunia, na Mamlaka ya kiraia walioalikwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambao kwa uaminifu wanaendelea na hija ya sala na mazungumzo yaliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II huko Assisi mnamo 1986. Eneo wanalofanyia mkutano kwa namna ya pekee linakumbusha hasa jambo la kihistoria; kuanguka kwa ukuta ambao ulikuwa unatengenisha Ujerumani mbili.    Na ukuta huo ulikuwa unagawanya hata dunia mbili za mashariki na magharibi mwa Ulaya. Kuanguka kwake, kulitokea kutokana na mchakato wa matukio mbali mbali, ujasiri wa wengi na sala za wengi, zilizofungua njia mpya za uhuru kwa ajili ya watu, kuunganisha familia lakini hata matumaini ya amani mpya ya ulimwenngu baada ya vita vya baridi.

Mkutano wa maombi huko Berli Ujerumani ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio
Mkutano wa maombi huko Berli Ujerumani ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwa bahati mbaya, katika miaka inavyokwenda hapakujengeka matumaini haya ya pamoja, lakini juu ya mafao maalum na juu ya kutokuaminiana kwa mtazamo wa wengine. Kwa njia hiyo badala ya kuvunja kuta, zimesimikwa nyingine. Na kuanza kutengeneza mitalo ambayo kwa bahati mbaya na  mara nyingi ni fupi. Leo hii vita vimetapakaa sana katika sehemu mbali mbali za dunia. Papa amekumbuka  sehemu za Afrika na Nchi za Mashariki ya Kati, lakini pia hata katika kanda nyingi za sayari; na Ulaya, ambayo inafahamika kwa vita vya  kwa mgogoro wa   Ukraine usiosemekana ambao hauoni mwisho na umesababisha vifo, majeruhi, uchungi, kuhama na uharibifu

“Mwaka jana nilikuwa nanyi huko Roma, katikka uwanja wa Masalia ya kale (Koloseo), kuombea amani. Tumesikia kilio cha amani kikivunjwa na kukanyagwa. Kisha nikasema: “ombi la amani haliwezi kuzuiwa: linatoka katika mioyo ya akina mama, limeandikwa kwenye nyuso za wakimbizi, za familia zinazokimbia, za waliojeruhiwa au wanaokufa. Na kilio hiki cha kimya kinainuka hadi Mbinguni. Hakijui kanuni mazingaombwe ili kutoka kwenye migogoro, lakini kina haki takatifu ya kuomba amani kwa jina la mateso ambayo inapata, na kustahili kusikilizwa. Inastahili kila mtu, kuanzia watawala, na zaidi wa chini kusikiliza kwa umakini na heshima. Kilio cha amani kinaonesha uchungu na utisho wa vita, mama wa umaskini wote.”

Mbele ya janga hili Papa  katika ujumbe anabainisha kwamba hatuwezi kujikabidhi, Inahitaji kufanya kitu zaidi. Inahitaji shauku ya amani ambayo iko kwenye kitovu cha mkutano wao, Uhalisia hautoshi, mazingatio ya kisiasa hayatoshi, vipengele vya kimkakati vinavyotekelezwa hadi sasa havitoshi; zaidi inahitajika, kwa sababu vita vinaendelea. Ujasiri wa amani unahitajika: sasa, kwa sababu migogoro mingi imeendelea kwa muda mrefu sana, kiasi kwamba baadhi inaonekana kutoisha, ili, katika ulimwengu ambapo kila kitu kinaendelea haraka, ni mwisho wa vita tu unaonekana polepole. Baba Mtakatifu Francisko amesema inahitaji Ujasiri wa kubadilisha, licha ya vizingiti na malengo magumu. Ari ya amani ni unabii ambao unaomba kwale ambao wanashirikia mamlka ya nchi na hatima ya nchi katika vita, kwa jumuiya ya Kimataia, sisi sote hasa wanaume na wanawake waamini kwa sababu waweze kutoa sauti kwa vilio vya maman a mababa ambao wanateseka na kuanguka , uahribifu usi ona mchiko, kutangaza uwehu wa vita.

Waziri wa Mambo ya Nje  wa Italia Bwana Antonia Tajani akiwa anatoa hotuba katika Mkutano huko Berlin
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Bwana Antonia Tajani akiwa anatoa hotuba katika Mkutano huko Berlin

“Ndiyo, ujasiri wa amani huwapa changamoto waamini kwa namna fulani, ambao ndani yake unageuzwa kuwa sala, kuomba kutoka Mbinguni kile kinachoonekana kuwa hakiwezekani duniani. Msisitizo wa maombi ni aina ya kwanza ya ujasiri. Katika Injili, Kristo anaonesha “uhitaji wa kusali siku zote, bila kuchoka” (Lk 18:1), akisema: “Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa(Lk 11:9). Hatuogopi kuwa ombaomba wa amani, kuungana na dada na kaka wa dini zingine, na wale wote ambao hawajajiuzulu kwa kuepukika  migogoro”. Kwa njia hiyo Papa amesema kuungana na maombi yako ili kuwepo na mwisho wa vita, kukushukuru kutoka chini ya moyo wake kwa kile wanachofanya.

Baba Mtakatifu amesema kiukweli inabidi kwenda mbele  ili kukwea ukuta isiyoweza kukanushwa, juu ya kumbukumbu ya maumivu mengi ya zamani na majeraha makubwa yaliyoteseka. Ni ngumu, lakini haiwezekani. Haiwezekani kwa waamini, ambao wanaishi ujasiri wa sala ya matumaini. Lakini ni lazima isiwezekane hata kwa wanasiasa, kwa wale wanaosimamia, na kwa wanadiplomasia. Ameomba kuendelea kusali kwa ajili ya amani bila kuchoka, kubisha hodo na roho ya unyenyekevu na kuendelea kubisha katika mlango daima ulio wazo wa moyo wa Mungu na katika milango ya watu. Papa amesema tuombe ili njia za amani zifunguke , hasa kwa ajili ya Nchi inayopigwa ya Ukraine, Tunayo imani kuwa Bwana daima anasikiliza kilio cha uchungu cha watoto wake. Bwana utusikilize, amehitimisha.

Papa ametuma Ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa maombi ya amani huko Berlin Ujerumani
12 September 2023, 16:00