Tafuta

2023.09.13 Turbai kutoka kumbu kumbu ya wahamiaji waliokufa huko Cutro kusini mwa Italia 2023.09.13 Turbai kutoka kumbu kumbu ya wahamiaji waliokufa huko Cutro kusini mwa Italia  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amepokea salio la familia ya Ulma na turubai la wahamiaji kutoka Cutro

Baada ya katekesi ya Papa,wakati wa salamu,Askofu Mkuu wa Przemyśl wa Poland alimpatia Papa Francisko mchoro na masalia ya familia ya Wapoland waliotangazwa wenyeheri hivi karibuni.Padre wa gereza la Crotone,ameleta kumbukumbu ya ajali ya meli ya wahamiaji huko Cutro,Calabria.Papa amebariki jiwe la Msingi wa Seminari.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Safu ya familia ya Ulma iliyotangazwa kuwa mwenyeheri huko Poland, turubai iliyoundwa na wafungwa wa Crotone katika kukumbuka ajali ya meli ya wahamiaji huko Cutro na jiwe la msingi la seminari mpya huko Ukraine zilikuwa ni alama tatu za historia  tofauti ambazo zilikabidhiwa mikononi mwa Papa Francisko, Jumatano tarehe 13 Septemba 2023, mara baada ya katekesi. Kwa hiyo wakati wa salamu na picha za makundi tofauti Papa aliweza kuona na kukabidhiwa mambo hayo. Na hivyo ushuhuda wa wanandoa wa Ulma na watoto wao saba ulirudiwa kuonekana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Hii ni Familia nzima iliyouawa kwa kuchukiwa imani yao wakati wanatoa ushuhuda wa ukarimu kwa Wayahudi, enzi za Kinazi, mnamo tarehe 24 Machi 1944 huko Markowa, na kutangazwa Wenyeheri na Kardinali Marcello Semeraro Mwenyekiti wa Baraz ala Kipapa la Kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu, Dominika  tarehe 10 Septemba 2023.

Papa alioneshwa Picha ya Wenyeheri wapya Familia ya Ulma na Picha ya Moyo Mtakatifu
Papa alioneshwa Picha ya Wenyeheri wapya Familia ya Ulma na Picha ya Moyo Mtakatifu

Papa alipewa masalia ya wenyeheri hao ambapo aliibusu kwa upole na picha inayoonesha familia hiyo. Waliokabidhi zawadi hizo muhimu ulikuwa ni ujumbe wa Poland, ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Przemyśl wa Kilatini, Adam Szal, ambaye alimwomba Baba Mtakatifu kubariki mchoro wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ambao utapelekwa katika parokia zote za Jimbo kuu.

“Tulikuja hasa kumshukuru Papa kwa uamuzi wake wa kuwatangaza  Józef na Wiktoria Ulma tukitumaini kwamba tukio hili la ajabu litazaa matunda ya kudumu na mengi katika maisha ya Kanisa. Tunaamini kwamba kwa ajili hiyo hija ya mchoro wa  Moyo Mtakatifu wa Yesu ambayo inaanza tarehe 18 Septemba 2023 na pia kutembelea Ufaransa itakuwa ya msaada mkubwa. Kwa dhamana maalum kwa Mtakatifu Maria Margaret Alacoque," alielezea Padre Witold Burda.

Kumbukumbu ya wahamiaji waliokufa huko Cutro

Mnamo Februari 26 iliyopita, huko Steccato ya  Cutro, Meli ya “Summer love", iliyojaa wahamiaji, ilizama mita chache kutoka ufukweni na vifo 94 vilivyothibitishwa, ambapo  35 walikuwa watoto. Ili kukumbuka moja ya janga kubwa la uhamiaji, wafungwa wa gereza la Crotone walitaka kukutoa zawadi  kwa Papa Francisko la  turubai, iliyokuwa kwenye sanduku la kioo, ambapo tukio hilo kubwa limeibuliwa tena la kuwakumbuka wafa maji katika harakati za kuvuka Bahari ya Mediterranea.

Turbai lililotengenezwa na wafungwa wa Crotone nchini Italia katika kumbukizi la vifo vya wahamiaji mwezi februati 2023
Turbai lililotengenezwa na wafungwa wa Crotone nchini Italia katika kumbukizi la vifo vya wahamiaji mwezi februati 2023

Kwa hiyo "Kuundwa kwa kazi hiyo pia ni njia ya kutoa sauti kwa wafungwa, alisema Padre msmamizi wa kiroho katika gereza la Crotone, Padre Oreste Mangiacapra  ambapo yeye ni nyeti kwa masula kama haya, akionesha kuwa wanataka kubadilika na kujiandaa, mara moja katika hukumu ili kuwa na muunganisho wa kweli wa kijamii, wa kibinadamu na wa kazi kama Papa Francisko ambavyo amezoea kusema na kutarajia. Kazi hiyo, aliongeza Federico Ferraro, mdhamini wa manispaa ya haki za wafungwa, kuwa “inawakilisha hisia zote za kushiriki wafungwa. Kwa wathirika  na ukaribu na waathirika na familia. Hii inamulika jinsi gani katika vituo vya magereza kuna watu ambao huhifadhi hisia za ushiriki wa kijamii."

Jiwe la msingi la Redemptoris Mater ya Uzhgorod

Ishara ya amani na onesho la hamu ya kujenga upya ndiyo maneno yaliyooneshwa na Padre Francesco Andolfatto, Mkuu wa Seminari ya Redemptoris Mater ya Uzhgorod, akielezea jiwe la msingi ambalo watajenga katika jiji la Kiukraine mpaka na Slovakia na Hungaria ambalo limebarikiwa na Papa Ftancisko, Jumatano 13 Septemba 2023 mara baada ya katekesi, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Kwa mujibu wa Padre huyo amesema “Wakati tunapopata ugumu sana huko  Ukraine tuko hapa kutokana na kibali maalum cha kuwachukua wanaseminari na wafundaji wote nje ya nchi, ambayo, kwa sababu ya kuandikishwa, haiwezekani kwa watu wa Ukraine wenye umri wa miaka 18 na zaidi ya miaka 60 kutoka nje. Kwa hivyo, pia tulifanya hija kusherehekea miaka kumi ya kuundw akwa mfuko wa seminari."

Papa anaonekana kuwa katikati ya ua na waamini mahujaji kutoka Asia
Papa anaonekana kuwa katikati ya ua na waamini mahujaji kutoka Asia

Makundi yalikuwa mengi ambayo yamemfuahia Baba Mtakatifu hata akwa ua kati ya waamini kutoka bara la Asia.

Papa amekutana na kupiga picha na kundi moja kutoka Afrika
Papa amekutana na kupiga picha na kundi moja kutoka Afrika

Vile hata makundi mengine ya mahujaji  kutoka bara la Afrika.

Papa alibusu masalia
13 September 2023, 10:41