Tafuta

2023.09.16 Papa amekutana na washiriki wa Shindano la la nyombo za Noeli 2023. 2023.09.16 Papa amekutana na washiriki wa Shindano la la nyombo za Noeli 2023.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko kwa wasanii wa Muziki ameshuri maeleano na ubunifu

Papa amekutana na washiriki wa Mashindano ya Noeli,shindano la kisanii kwa vijana ambao huandika nyimbo ambazo hazijachapishwa zilizochochewa na maadili ya Kuzaliwa kwa Bwana.Papa amewaeleza kuwa Muziki hauzungumzi na wao wenyewe tu,bali pia juu ya kutafuta Mungu na wakati mwingine Mungu mwenyewe.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 16 Septemba 2023   amekutana na kuwasalimu washiriki kwa furaha, wanamuziki vijana wanaoshiriki Shindano la Nyimbo za Noeli 2023, waandaaji, wasindikizaji na wafadhili. Hawa ni vijana ambao hutunga nyimbo ambazo hazijachapishwa zinazochochewa na maadili ya kuzaliwa kwa Bwana. Amefurahishwa na mpango huo, unaolenga kuwekeza katika elimu ili kutoa sauti kwa vijana na ubunifu wao. Pia ametoa shukrani kwa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, Mfuko wa Gravissimum Educationis na Jamhuri ya San Marino kwa ushirikiano wao wenye matunda katika kufanikisha tukio hilo, na pia kwa waendelezaji wa mpango wa "Il bene fa notizia" yaani wema unafanya habari, iliyounganishwa nayo, ambayo wakati wa majira ya kiangazo imetoa fursa muhimu ya mafunzo kwa vijana kutoka nchi za mbali kwenye Baraza la Kipapa la Mawasiliano, shukrani kwa wote.

Papa Francisko akiwageukia vijana hao kwamba watunzi! Na utunzi ni sanaa inayodai, ambayo inahitaji, kwa upande mmoja, ujuzi wa muziki na sheria zake na lugha yake na, kwa upande mwingine, uwezo wa kutoa sauti kwa maswali, maongozi na matamanio ya moyo. Ni sanaa inayohitaji, kwa maneno mawili, maelewano na ubunifu, ambayo yanakwenda pamoja. Kwa maana hiyo Papa ameongeza kusema kuwa  tunaweza kusema kwamba kutunga muziki ni muundo wa  maisha, ambapo tunahitaji yanahitajika mambo yote  wawili kuungana kwa amani na wengine, na jamii na sheria zake, na kutoa nafasi kwa uhalisi wa namna ya watu kuwa na kujieleza pamoja. Maelewano na ubunifu, kwa sababu havipo katika mzozo bali kiukweli ni utaftaji wa maelewano, ambao unahitaji kujitolea, na uthabiti, katika muziki kama maishani, haufedheheshi, lakini hukomboa upekee wa kila mmoja, kumpatia msanii zana za kuwasiliana kwa njia ambayo inaeleweka kwa wengine, ili kuwa zawadi ya kujenga kwa furaha ya wote. Kwa hiyo,  Papa ametoa shukrani ya  kwanza kwenda katika  usahihi kwa ahadi yao hii katika kujifunza sanaa ya muziki ya maelewano ambayo inahitaji jitihada na masaa mengi ya mazoezi!

Papa na wasanii wa Muziki
Papa na wasanii wa Muziki

Baba Mtakatifu amebainisha kuwa wakati huo huo, hata hivyo, kile ambacho  msanii anashiriki katika kila moja ya kazi zake huzungumza juu ya hisia za kipekee, za kibinafsi na za karibu. Kwa hivyo katika nyimbo wanazowasilisha kwenye Shindano, nyuma ya kila mada ambayo umependekeza, wanatupatia uwezekano wa kukutana nao katika wakati usioweza kurudiwa, ule wa msukumo, ambao ni wao wote, lakini ambao walitaka kushirikirikisha kwa  kumeta meta kwa nuru, tetemeko la upendo, mtazamo wa bluu katika anga ya maisha, mshtuko wa mshangao katika uso wa uzuri, au labda uchungu wa maumivu au kilio cha kupinga, ambacho kimeonekana moyoni mwao na ambayo wametoa sauti kupitia sanaa. Hivi ndivyo wanavyotupatia, na kwa hiyo imebua shukrani ya pili ya Baba Mtakatifu kwa sababu kwa nyimbo zao wanatupatia kidogo wao mwenyewe! Hii ni muhimu, msanii hujitolea wakati anaunda kazi, wakati anafanya kazi, Papa amekazia

[ Photo Embed: Papa akutana na wasanii wa muziki]

Hatimaye, shindano hilo linafanyika kwa mtazamo wa Tamasha la Noeli wakati ambapo nyimbo za washindi zitaimbwa. Inaonekana mapema kidogo kuzungumza juu ya Noeli sasa, katikati ya Septemba. Siku kuu  muhimu, hata hivyo, huanza kutayarishwa mapema, na Kuzaliwa kwa Yesu kunastahili hili na zaidi! Na kisha muziki hauzungumzi tu juu yetu wenyewe, bali pia juu ya utafutaji wa Mungu, na wakati mwingine wa Mungu mwenyewe! Na ni vizuri, kwa sababu maelewano na ubunifu, ambayo alitaka kuwambia hupatikana kwanza ndani yake, na Noeli inawaonesha kwa njia maalum na ya kusisimua, ikitupatia Bwana kuwa mdogo kwa ajili yetu, kuwa wake, yaani  mwanadamu kuwasiliana nasi lile joto lisilo na mwisho la upendo wake wa kimungu. Wakati wa Noeli, Mungu, Neno la milele, huja kutusikiliza na kufanya kazi ili kuunda maelewano na wanadamu, wakati katika ubunifu wake wa kushangaza anatutazama kwa macho ya mtoto, akitushangaza kwa huruma yake isiyo na hatia. Na hii haifanyiki tu mnamo Desemba 25, lakini kila siku!

Papa na wasanii wa shindano la Muziki wa Noeli 2023
16 September 2023, 12:10