Tafuta

Papa Francisko:Jumuiya ya Mongolia ni Kanisa nyenyekevu na furaha

Papa Francisko katika katekesi yake Septemba 6,baada ya kurejea kutoka ziara ya kitume,ameelezea hatua muhimu zaidi za nchi aliyotembelea huko Mongolia kwamba alikutana na Kanisa nyenyekevu na lenye furaha na kwamba ni watu wanaojisikia pumzi ya muumba.Amewaomba watu kuwa na moyo wa ukaribu kwa kika mtu na kila ustaarabu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumatano tarehe 6 Septemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko amejikita katika katekesi yake kutoa mhutasari  wa Hija yake ya kitume ya 43 Nchini Mngolia kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza mhutasari huo amesema Jumatatu alirudi kutoka Mongolia. Na kwa hiyo angependa kutoa shukrani zake kwa wale waliomsindikiza katika ziara yake kwa maombi, na kurudia shukrani zake kwa wenye mamlaka, ambao walimkaribisha kwa dhati: hasa Mheshimiwa Rais Khürelsükh, na pia Rais wa zamani Enkhbayer, ambaye alimpatia mwaliko rasmi wa kutembelea nchi hiyo. “Ninakumbuka nyuma kwa shangwe ya Kanisa la mahali hapo na watu wa Kimongolia: watu waungwana na wenye busara, ambao walinionesha uchangamfu na upendo mwingi. Na kwa hiyo Papa amependa kuelezea lengo la safari hiyo. “Mtu anaweza kuuliza: kwa nini Papa alikwenda mbali sana kutembelea kundi dogo la waamini? Kwa sababu ni pale hasa, mbali na mwangaza, ambapo mara nyingi tunapata ishara za uwepo wa Mungu, ambaye haangalii sura, bali moyo, kama tulivyosikia katika kifungu kutoka kwa nabii Samweli (rej. 1Sam 16:7). Bwana hatazamii jukwaa la katikati, bali moyo mwepesi wa wale wanaomtamani na kumpenda bila kujionesha, bila kutaka kujiinua juu ya wengine. Na nilikuwa na kundi mkutano, huko Mongolia, Kanisa nyenyekevu, na Kanisa lenye furaha, ambalo liko moyoni mwa Mungu, na ninaweza kushuhudia furaha yao ya kujikuta pia katikati ya Kanisa kwa siku chache.”

Papa Francisko katika katekesi 6 Septemba
Papa Francisko katika katekesi 6 Septemba

Baba Mtakatifu akiendelea na kuelezea ziara yake nchini Mongolia amesema kuwa “Jumuiya hiyo ina historia ya kugusa moyo. Ilitokea, kwa neema ya Mungu, kutoka kwa bidii ya kitume  ambayo tunatafakari juu yake wakati huo  ya wamisionari wachache ambao, kwa kupendezwa na Injili, walikwenda kama miaka thelathini iliyopita hadi nchi ambayo hawakuijua. Walijifunza lugha  ambayo si rahisi na, licha ya kutoka mataifa tofauti, ilitoa uhai kwa jumuiya ya Kikatoliki yenye umoja na ya kweli. Hakika, hii ndiyo maana ya neno ‘katoliki, ambalo linamaanisha ‘ulimwengu.’ Lakini sio ulimwengu wote ambao unafanya kufananisha yote,  badala yake  ni ulimwengu wote unaojumuisha, ni ulimwengu wote ambao umekuzwa. Huu ni ukatoliki unaojumuishwa, kiutamaduni, na ambao unakumbatia mema pale inapopatikana na kuwatumikia watu ambao wanaishi nao. Hivyo ndivyo Kanisa linavyoishi katika kushuhudia upendo wa Yesu kwa upole, kwa maisha kabla ya maneno, kufurahishwa na utajiri wake wa kweli katika huduma kwa Bwana na kwa ndugu. Kwa kusisitiza Papa amesema kuwa, hivyo ndivyo Kanisa hilo changa lilivyozaliwa: katika roho ya upendo, ambayo ni ushuhuda bora wa imani.

Waamini kutoka pande za dunia katika Katekesi ya Papa
Waamini kutoka pande za dunia katika Katekesi ya Papa

Mwishoni mwa ziara yake Papa amebainisha alivyofurahi kubariki na kufungua “Nyumba ya Huruma, kazi ya kwanza ya Upendo ambayo ilianzishwa nchini Mongolia kama maonesho ya vipengele vyote vya Kanisa la mahali hapo. Nyumba ambayo ni kadi utambulisho wa wito ya Wakristo hao, lakini ambayo inaomba kila jumuiya yetu iwe nyumba ya huruma: yaani, mahali pa wazi, mahali pa kukaribisha, ambapo mateso ya kila mtu yanaweza kuingia bila aibu katika kuwasiliana nao. Huruma ya Mungu, inayoinua na kuponya. Huu ni ushuhuda wa Kanisa la Kimongolia, lenye wamisionari kutoka nchi mbalimbali wanaojisikia kuwa na umoja na watu, wenye furaha kuwahudumia na kugundua uzuri ambao tayari upo. Kwa sababu wamisionari hawa hawakwenda kugeuza imani; kwa sababu hiyo sio uinjilishaji. Wao walikwenda kuishi huko kama watu wa Kimongolia, kuzungumza lugha yao, lugha ya watu hao, kuchukua maadili ya watu hao na kuhubiri Injili kwa mtindo wa Kimongolia, kwa maneno ya Kimongolia. Walikwenda na wakakuzwa na wakavaa utamaduni wa Kimongolia wa kutangaza Injili katika utamaduni huo.

Papa akiwalekea waamini na mahujaji katika katekesi 6 Septemba 2023
Papa akiwalekea waamini na mahujaji katika katekesi 6 Septemba 2023

Baba Mtakatifu aidha amesimulia jinsi ambavyo aliweza kugundua kitu cha uzuri huo pia kwa kukutana na baadhi ya watu, kusikiliza historia zao, kufahamu jitihada zao za kidini. Katika suala hilo Papa ameshukuru mkutano wa kidini na wa kiekumeni wa Dominika tarehe 3 Septemba.  Mongolia ina mila kuu ya Kibuddha, yenye watu wengi ambao wanaishi dini yao kwa njia ya kweli na kali, kwa ukimya, kwa kujitolea na ujuzi wa shauku  zao wenyewe.  Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amewaalika kufikiria ni mbegu ngapi za wema zilizofichwa na  zinazofanya bustani ya dunia isitawi, na wakati huku kwa kawaida tunasikia sauti  tu za miti inayoanguka! Kwa kuongezea  Papa amesema “ na watu hata sisi, tunapenda kashfa: lakini tazama unyama mti umenguka, ulipiga kelele gani:  Lakini huoni msitu unaokua kila siku? Kwa sababu ukuaji ni  wa kimya. Ni jambo la kuamua kuweza kung’amua  na kutambua mema. Hata hivyo, mara nyingi tunathamini wengine kwa kadiri tu wanavyopatana na mawazo yetu; na lazima tuone jambo hilo jema. Na hiyo ndio sababu ni muhimu kuelekeza mitazamo  yetu juu, kuelekea nuru ya wema. Ni kwa njia hiyo tu, kuanzia na utambuzi wa mema tu, tunaweza kujenga mustakabali wa pamoja;  kwa kuwathamini wengine tu tunaweza kuwasaidia wafanye maendeleo.

Papa akisalimia watu katika uwanja
Papa akisalimia watu katika uwanja

Papa Francisko amesema kwamba “Nilikuwa katika moyo wa Asia, na hiyo ilinifanyia mema. Ni vizuri kuingia katika mazungumzo na bara hilo kubwa, kukusanya jumbe zake nyingi, kujua hekima yake, njia yake ya kutazama mambo, kukumbatia wakati na nafasi”. Kwa hiyo ilikuwa vizuri kwake kukutana na watu wa Kimongolia, ambao wanathamini mizizi na mila zao, wanaoheshimu wazee na kuishi kwa amani na mazingira. Ni watu wanaotafakari anga na kuhisi pumzi ya uumbaji. Kufikiria upanuzi usio na kikomo na wa kimya wa Mongolia, Papa ameombea hivyo   tuchochewe na hitaji la kupanua mipaka ya mitazamo yetu, tafadhali: tupanua upeo wa mtazamoa kwa kuagalia, juu na chini, lakini kwa kuwa makini ili tusiangukie kuwa mfungwa kwa mambo madogo. Tupanue mipaka ya mitazamo  yetu, ili tuweze kuona mema kwa wengine na kuwa na uwezo wa kupanua upeo wetu, na tufungue mioyo yetu pia; tunahitaji kuufanya moyo wetu ukue na kupanuka, ili kuelewa, kuwa karibu na kila mtu na kila ustaarabu. Ameshukuru.

Katekesi ya Papa 6 Septemba 2023
06 September 2023, 16:34