Tafuta

2023.09.27 Papa Francisko wakati wa katekesi yake. 2023.09.27 Papa Francisko wakati wa katekesi yake.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Bahari ya Mediterania iwe picha ya ustaarabu na sio kaburi

Papa Francisko katika katekesi yake Septemba 27 ameeleza kwa kifupi ziara yake ya kitume ya Septemba 22 na23 huko Marsiglia kwa kushiriki katika kikao cha mwisho cha ‘Rencontres Méditerranéennes.’Amekumbusha kuwa watu kwa heshima kamili wanaweza kuchagua kuhama au kutohama.

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika katekesi yake Jumatano tarehe 17 Septemba 2023, kwa waamini na mahujaji walikusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro ameelezea juu ya ziara yake ya 44 ya Kitume huko Marsiglia, iliyofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 23 Septemba 2023 ili kuhitimisha mikutano ya Mediteranea iliyokuwa inaendelea karibu kwa Juma zima kwenye mji wa Kusini mwa Ufaransa. Papa Francisko akianza amesema: “Nilikwenda Marsiglia mwishoni mwa Juma lililopita ili kushiriki katika hitimisho la Rencontres Méditerranéennes (Mikutano ya Mediterania), iliyohusisha Maaskofu na mameya kutoka eneo la Mediterania, pamoja na vijana wengi, ili mtazamo wao uwe wazi kwa siku zijazo. Kwa kweli, tukio lililofanyika Marsiglia liliitwa "Muundo mzuri wa Matumaini". Hii ndiyo ndoto, hii ndiyo changamoto: kwamba Mediterania ipate kurejesha wito wake, ule wa kuwa maabara ya ustaarabu na amani. Papa Francisko amesema.

Kundi mojawapo la wanahija katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kundi mojawapo la wanahija katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Kama tunavyojua, Mediterania ndio chimbuko la ustaarabu na utoto ni wa maisha! Haivumiliwi kuwa kaburi, wala isiwe mahali pa migogoro. Bahari ya Mediterania ni kinyume kabisa cha mgongano kati ya ustaarabu, vita na  biashara ya binadamu. Ni kinyume kabisa kwa sababu Mediterania ni njia ya mawasiliano kati ya Afrika, Asia, na Ulaya; kati ya kaskazini na kusini, mashariki na magharibi, watu na tamaduni, watu na lugha, falsafa na dini. Bila shaka, bahari daima ni shimo la kushinda kwa namna fulani, na inaweza hata kuwa hatari. Bali maji yake hulinda hazina za uhai; mawimbi yake na upepo wake hubeba vyombo vya kila aina. Kutoka ufukwe wake wa mashariki, miaka elfu mbili iliyopita, Injili ya Yesu Kristo ilipelekwa. Bila shaka, hili tangazo la Injili halitokei kama kiini macho, wala halitimizwi mara moja na kwa wote. Ni matunda ya mchakato wa safari ambayo kila kizazi kinaitwa kusafiri kipande,  na kusoma alama za nyakati ambacho kinaishi.

Makundi ya wanahija na Papa Francisko mara baada ya katekesi
Makundi ya wanahija na Papa Francisko mara baada ya katekesi

Baba Mtakatifu Francisko katika kueleza ziara yake amesisitiza kuwa: Mkutano huo huko Marsiglia ulifanyika baada ya mikutano kama hiyo iliyofanyika Bari mnamo 2020 na huko Firenze 2022. Haikuwa tukio la pekee, lakini ni kupiga hatua mbele kwenye ratiba iliyoanza na "Mediterranean Colloquia" yaani  Majadiliano ya Mediteranea iliyoandaliwa na Giorgio La Pira, aliyekuwa Meya wa Fierenze nchini Italia , mwishoni mwa miaka ya 1950. Ni hatua ya mbele leo  hii ni kujibu ombi lililozinduliwa na Mtakatifu Paulo VI katika Waraka wake wa kitume wa  Populorum progressio, yaani maendeleo ya binadamu, kuhamaisha “jumuiya ya ulimwengu yenye utu zaidi, ambapo wote wanaweza kutoa na kupokea na ambapo maendeleo ya wengine hayanunuliwi kwa gharama ya wengine.” 

Katika muktadha huo Baba Mtakatifu ameuliza swali kuwa: Je ni nini kilitokea katika tukio la Marsiglia? Kilichojitokeza ni mtazamo wa Bahari ya Mediterania ambao alisema angeuita tu binadamu, si wa kiitikadi, si wa kimkakati, si sahihi kisiasa wala si chombo; hapana, mwanadamu, yaani, anayeweza kurejea kila kitu kwa thamani ya msingi ya mtu na hadhi yake isiyoweza kukiukwa. Kisha, wakati huo huo, mtazamo wa matumaini ulitokea. Papa amesema kuwa : “ leo hii inashangaza unaposikia ushuhuda kutoka kwa wale ambao wameishi katika hali zisizo za kibinadamu, au ambao wameshirikishana nao, na wao wenyewe wanakupatia "fundisho la matumaini". Na pia mtazamo wa kidugu.

Katekesi ya Papa 27 Septemba 2023

Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amewaeleza kuwa:"tumaini hili, na udugu huo haupaswi “kuyeyuka”; hapana, badala yake, linahitaji kupangwa, kuunganishwa kupitia vitendo vya muda mrefu, vya kati na vya muda mfupi ili watu, kwa heshima kamili, waweze kuchagua kuhama au kutohama. Mediterania lazima iwe ujumbe wa matumaini." Lakini kuna kipengele kingine cha nyongeza kwamba matumaini yanahitaji kurejeshwa kwa jamii zetu za Ulaya, hasa kwa vizazi vipya. Kiukweli, tunawezaje kuwakaribisha wengine ikiwa sisi wenyewe hatuna upeo wa kuona wakati ujao? Je, vijana, ambao ni maskini wa matumaini, wanawezaje kujifungia katika maisha yao ya kibinafsi, wakiwa na wasiwasi juu ya kudhibiti hatari zao wenyewe, ili wajifungue kukutana na wengine na kushiriki?

Papa amewasalimia kundi moja la kimchezo katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa amewasalimia kundi moja la kimchezo katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Jamii zetu, ambazo mara nyingi zimekithiri na ubinafsi,na utumiaji wa vitu na kuwa na utupu, zinahitaji kujifungua moyo zao ili kupata kujazwa na oksijeni na kisha wataweza kjifunza shida kama fursa na kukabiliana nayo vyema. Ulaya inahitaji kurejesha shauku na ari.  Na amewezea kusema kuwa alifurahishwa  huko Marsiglia na  Mchungaji wake, Kardinali Aveline; makuhani na watu waliowekwa wakfu; Waamini Walei waliojitolea kwa upendo, kwa elimu; katika Watu wa Mungu walioonesha uchangamfu mkubwa wakati wa Misa katika Uwanja wa Vélodrome, amewashukuru wote na Rais wa Jamhuri, ambaye kwa uwepo wake alishuhudia kwamba Ufaransa yote ilikuwa makini na tukio la Marsiglia.  Kwa kuhitimisha amesema "Mama Yetu, ambaye watu wa Marsiglia wanamheshimu kama Notre Dame de la Garde, yaani Mama Yetu wa Ulinzi awasindikize katika safari ya watu wa Mediterania ili eneo hilo liwe kama limekuwa likiitwa kuwa – Muundo mzuri wa ustaarabu na matumaini."

27 September 2023, 13:06