Papa atoa wito kwa ajili ya Nchi ya Libya na Morocco katika mikasa
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya Katekesi, kwa waamini na mahujaji waliunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 13 Septemba 2023, mawazo yake yamewaendea watu wa nchini Libya ambao wamekumbwa na mvua ya nguvu, ambayo ilisababisha mafuriko makubwa hadi kusababisha kujaa kwa mabwawa mawili kwa wakati mmoja ambayo yaliporomoka na kuua watu wengi na majeruhi ikiwa ni pamoja na madhara makubwa ya miundo mbinu nchini humo. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesema: “Ninawaalika kuungana na sala yangu kwa ajili ya wale walipoteza maisha, kwa ajili ya familia zao na kwa wale waliorundikana. Wasikose mshikamano wetu wa kuelekeza kwa kaka na dada waliojaribiwa namna hiyo na mkasa huu”.
Tetemeko la Morocco
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea aidha mawazo yake pia yamewageukia watu watukufu wa Morocco "ambao wameteseka kutokana na mtikisiko wa ardhi, wa matetemeko haya. Tusali kwa ajili ya Morocco, tusali kwa ajili ya wakazi. Na Bwana awapatie nguvu za kuanza tena; ya kuanza tena baada ya janga hili lisilosemakana ambalo limepita.” Papa amekazia
Pyaisheni mwamko wa huduma ya Injili
Baba Mtakatifu vile vile amewaelekea na kuwakaribisha mahujaji wa lugha ya kitaaliano kwa namna ya pekee Watawa wa Shirika la Watumishi wa Masikini, huku akiwatakia wawe na Mkutano Mkuu mwema na kupyaisha mwamko wa kitume katika huduma ya Injili.
Manajeshi kutiwa moyo kwa huduma ya ndugu
Furaha ya Baba Mtakatifu pia ni kuwakaribisha kikundi cha AVIS ambacho ni chama cha Italia cha kutoa damu cha Vallecorsa, Kikundi cha kujitolea Love Bridges, Wanajeshi wa Motta ya Lavenza na wa Portogruaro ambapo amewatia moyo kila mmoja wa kikundi hicho katika shughuli ya huduma kwa ndugu.
Hatimaye kama kawaida yake, mawazo yake ni kwa vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya. Baba Mtakatifu Francisko amependa kukumbusha kila tarehe 14 Septemba ya kila mwaka, ambapo Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu. Kwa hiyo amesema: “Tusichoke kuwa waaminifu wa Msalaba wa Kristo, Ishara ya upendo na wa Wokovu. Na kwa wote amewabariki.