Papa atafanya ziara huko Marsiglia kuanzia 22-23 Septemba 2023
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Baba Mtakatifu Dominika tarehe 17 Septemba 2023, mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, amewaeleza jinsi ambavyo Ijumaa tarehe 22 Septemba 2023, atakwenda huko Marsiglia nchini ufaransa kwa ajili ya kushiriki hitimisho la Mkutano wa Rencontres Méditerranéennes, yaani Mikutano ya Mediterania, na kwamba ni mpango mzuri ambao unajitokeza katika miji muhimu ya Mediterania, ikiwaleta pamoja viongozi wa kikanisa na kiraia ili kukuza njia za amani, ushirikiano na mshikamano kuzunguka 'Nostrum mare', yaani 'Bahari yetu' kwa kuzingatia kwa namna ya pekee jambo la uhamiaji.
Hii inawakilisha changamoto ambayo si rahisi, kama tunavyoona kutoka katika habari za siku za hivi karibuni, lakini ambayo lazima ikabiliwe kwa pamoja, kwani ni muhimu katika maisha ya baadaye ya kila mtu, ambayo yatakuwa na mafanikio ikiwa yatajengwa juu ya udugu, na kuweka hadhi na utu wa binadamu, watu thabiti hasa wale wanaohitaji zaidi. Baba Mtakatifu Francisko kwa kuongezea amesema kwamba: “Wakati ninawaomba mnisindikize na safari hii kwa maombi, ningependa kuwashukuru viongozi wa serikali na wa kidini, na wale wanaofanya kazi ya kuandaa mkutano huko Marseille, jiji lenye watu wengi, linaloitwa kuwa bandari ya matumaini. Kuanzia sasa na kuendelea ninawasalimu wakazi wote, nikingoja kukutana na kaka na dada wengi wapendwa.”
Amewasalimu wote, Warumi na mahujaji kutoka Italia na nchi mbalimbali, hasa wawakilishi wa baadhi ya parokia za Miami, Banda la Gaitas ya Batallon de San Patricio, waamini wa Pieve ya Cairo na Castelnuovo Scrivia, Masista Wamisionari. wa Mkombozi Mtakatifu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiukraine.
Lakini pia Papa akuhasahu kwamba “Na tunaendelea kuwaombea watu wa Kiukraine wanaoteswa na amani katika kila nchi iliyomwaga damu na vita. Na amewasalimu Vijana wa Moy safi wa maria . Amehitimisha kwa kuwatakia Dominika njema na tafadhali wasisahau kumuombea. Mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana.