Tafuta

2023.09.22 Papa Francisko amefika na kukaribishwa huko Marsiglia 2023.09.22 Papa Francisko amefika na kukaribishwa huko Marsiglia  (Vatican Media)

Papa amefika Marsiglia kwa ajili ya Mkutano kuhusu mediteranea

Papa hatimaye amefika Marsiglia kusini mwa Ufaransa na kupokelewa uwanja wa ndege.Akiwa kwenye ndege Papa kama kawaida ya ziara zake za kitume,aliwasalimia mmoja baada ya mwingine waandishi wa habari kimataifa na na kuonesha huchungu kuhusu wahamiaji kuwa wanafanyiwa ukatili.

Vatican News

Ninatumaini nitakuwa na ujasiri wa kusema kile ninachotaka kusema. Haya ni matumaini binafsi ambayo Baba Mtakatifu Francisko aliwashirikisha kwa waandishi wa habari takriban 70 wanaoandamana naye katika ziara yake ya 44 ya kitume hadi Marsiglia, ambapo Papa atashiriki katika  Kufunga "Rencontres Méditerranéennes" yaani Mikutano ya kimeteranea, ambalo ni tukio linaoongozwa na mada ya uhamiaji. Akichukua kipaza sauti kwenye ndege kuwageukia waandishi wa habari, Papa Francisko alisema: "Habari za mchana wote na asante kwa kuja, ninawatakia kazi njema. Inaweza kuwa muda mfupi lakini mambo mengi katika jiji hilo ambalo ni mlango, dirisha, kwa hiyo ni kila kitu. ... kwenye Mediterania… Asanteni.”

Papa Francisko amezungumza na waandishi wa habari
Papa Francisko amezungumza na waandishi wa habari

Kama kawaida ya ziara zake, Papa aliwasalimia waandishi na wapiga picha wote wa magazeti ya kimataifa mmoja baada ya mwingine. Kwa wale waliomkumbusha juu ya hali ya siku za hivi karibuni huko Lampedusa na katika maeneo mengine ya kutua kwa  idadi ya wahamiaji damu" wa kutisha. Papa pia alielezea uchungu wake kwa picha iliyooneshwa kwake ya mama mmoja mhamiaji akiwa na mtoto wake, maumivu kwa wengi kama mwanamke huyu aliyezuiliwa katika "kambi" za Libya na kisha kuwekwa kwenye boti baharini, akikabiliwa na hatari nyingi.

Papa akipokelewa Uwanja wa Ndege
Papa akipokelewa Uwanja wa Ndege
22 September 2023, 17:15