Tafuta

Papa Francisko ametuma ujumbe wa rambirambi na kuonesha ukaribu wa watu wa Libya waliokumbwa na kimbunga na mafuriko. Papa Francisko ametuma ujumbe wa rambirambi na kuonesha ukaribu wa watu wa Libya waliokumbwa na kimbunga na mafuriko.  (AFP or licensors)

Papa anaonesha ukaribu kwa waliokumbwa na kimbunga na mafuriko,Libya!

Katika telegramu kwa Balozi wa Vatican huko Rabat nchini Libya,Papa anaonesha uchungu na kuwaombea marehemu zaidi ya 2,300 waliokufa kutokana na mafuriko yaliyokumba eneo la mashariki mwa nchi na kueleza ukaribu kwa walionusurika na waokoaji.Askofu Overend,Msimamizi wa kitume wa Benghazi:kuna hitaji kubwa la msaada wa kimataifa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican,

Faraja,nguvu na ustahimilivu ndiyo maombi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya wale ambao wameathiriwa na uharibifu uliosababishwa na mafuriko mashariki mwa Libya. Ni katika telegramu ya Baba Mtakatifu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Jumanne tarehe 12 Septemba 2023  akielekezwa kwa  Balozi wa Vaticani Askofu Mkuu Savio Hon Tai-Fai.  Katika ujumbe huo, “anaonesha masikitiko makubwa kuhusu hasara kubwa ya maisha na uharibifu uliosababishwa na mafuriko katika eneo la mashariki mwa Libya, na anawahakikishia maombi yake kwa ajili ya roho za marehemu na wale wote wanaoomboleza kupoteza wapendwa wao”. Baba Mtakatifu “pia anaonesha ukaribu wa kina wa kiroho kwa waliojeruhiwa, kwa wale wanaoogopa wapendwa wao waliopotea na wafanyakazi wa dharura wanaotoa msaada na usaidizi. Kwa wale wote walioguswa na janga hilo, Baba Mtakatifu Francisko kwa utashi wake mwema anawaomba baraka za Mungu za faraja, nguvu na uvumilivu.” Unasomeka Ujumbe huo uliotiwa saini na Katibu wa Vatican.

Elfu kumi wamepotea na zaidi ya wahanga 2,300

Idadi ya watu waliopotea kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Daniel, kilichosababisha vifo vya watu 2,300 katika eneo la mashariki mwa nchi, kulingana na idadi kubwa ya watu waliopotea, ni elfu kumi. Dhoruba kali sana, baada ya kuzuru Ugiriki, Uturuki na Bulgaria, ilisababisha kuporomoka kwa wakati mmoja kwa mabwawa mawili ambayo yalitoa lita milioni 33 za maji. Kwa hiyo hali ni mbaya kama ile ya Morocco, ambayo inashughulikia matokeo ya tetemeko la ardhi: hii imesemwa na mkuu wa ujumbe wa Msalaba Mwekundu katika mkutano wa UN huko Geneva aliyeunganishwa kupitia video na Tunisia.

Miili imetanda kila mahali: baharini, kwenye mabonde, chini ya majengo, waziri wa usafiri wa anga na mjumbe wa kamati ya dharura, Hichem Chkiouat, aliiambia shirika la habari Reuters. Robo ya jiji la Derna limeangamizwa, alisema mmoja wa mawaziri wa utawala unaoongoza mashariki mwa nchi. Akiwa amehuzunishwa na picha za uharibifu nchini Libya, ulioharibiwa na hali mbaya ya hewa ambayo imesababisha hasara mbaya ya maisha ya watu wengi  Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa Sera ya Mambo ya Nje, Josep Borrell, aliandika katika X, na kuongeza:  Umoja wa Ulaya (EU) unafuatilia kwa karibu na wako tayari kutoa msaada.

Huzuni wa kina na kushiriki kwa dhati katika maumivu ya watu wa Libya wenye urafiki ni maneno ya  Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, katika ujumbe uliotumwa kwa Rais wa Nchi ya Libya, Mohamed Younis Al- Menfi. Na katika kusindikiza rambi rambi hizo pia ni utayari wa Italia kuchangia juhudi za misaada. Na kuchanganyikiwa, msisimko, hali fulani ya kutokuwa na uwezo ni dhahiri katika maneno ya Askofu  Sandro Overend Rigillo, msimamizi wa kitume huko Benghazi, aliyefikiwa kwa njia ya simu na Vatican News ambapo alisema mahali walipo kulikuwa kumetulia hata kama kulikuwa na dhoruba kali na mabomu ya maji hapakuwapo na matatizo fulani eneo lao. Walakini, viongozi waliwaamuru kukaa nyumbani kwa siku tatu. “Tatizo liko katika mlima. Aliripoti kuwa aliwasiliana na kaka zake huko Bayda, wakijihakikishia usalama wao, hata kama walikuwa na hofu kubwa. Alikumbuka kwamba dhoruba za ukubwa huu nchini Libya ni nadra sana, labda ni mara ya kwanza  jambo kama hili kutokea.

Telegrma ya Papa kwa waathirika wa maporomoko Nchini Libya.
12 September 2023, 16:21