Tafuta

Papa Francisko amemtuma tena kuwa mwakilishi wake huko Beijing China katika nyayo za utafutaji amani. Papa Francisko amemtuma tena kuwa mwakilishi wake huko Beijing China katika nyayo za utafutaji amani. 

Kardinali Zuppi anakwenda Beijing kwa kutumwa na Papa kwa ajili ya amani ya haki

Baada ya safari za Kyiv,Moscow na Washington,rais wa CEI anaendelea na mpango aliokabidhiwa na Papa Francisko katika harakati za “kupunguza mvutano huko Ukraine.Vatican inabanisha kuwa ni “Hatua zaidi ya kuunga mkono mipango ya kibinadamu na utafutaji wa njia ambazo zinaweza kuleta amani ya haki.Kardinali Zuppi:“Maombi ya wengi yananisukuma kufuma mtandao mgumu wa amani.”

Vatican News

Mara baada ya miezi kadhaa ya kungoja na kutazamia, kwenda Beijing, kwa ajili ya utume wa amani hatimaye  uthibitisho umefika kwamba Kadinali Matteo Maria Zuppi, kwa kile ambacho Papa alikiita "chukizo la amani" ili "kupunguza mivutano" katika Ukraine inayoteswa, unaendelea nchini China. Safari yake ni mpango wa kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba 2023. Ni Vatican iliyotangaza juu ya  safari mpya ya Kadinali ambayo tayari ilikuwa imemwona akiwa na shughuli nyingi kati ya mwezi Juni na Julai huko Kyiv, nchini Ukraine, Moscow nchini Urussi na Washington nchini Marekani.

Kwa njia hiyo  "tarehe 13 - 15 Septemba 2023, Kardinali Matteo Maria Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) akifuatana na afisa kutoka Sekretarieti ya Vatican, watasafiri kwenda Beijing, kama mjumbe wa Baba Mtakatifu Francisko". Kwa mujibu wa maandiko ya taarifa ya Vatican, inasomeka kuwa. “Ziara hiyo inajumuisha hatua zaidi katika utume kwa utashi wa  Papa wa kuunga mkono mipango ya kibinadamu na kutafuta njia ambazo zinaweza kuleta amani ya haki".

Kwa "Hakika sala za wengi kwa siku hizi, za kidini na za kiekumeni, ni sababu zaidi ya kutafuta zawadi ya amani ambayo ni zawadi kwa kila mtu, kutoka kwa kila mtu na ambayo kila mtu anapaswa kuipata". Hayo yalikuwa ni maoni yake mwenyewe Kardinali Zuppi, mara baada ya kufunguliwa rasmi  tukio la taarifa hiyo ya safari mpya, huku akisema kukabiliana na hatua hii kwa matumaini ya kuweza "kufuma mtandao mgumu wa amani."

Kardinali  Zuppi alizungumza hayo akiwa Berlin nchini Ujerumani ambako amekuwako tangu tarehe 11 Septemba 2023, katika mkutano uliohamasishwa  na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ukiongozwa na mada:  “Bidii ya amani” uliowaona viongozi wa dini kuu za ulimwengu, pamoja na wawakilishi wa siasa na utamaduni kutoka  nchi 40. Miongoni mwao, kulikuwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Bwana Antonio Tajani ambaye Kardinali huyo alikuwa na mazungumzo marefu ya faragha tarehe 11 Septemba 2023 mchana katika Ubalozi wa Italia.

Mjumbe wa Papa Beijing-China
12 September 2023, 17:51