Tafuta

Dakika moja ya Picha kwa siku ya 3 ya Papa Nchini Mongolia

Siku yake ya 3 ya Papa Francisko akiwa Mongolia imeanza na mkutano wa kiekumeni na kidini katika Ukumbi wa mchezo wa Hun;amesalimiwa na kiongozi wa kituo cha Wabudha wa Mongolia,ujumbe wa kiorthodox kwa viongozi 11 wa kidini na hatimaye Misa Takatifu ndani ya Nyika kubwa.Nchin

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika siku yake ya Tatu ya Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 3 Septemba 2023, katika misa kwenye Uwanja wa Nyika huko Ulaanbaatar, ilikuwa karibu kumalizika, ambapo kimya kilitanda wakati Papa aliponyoosha mikono yake, kabla ya kutamka shukrani zake kwa Kadinali Giorgio Marengo, akiwafanya wakaribie makardinali wawili John Tong Hon na Stephen Chow hasa aliyestaafu na askofu wa sasa wa Hong Kong, ambaye ni Kardinali mteule atakaye pokea kofia katika Baraza la Makardinali tarehe 30 Septemba 2023. Papa alisema: "Hawa maaskofu wawili, mstaafu wa Hong Kong na Askofu wa sasa wa Hong Kong.

Makardinali wa China
Makardinali wa China

Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo aliwashika mkono wote wawili, ambao wamekuwepo kwa siku hizi katika hafla zote za ziara ya Kipapa nchini Mongolia na kuwatikisa akisema: "Ningependa kuchukua fursa hii, mbele ya hawa maaskofu ndugu wawili, Mstaafu wa Hong Kong na Askofu wa sasa wa Hong Kong, kutuma salamu za dhati kwa watu mashuhuri wa China. Ninatuma salamu zangu nzuri kwa wote: msonge mbele kila wakati, msonge mbele kila wakati! Na kwa Wakatoliki wa China: Ninawaomba muwe Wakristo wema na raia wema. Kwenu nyote, asante." Kwa njia hiyo ukimya ulivunjwa na kwaya ya "Viva il Papa!" Wa kwanza kuizindua walikuwa wanawake wawili kutoka Hong Kong wakipeperusha bendera nyekundu ya China. Akiwatazama na Wachina wengine wapatao 200 waliofika Ulaanbaatar wengine  kwa treni, kwa ndege na kwa gari kutoka China Bara, lakini pia kutoka Macao na Taiwan, Papa  kwa hiyo alizindua wito kwa wamini wote katika nchi ya Asia.

Papa akiwa amewashikilia mikono makardinali wa China
Papa akiwa amewashikilia mikono makardinali wa China

Baba Mtakatifu akiendelea amesema “Asante, mwadhama (akiwa na maana ya Kardinali G Marengo aliyekuwa amemaliza kutoa shukrani kwa Papa), kwa maneno yako mazuri, na asante kwa zawadi yako! Ulitaja kwamba katika siku hizi umeweza kuhisi jinsi watu wa Mungu nchini Mongolia wanavyopendwa moyoni mwangu. Hiyo ni kweli: nilianza hija hii kwa hamu kubwa, nikiwa na shauku ya kukutana nanyi nyote na kuwafahamu. Sasa ninamshukuru Mungu kwa ajili yako, kwani, kupitia wewe, unapenda kutumia kilicho kidogo kufikia mambo makubwa. Asante, kwa sababu ninyi ni Wakristo wazuri na raia waaminifu. Msonge mbele, kwa upole na bila woga, mkijua ukaribu na faraja ya Kanisa zima, na zaidi ya yote macho ya huruma ya Bwana, ambaye hasahau mtu yeyote na kumtazama kila mmoja wa watoto wake kwa upendo.

Kardinali Marengo akimshukuru Papa ujio wako baada ya misa Takatifu
Kardinali Marengo akimshukuru Papa ujio wako baada ya misa Takatifu

Ninawasalimu ndugu zangu maaskofu, mapadre, wanaume na wanawake watawa, na marafiki wote ambao wamekuja hapa kutoka nchi mbalimbali, hasa kutoka sehemu mbalimbali za bara kubwa la Asia, ambako nimejivunia kufika. Ninawakumbatia nyote kwa mapenzi makubwa. Ninawashukuru sana wale wote ambao walisaidia Kanisa mahalia kwa usaidizi wao wa kiroho na kimwili. Katika siku hizi, wajumbe muhimu wa Serikali wamekuwa wakihudhuria kila tukio. Namshukuru Rais na Mamlaka kwa ukaribisho na ukarimu wao, na kwa maandalizi yote yaliyofanywa. Nilihisi mara ya kwanza urafiki wako wa jadi; Asante!

Ishara ya Upendo wa Papa kwa viongozi wa Kanisa la China
Ishara ya Upendo wa Papa kwa viongozi wa Kanisa la China

Pia ninatoa salamu za uchangamfu kwa kaka na dada zetu wa madhehebu mengine ya Kikristo na dini nyinginezo. Na tuendelee kuwa karibu zaidi katika udugu, kama mbegu za amani katika ulimwengu ulioharibiwa vibaya na vita na migogoro mingi. Shukrani zangu za dhati vile vile ziwaendee wale wote ambao wamefanya kazi, kwa bidii na kwa muda mrefu, kuifanya Safari yangu iwezekane na kufanikiwa, na kwa wale wote walioitayarisha kwa maombi yao. Ulitukumbusha kwamba katika lugha ya Kimongolia neno "Asante" linatokana na kitenzi ‘kufurahi’. ‘Asante’ yangu inahusiana kikamilifu na ufahamu huu wa ajabu wa lugha ya ndani, kwa kuwa imejaa furaha. Ni ‘Asante’ kubwa kwa watu wa Kimongolia, kwa zawadi ya urafiki ambayo nimepokea siku hizi, kwa uwezo wenu wa kweli wa kuthamini hata mambo rahisi zaidi ya maisha, kuhifadhi kwa busara uhusiano na mila, na kukuza kila siku maisha kwa uangalifu na umakini.

Waamini katika maadhimisho ya misa
Waamini katika maadhimisho ya misa

Misa yenyewe ni njia ya kutoa shukrani: “Ekaristi”. Kuadhimisha Misa katika nchi hii kulinikumbusha sala ambayo Padre Mjesuit Pierre Teilhard de Chardin alitoa kwa Mungu miaka mia moja iliyopita, katika jangwa la Ordos, si mbali na hapa. Yeye aliomba kwamba: “Mungu wangu, ninasujudu mbele ya uwepo wako katika ulimwengu ambao sasa umekuwa moto hai: chini ya safu za kila kitu nitakachokutana nacho siku hii, yote yanayonipata, yote ninayopata, hamu yangu ni wewe, ninakungoja”. Padre Teilhard de Chardin alikuwa akijishughulisha na utafiti wa kijiolojia. Alitamani sana kuadhimisha Misa Takatifu, lakini alikosa mkate na divai. Kwa hiyo alitunga “Misa juu ya Ulimwengu”, akieleza utoaji wake kwa maneno haya: “Pokea, Ee Bwana, jeshi hili linalokumbatia yote, ambalo uumbaji wako wote, ukiongozwa na sumaku yako, unakupa katika mapambazuko ya siku hii mpya.”  Sala kama hiyo tayari ilikuwa imepata sura ndani yake alipotumikia akiwa mbeba machela kwenye mstari wa mbele wakati wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu.

Waamini wakiwa wanasali
Waamini wakiwa wanasali

Padre huyu, ambaye mara nyingi hakueleweka vizuri, aligundua kwamba “Ekaristi kila mara kwa namna fulani inaadhimishwa kwenye madhabahu ya ulimwengu” na ni “kitovu cha uhai cha ulimwengu, kiini cha upendo na maisha yasiyoisha” (Laudato Sì, 236), hata katika nyakati kama zetu, zilizo na mizozo na vita. Basi, na tusali siku hii kwa maneno ya Padre Teilhard de Chardin: “Neno lenye kung’aa, Nguvu inayowaka, wewe unayefinyanga mambo mengi ili kuyatia uhai, ninakuomba, uweke juu yetu mikono yako, yenye nguvu mwenye kujali, aliye kila mahali.” Kaka na dada wapendwa wa Mongolia, asante kwa ushuhuda wenu. Bayarlalaa! Asante! Mungu awabariki. Mko moyoni mwangu, na moyoni mwangu mtabaki. Nikumbuke, tafadhali, katika maombi yenu na katika mawazo yenu. Asante.”

Hata hivyo kuhusiana na tendo la Papa kuwaonesha makardinali wawili, Papa Francisko  alisema tena asante akiwa ameshikilia mikono yake Kardinali Chow kwa nguvu. Hata hivyo kutakuwa na makadinali watatu wa Hong Kong pia kwa kuzingatia aliyestaafu Joseph Zen ambapo ni moja ya kesi adimu za makadinali watatu ambao bado wanaishi katika jimbo moja. Papa Francisko alikuwa tayari amehutubia watu wa China maneno sawa na hayo mnamo tarehe 23 Mei 2023 mwishoni mwa katekesi  wakati, akikumbuka Siku ya Dunia ya Kuombea Kanisa Katoliki nchini China, ambayo inafanya maadhimisho ya Sikukuu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo, inayoadhimshwa katika Madhabahu ya Mama  Yetu wa Sheshan huko Shanghai. Wakati huo alisema: “Katika hali hii ningependa kuwahakikishia kumbukumbu na kueleza ukaribu wangu kwa kaka na dada zetu nchini China, nikishiriki furaha zao na matumaini yao. Kisha Papa alitoa wazo la kipekee kwa wale wote wanaoteseka, wachungaji na waamini, ili katika ushirika na mshikamano wa Kanisa la kiulimwengu waweze kupata faraja."

Waamini waliudhuria misa
Waamini waliudhuria misa

Kama ilivyotajwa, Wachina wapatao 200 wamekuja jijini Ulaanbaatar siku hizi. Walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika sherehe ya kukaribisha huko kwenye uwanja wa  Sükhbaatar mnamo tarehe 2 Septemba 2023 iliyokuwa tarehe ya kwanza ya safari, rasimi ya Papa, waamini hao waliwambia waandishi wa habari kwamba walitaka kushiriki katika tukio hilo na baadhi, walisema, kuwa walipata shida fulani pia. Bado wengine hawakutaka kutaja jina au asili. Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Yosefu huko Hong Kong walipanga safari ya kwenda Mongolia miezi kadhaa iliyopita ili kuendana na ziara ya Papa. Mtu mmoja alisema kuwa aliondoka kuja Mongolia ili kuonesha: “kwamba sisi sote ni Kanisa moja, kwamba tunampenda Papa, kwamba na yeye aanatupende  na kuipenda China.”

Papa alitoa shukrani mara baada ya misa Takatifu 3 Septemba 2023
03 September 2023, 19:58