Tafuta

2023.09.22 Balozi S.E. Andrii Yurash, wa Ukraine katika anayewakilisha Nchi yake Vatican akiwa na Papa Francisko. 2023.09.22 Balozi S.E. Andrii Yurash, wa Ukraine katika anayewakilisha Nchi yake Vatican akiwa na Papa Francisko.  (Vatican Media)

Balozi wa Ukraine Yurash ampatia Papa mdoli wa dubu kuashiria

Andrii Yurash akipokelewa na Papa Francisko katika Jumba la Kitume,alimpa mdoli kutokana na roketi ya Urussi kugonga nyumba mnamo Januari huko Dnipro,ambayo ilisababisha vifo vya watu 46,wakiwemo watoto watatu.Mdoli wa Dubu uliopatikana kati ya vifusi,hakurekebishwa lakini imekuwa zawadi kama majeraha na ishara ya mateso ya watu wa Ukraine.

Vatican News

Mdolimkubwa wa Dubu, ukiwa na jeraha kwenye makucha yake ya kulia, ulioshonwa na kuchomwa kwa ajili ya kumbukumbu ya watoto wote wa Kiukraine ambao sasa hawataweza tena kucheza na mnyama aliyejaa kwa sababu maisha yao machanga yaliingiliwa na roketi au kombora. Ni zawadi ya mfano wa hali ya juu ambao asubuhi tarehe 22 Septemba 2023, Balozi wa Ukraine anayewakilisha Nchi yake mjini Vatican, alimkabidhi Baba Mtakatifu Francisko aliyekutana naye kwenye jumba la Kitume tarehe 22 Septemba 2023. Huyo alikuwa ni mmoja kati ya wale aliokutana nao  Papa, mapema asubuhi kabla ya alasiri kuanza ziara yake ya 44 ya kitume huko Marsiglia Kusini mwa Ufaransa  22-23 Septemba katika fursa ya  kufunga Mikutano ya Mediterania.

Baba Mtakatifu kwa njia hiyo akiwa na mwanadiplomasia na  mwakilishi wa Ukraine mjini Vatican  tangu  mwezi Aprili 2022, karibu mwezi mmoja na nusu baada ya shambulio la kwanza la Urussi dhidi ya Kyiv, alizungumza naye kwa takriban saa moja kwenye Ukumbi wa Maktaba ya Kitume, mbele ya Mfransiskani wa Kiukreni kama mtafsiri. Balozi  wa Ukraine Andrii Yurash alimletea Papa maneno ya kupendeza hasa ya shukrani kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje, Dmytro Kuleba.

Papa akutana na Balozi wa Ukraine anayewakilisha Nchi yake mjini Vatican
Papa akutana na Balozi wa Ukraine anayewakilisha Nchi yake mjini Vatican

Vita na mapendekezo ya amani kwa upande wa Ukraine yalikuwa, kwa kawaida, mada kuu ya mazungumzo, pamoja na utume wa Kardinali Matteo Zuppi ambao ulimwona kama mjumbe wa amani huko Kyiv, Moscow, Washington na hivi karibuni, pia Beijing nchini China. Balozi alitoa shukrani zake kwa mpango huu wa Papa, pamoja na maneno ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, ya tarehe 20 Septemba  2023 katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Pia kulikuwa na kutajwa kwa shambulio kubwa la siku tatu zilizopita kwenye ghala huko Lviv ambalo lilikuwa na takriban tani 300 za misaada ya kibinadamu na kuharibiwa na moshi. Balozi huyo pia alikumbuka kumbukumbu ya miaka 90 ya janga la mauaji ya kimbari ya Holodomor ambalo linakumbukwa kila Novemba ya kila mwaka

Wakati wa kubadilishana zawadi Papa na Balozi Andrii Yurash wa Ukraine
Wakati wa kubadilishana zawadi Papa na Balozi Andrii Yurash wa Ukraine

Kwa hiyo mazungumzo na viongozi hawa yalimalizika kwa utoaji wa zawadi maalum: dubu kutoka kwa nyumba iliyoharibiwa mnamo Januari 14 huko Dnipro, jiji la mashariki mwa Ukraine, na roketi ya Kirusi. Jengo lilipigwa moja kwa moja katika shambulio hilo: watu 46 waliuawa, wakiwemo watoto watatu; wengine 75 walijeruhiwa, kati yao 13 watoto. Dubu ilipatikana karibu kabisa kati ya vifusi, na hivi karibuni ikawa moja ya alama na ushahidi wa nyenzo wa mateso ya watu wa Kiukreni.

Andrii Yurash alikuwa amepokea hiyo Dubu tangu Juni na alikuwa bado akingojea kuikabidhi kwa Papa jinsi ilivyo, bila urejesho wowote, lakini bado ikiwa na ishara zilizoripotiwa wakati wa mkasa huo. Mwanadiplomasia huyo aliandamana na zawadi hiyo na baadhi ya picha zinazoonesha mnyama huyo aliyejazwa vitu mara baada ya kulipuliwa na bomu: akiwa ameketi, kichwa chake kikitazama chini, kimezingirwa na uharibifu. Picha ambazo zilisambazwa sana nchini Ukraine. Papa Francisko alijibu kwa kutoa zawadi za Rozari na kwa uhakika kwamba ukaribu wake na sala zake hazitakosekana kwa ajili ya Ukraine na idadi ya watu ambayo sasa amewakumbuka zaidi ya mara mia kama "wanaoteswa" katika kila tamko la umma.

22 September 2023, 12:57