Siku ya hupashanaji habari 2024:Akili bandia na hekima ya moyo:kwa mawasiliano kamili ya binadamu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Akili bandia na hekima ya moyo:kwa ajili ya mawasiliano kamili ya binadamu ndiyo Mada ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya 58 ya Siku ya Kimataifa ya Hupashanaji habari kijamii itakayofanyika tarehe 12 Mei 2024 ambayo imetangazwa Ijumaa tarehe 29 Septemba 2023 ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Malaika wakuu Walinzi, Gabrieli, Rafaeli na Mikaeli. Katika maelezo ya mada ya Ujumbe huo ni kwamba Mageuzi ya mifumo ya akili bandia hufanya iwe ya asili zaidi kuwasiliana kupitia na kwa mashine, kana kwamba imekuwa ngumu kutofautisha kati ya mawazo, na lugha inayotolewa na mashine na ile ya wanadamu.
Kama ilivyo kwa mapinduzi yote, hili la msingi katika akili bandia, pia, linaleta changamoto mpya za kuhakikisha kuwa mashine hazichangii mfumo mkubwa wa upotoshaji na ule wa kuongeza upweke kwa wale ambao tayari wako peke yao, na kutunyima uchangamfu kwamba mawasiliano kati ya watu yanaweza kutolewa. Kwa hiyo ni muhimu kuongoza akili bandia na kanuni zake, ili kwa kila mtu apate mwamko wa kuwajibika wa matumizi na maendeleo ya aina hizi tofauti za mawasiliano zinazoendana na mitandao ya kijamii na Inteneti. Ni muhimu kwa mawasiliano kuelekezwa kuelekea maisha kamili ya mwanadamu.