Tafuta

2023.08.21 Papa amekutana na Uwakilisha wa Baraza la Kilataifa la Wanasheria wa Ufaransa. 2023.08.21 Papa amekutana na Uwakilisha wa Baraza la Kilataifa la Wanasheria wa Ufaransa.  (Vatican Media)

Papa kwa wanasheria:Kizazi cha vijana wana haki ya kupata sayari nzuri!

Papa amekutana na ujumbe wa wanasheria kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ulaya jijini Vatican na kueleza marajio:“Ninaandika sehemu ya pili ya Laudato si'.”Papa amekemea tabia ya kudai haki zaidi na zaidi za mtu binafsi:“Bila utafutaji wa ukweli kuhusu mwanadamu,kulingana na mpango wa Mungu,kila mtu anakuwa kipimo chake mwenyewe.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Papa Francisko Jumatatu tarehe 21 Agosti 2023  amekutana mjini Vatican na Uwakilishi wa Wanasheria tofauti kutoka Nchi mbali mbali wa Baraza la Umoja wa Ulaya waliotia saini ya Wito wa Vienna  mnamo tarehe 11 Juni ambapo ulikuwa unawaalika Nchi wanachama wa Baraza, kujikita zaidi kwa ajili ya Sheria na uhuru wa haki. Wito huo ulikuwa unajikita katika Muktadha wa Ulaya ya sasa, ambayo chini ya mtazamo mwingi ni ngumu kwa sababu pamoja na mengine kuna vita visivyo na maana nchini Ukraine, amesema Papa Francisko.

Papa Francisko na Manasheria katika mkutano 21 Agosto 2023
Papa Francisko na Manasheria katika mkutano 21 Agosto 2023

Papa Francisko amewashukuru Waasheria hawa kwa mchango muhimu ambao wanautoa kwa ajili ya kuhamasisha demokrasia na kuheshimu uhuru na hadhi ya binadamu. Katika  nyakati za mgogoro wa kijamii, kiuchumi, kiitikani na usalama zinachangamotisha deokrasia za magharibi kujibu kwa dhati, kwa kubaki lakini daima waaminifu wa misingi yao: Misingi ya kupata kila wakati na ambayo inahitaji ulinzi mkubwa. Sio hiyo tu lakini hata hivyo migogoro ya asili ya hatarishi dhidi ya uhuru na Sheria ya Nchi katika umbu la demokrasia. Kwa hakika, dhana potofu ya maumbile ya mwanadamu na ya mwanadamu inaenea zaidi na zaidi, dhana ambayo inadhoofisha ulinzi wao wenyewe na ambayo polepole inafungua unyanyasaji mkubwa chini ya kivuli cha wema.

Kwa hiyo Baba Mtakatifu anabainisha kwamba inahitaji kukumbusha kuwa msingi wa hadhi ya mtu binadamu inakaa katika asili yake ya kimungu, ambayo kwa hiyo inakataza ukiukwaji wowote; na upitaji mipaka huu unahitaji kwamba, katika kila shughuli ya mwanadamu, mtu huyo amewekwa katikati na asijikute kwenye huruma ya mitindo na nguvu za wakati huu. Kwa hakika Ulaya ambayo haina uwezo tena wa kujifungulia ukuu wa aliye juu wa maisha, ni Ulaya ambayo pole pole inahatari ya kupoteza roho yake na hata ile roho ya ubinadamu ambayo hata hivyo inapenda na kutetea. Heshima kwa haki za binadamu inaweza kuhakikishwa na utawala wa sheria unaweza kupata uthabiti hadi tu watu wabaki waaminifu kwa mizizi yao ambayo inalishwa na ukweli, ambao unaunda damu ya maisha ya jamii yoyote inayotaka kuwa huru kweli kweli, ubinadamu na kuunga mkono (Rej. Hotuba kwa Baraza la Ulaya, 25 Novemba 2014). Bila utafutaji huu wa ukweli kuhusu mwanadamu, kulingana na mpango wa Mungu, kila mtu anakuwa kipimo chake mwenyewe na cha matendo yake mwenyewe.

Kwa sasa kiukweli, kuna mwelekeo wa kudai haki zaidi na zaidi za mtu binafsi bila kutilia maanani ukweli kwamba kila mwanadamu ameunganishwa na muktadha wa kijamii ambamo haki na wajibu wake unaunganishwa na zile za wengine na kwa manufaa ya wote ya jamii yenyewe (tazama Hotuba kwa Bunge la Ulaya). Kutokuelewana kwa dhana ya haki za binadamu na unyanyasaji wao wa kipingamizi kunaweza kuwapeleka watu kwenye katika uimla wa ujamaa, [...] [kwa] misingi ya kupinga historia, maadili bila wema, akili zisizo na hekima” (Rej. Evangelii gaudium, 231), ambapo utawala wa sheria haungekuwa tena katika huduma ya mwanadamu ambaye amepotoshwa na kudanganywa kulingana na masilahi ya kiuchumi na kiitikadi. Papa Francisko anawapongeza kwa  wito wake, kati mantiki ambayo yanapaswa kuwekewa maanani katika taaluma yao ya kukumbusha misingi mikuu ya siri ya kitaaluma ambayo wanajutia ukiukwaji huo katika baadhi ya Nchi Wanachama. Papa anatambua na kishirikisha wasiwasi wao na kuwatia moyo katika matendo yao.

Papa amekutana na mawakilis wawaakilishi wa kitaifa
Papa amekutana na mawakilis wawaakilishi wa kitaifa

Ni muhimu kwamba nafasi za kujiamini zihifadhiwe katika jamii zetu ambapo watu wanaweza kujieleza na kuweka mizigo yao. “Hii ni Muhimu katika kanisa siri ya maungamo, lakini wao wawana hata nafasi hiyoo, mahali ambapo mtu anaweza kusema ukweli kwa wakili wake, ili aweza kusaidiwa na kuondokana”. Papa ameelezea hata unyeti wake juu ya  utunzaji ambao wao wanauelekeza katika nyumba yetu ya  pamoja na katika jitihada ya kushirikishana katika mfumo wa udhibiti wa ulinzi wa mazingira. Amesema wasisahau kamwe kuwa kizazi cha vijana wana haki ya kupata kutoka kwetu ulimwengu mzuri na ambao unaweza kuishi, na kwayo lazima kuwekeza uwajibikaki mkubwa mbele ya kazi ya uumbaji ambayo tulipokea kutoka katika mikono mikarimu ya Mungu. Papa Francisko amewashukuru kwa mchango wao.  “Aidha amebainisha jinsi ambayo yuko anaandika Sehemu ya Pili ya Laudati si kwa ajili ya kusasisha matizo ya sasa.”Baba Mtakatifu mehitimisha kwa kupyaisha akiwatia moyo mawakili hawa ili waendelee na zoezi hilo la kitaaluma, wakiielekeza katika huduma ya kweli na ya haki, na  ulazima wa kutafuta  amani katika ulimwengu na maelewano katika jamii zetu. Bikira Maria na Mtakatifu Ivo anawalinde na kuwasaidia. Kwa moyo amewabariki.

Papa na wanasheria
21 August 2023, 15:21