Tafuta

Roho ya Marehemu Luca Re Sartù kijana mwenye umri wa miaka 24 huko Valese Italia apumzike kwa amani Roho ya Marehemu Luca Re Sartù kijana mwenye umri wa miaka 24 huko Valese Italia apumzike kwa amani 

Papa ampigia simu mama yake Luca,aliyefariki aliporejea kutoka WYD

Baba Mtakatifu Francisko alimpigia simu mama wa kijana mwenye umri wa miaka 24,ambaye alikufa kutokana na ambukizo la bakteria siku chache baada ya kushiriki siku ya Vijana (WYD) huko Lisbon. skofu aliyeadhimisha misa alikutana na Mwanamke huyo akamuomba amshukuru Baba Mtakatifu kwa kumfariji.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mazishi ya Luca Re Sartù, muhuishaji wa kituo katoliki mwenye umri wa miaka 24, aliyekuwa na shughuli nyingi sana katika parokia, ambaye alifariki aliporejea kutoka Siku ya Vijana Duniani nchini Ureno, yaliadhimishwa tarehe 18 Agosti 2023 huko Marnate jimbo Kuu la Milano. Kumbukumbu ya wanafamilia imebainisha kuwa alikuwa ni mfano mzuri kwa kila mtu ambaye alipata bahati ya kumjua na kukutana naye. Kijana Luka alifariki tarehe 11 Agosti baada ya kukimbizwa kwenye Hospitali mbili kutokana na kuambukizwa na bakteria siku chache baada ya kushiriki siku ya Vijana (WYD) huko Lisbon. Askofu aliyeadhimisha misa alikutana na Mwanamke huyo akamuomba amshukuru  Baba Mtakatifu kwa kumfariji.

Kwa hiyo maombi na sala kwa ya siku ya WYD yalikuwa yakisikika kwa vijana walioudhuria mazishi hayo. Kufuatia na kifo chake Papa Francisko  alimpigia simu mama yake ambayo hakutarajia mama huyo. Na alipata hisia kali  mwanamke huyo kwa mujibu wa Askofu Luca Raimondi ambaye aliongoza ibada ya mazishi Ijumaa 18 Agosti  2023 na ambaye amehojiwa na vyombo vya habari  vya Vatican/Vatican News.

Askofu Raymond alisema kuwa maneno ya mama huyo yalikuwa ni kwamba atakapomwona, amshukuru Baba Mtakatifu kwa sababu kijana wake alikuwa wa Kanisa na mwema wa hali ya juu. Mama huyo alimweleza Askofu jinsi alivyo lia pamoja na Baba Mtakatifu na zaidi ya yote  alihisi kuwa kama baba. "Alinifariji kana kwamba alikuwa baba yangu”. Alisema mama huyo. Kwa  njia hiyo Mama alivutiwa sana na  tendo  hilo la Baba kumfariji kwa kumpiga simu.

Papa ampigia simu Mama mmoja kupa pole ya kufiwa na kijana wake
19 August 2023, 17:18