Tafuta

Mkesha wa WYD,Papa kwa vijana:eneza popote furaha ya kimisionari

Kwa mujibu wa Mamlaka mahalia ni kwamba karibu watu milioni moja na nusu walikuwa kwenye hifadhi ya Tejo ya Lisbon katika Mkesha na Papa.Akizungumza nao,aliwaomba watambue kuwa furaha ni ya kimisionari hivyo waipeleka kila mahali na wawasaidie wale wanaonguka wasibaki chini.Onyo:“Msiogope kushindwa,kwani kushindwa ni unapokosa nguvu ya kuinuka tena.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Mkesha wa Jummosi tarehe 5 Agosti 2023 kwenye hifadhi  ya Graca huko Tejo, karibu na jiji la Lisbon iliwakaribisha vijana wapatao milioni moja nusu kadiri ya taarifa kutoka Mamlaka ya nchi, ambapo mkesha huo ulikuwa umegawanyika katika sehemu kubwa mbili. Ya kwanza ilikuwa inahusu dansi ya vijana, na sehemu ya pili ilijikita kuabudu Ekaristi Takatifu. Mwanzo wa Mkesha ulianza karibia saa 2.45 za usiku na kuudhuriwa na wahusika wakuu vijana, mahujaji, maaskofu, makardinali, mapadre mashemasi, baadhi ya mamlaka, wageni waalikwa  na watu wengine wengi wa Ureno na wageni kutoka nchi za Nje.

Utamadunisho wakati wa mkesho huko Tejo, Lisbon
Utamadunisho wakati wa mkesho huko Tejo, Lisbon

Ilipendeza kwa wengi kuona ni jinsi gani kulikuwa na vijana ambao walikuwa katika jukwaa wakicheza,  nyimbo kwa kuonesha vitendo ambavyo viliendana na wimbo na  kila kitu kilikuwa na maana hata viziwi  walioweza kutambua ni nini wanaimba. Katika mkesha huo sehemu ya kwanza ilisimulia historia ya kukutana katika mabadiliko. Kupitia muziki na densi ya kisasa, imesimulia historia ya mtu ambaye alijiruhusu kupingwa na Mungu kwa jinsi hiyo ilibadilisha maisha yake, kwa kuambukiza kila mtu aliyekutana naye. Kwahiyo aliye msafiri yeyote, kuona huko kunaweza kuamsha shukrani kwa ajili ya uhusiano wake pamoja na Mungu au kiu ya kuuimarisha. Kwa njia moja au nyingine, kusudi la Mkesha umekuwa ni kuimarisha ndani ya kila mtu hamu ya kuendelea kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu na kuwatumikia wengine watakaporudi nyumbani.

Kijana kutoka Msumbiji ametoa ushuhuda wake
Kijana kutoka Msumbiji ametoa ushuhuda wake

Mkutano uliofanywa katika sehemu ya kwanza ya mkesha ulifanywa kuwa halisi na thabiti katika sehemu ya pili hasa ile ya kuabudu Sakramenti Takatifu. Hiyo na  kauli mbiu ya Siku ya  tukio hilo ilionnesha ulinganifu kati ya kile kinachowakilishwa na historia ya Mama Yetu. Mkutano (Tamko) ulibadilisha maisha ya Maria na, kwa hivyo, historia ya ubinadamu. Ndiyo au tazama mimi hapa ya Maria kwa pendekezo la Mungu la upendo ambalo kwa hakika hututia moyo wa kufanya vivyo hivyo: kujitoa kabisa kwa Bwana, kumkabidhi maisha yetu yote, kukataa mipango, miradi na dhamana, kuwa vyombo vyake katika historia  hii ya upendo wa Mungu kwa kila mmoja wetu.

Jukwaa la Altare huko Tejo, Lisbon
Jukwaa la Altare huko Tejo, Lisbon

Waimbaji, wapiga vyombo na waliocheza  walikuwa ni mchanganyiko kutoka nchi 23: Argentina, Australia, Brazil, Chile, Colombia, Hispania, Ufilipino, Ufaransa, Guatemala, Iraq, Italia, Malaysia, Mexico, Nigeria, Slovakia, Puerto Rico, Ureno, Jamhuri ya Dominika, Venezuela, Vietnam na Zimbabwe.  Mara baada ya hayo yote, ilifuatia hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko na kufuatiawa na kuabudu.

Wakati wa Mkesha
Wakati wa Mkesha

Katika hotuba ya Baba Mtakatifu kwa vijana hao amesema kusema kuwa “Jinsi gani livyo nzuri kuwaona! Asante kwa kusafiri, kwa kutembea, asante kwa kuwa hapa! Na nadhani hata Bikira Maria alilazimika kusafiri kwenda kumwona Elizabeti: “Akaondoka akaenda kwa haraka ( Lk 1:39. Mtu anaweza kujiuliza: kwa nini Maria aliamka na kwenda kwa binamu yake haraka? Bila shaka, yeye tu alijifunza  kwamba binamu ni mjamzito, lakini hata yeye pia; kwa hiyo ni kwa nini basi haende ikiwa hakuna mtu aliyemuomba? Maria anatimiza ishara isiyoombwa na isiyo ya lazima; Maria alikwenda kwa sababu anapenda na anayependa   huruka, hukimbia kwa furaha. Hivi ndivyo upendo unavyotufanyia. Furaha ya Maria ni mara mbili, kwanza  alikuwa ametoka tu kupokea tangazo la Malaika kwamba angemkaribisha Mwokozi, na pia habari kwamba binamu yake alikuwa mjazito”.

Papa akiwa katikati ya waliotamadunisha jukwaani na altareni
Papa akiwa katikati ya waliotamadunisha jukwaani na altareni

Inashangaza: badala ya kujifikiria mwenyewe, anafikiria mwingine. Kwa nini? Kwa sababu furaha ni mmisionari, furaha si ya mtu mmoja, ni kuleta kitu. Ninawauliza: ninyi, mlio hapa, mliokuja kukutana na kila mmoja, kupata ujumbe wa Kristo, kupata maana nzuri ya maisha, je, mtauweka kwa ajili yenu wenyewe au mtawapelekea wengine? Nini unadhani; mnafikiria nini? Sisikii… Ni kwa ajili ya kuwapelekea wengine. Kwa sababu furaha ni mmishonari. Hebu sote turudie kwa pamoja: furaha ni mmisionari. Kwa hivyo ninapeleka furaha hii kwa wengine.” Baba Mtakatifu amesema kuwa “Lakini furaha hii tuliyo nayo, wengine wametutayarisha kuipokea. Kwa hiyo, hebu tutazame nyuma juu ya yote ambayo tumepokea: yote haya yameweka mioyo yetu kuwa na kila mtu".

Wakati wa mkesha
Wakati wa mkesha

Kwa kukazia tena Papa amesema "Tukitazama nyuma, kumekuwa na watu ambao wamekuwa mwali wa nuru katika maisha yetu kuanzia na  wazazi, babu na bibi, marafiki, mapadre, watawa, makatekista, watumbuizaji, walimu… Wao ndio mizizi ya furaha yetu. Sasa tunyamaze kwa muda na kila mmoja awafikirie wale waliotuamini maishani, ambao ndio chimbuko la furaha”. Papa aliwaomba wakae kimya." Je mmeona? Mmeona nyuso na  historia? Furaha hii inayotoka kwenye mizizi ndiyo tunapaswa kutoa, kwa sababu tuna mizizi ya furaha. Na vivyo hivyo, tunaweza kuwa mizizi ya furaha kwa wengine. Si furaha ya kupita muda, furaha ya kitambo; juu ya yote ni ya kupeleka furaha ambayo inatengeneza mizizi. Baba Mtakatifu kwa kuongezea hotuba yake bila kusoma amesema “Walakini, ninajiuliza: jinsi gani ya kuwa mizizi ya furaha? Huwezi kupata furaha imefungwa kwenye maktaba, hata ikiwa ni muhimu kujifunza, eh?; lakini ni mahali pengine. Haiko chini ya ufunguo. Lazima uitafute furaha, lazima uigundue, lazima uigundue katika mazungumzo na wengine ambayo inatupasa kutoa mizizi hii ya furaha ambayo tumepokea. Na hii wakati mwingine huchosha.

Kipindi cha kuabudi ekaristi
Kipindi cha kuabudi ekaristi

Ninawauliza swali: wakati mwingine mnachoka? Hapana…ndio? Sisikii.” Papa amewauliza, Je, wakati mwingine mnachoka? Fikiria juu ya kile kinachotokea wakati mtu amechoka: mtu hataki kufanya chochote, kama tunavyosema kwa Kihispania: mtu hutupa sponji kwa sababu hataki kuendelea na kisha anakata tamaa, anaacha kutembea na kuanguka. Je, mnaamini kwamba mtu anayeanguka katika maisha, ambaye anakabiliwa na kushindwa, ambaye pia hufanya makosa makubwa, yenye nguvu, kwamba maisha yake yamekwisha? Hapana. Ameuliza swali jingine akitaka jibu: Sisikii… Hapana. Je inabidi nifanye nini? Siwezi kusikia. Kusimama.

Yesu nakuabudi na ninakupenda
Yesu nakuabudi na ninakupenda

Na kuna jambo zuri sana ambalo ningependa kuwaachia leo hii  kama ukumbusho. Wapanda milima ambao wanapenda kupanda milima, wana wimbo mzuri sana unaosema  hivi: “Katika sanaa ya kupanda mlima, cha muhimu sio kutoanguka, lakini sio kubaki chini”. Ni nzuri,” Papa amefafanua. Yeyote anayebaki ameanguka tayari amestaafu kutoka katika maisha, amefunga tumaini, amefunga kwa udanganyifu na anabaki pale alipoanguka. Na tunapomwona rafiki yetu ambaye ameanguka, tunapaswa kufanya nini? Kumwinua, kwa nguvu. Tazama ishara unayofanya wakati  unapopaswa kumwinua mtu  au unapaswa kumsaidia mtu kumwinua: Unamtazama kutoka juu kwenda chini . Ni kesi pekee, tukio la kipekee ambalo unaruhusiwa kumtazama kutoka juu kwenda chini ili kumwinua.

Papa akitoa hotuba yake
Papa akitoa hotuba yake

Baba Mtakatifu Francisko amekazia kuwa “Ni mara ngapi, mtu anaona watu wakitutazama hivyo, juu ya mabega yetu, kutoka juu hadi chini. Inasikitisha. Tukio la pekee, hali pekee ambayo inaruhusiwa kumtazama  mtu ni ... itaje” Papa ameomba: ni hivyo? Semeni kwa Nguvu! Kumsaidia kuamka. Ni kweli, hii ni safari kidogo, ya uvumilivu katika kutembea. Na katika maisha, ili kupata vitu lazima ujizoeze kutembea. Wakati mwingine hatujisikii kutembea, hatujisikii kufanya kazi kwa bidii, tunadanganya kwenye mitihani kwa sababu hatujisikii kusoma na hatupati matokeo. Baba Francisko ameuliza swali jingine kuwa “Sijui kama kuna yeyote kati yenu anapenda mpira wa miguu: Mimi ninaupenda. Lakini nyuma ya goli kuna nini? Mafunzo mengi. Ni nini nyuma ya matokeo? Mafunzo mengi. Na katika maisha siku zote mtu hawezi kufanya anavyotaka, bali kinachotuongoza ni kufanya wito nilionao ndani maana kila mtu ana wito wake. Kutembea; na nikianguka, nainuka au mtu atanisaidia kuinuka; nisibaki nimeanguka; na kufanya mazoezi katika kutembea.”

Bahari ya vijana katika mkesha Agosti 5 huko Tejo, Lisbon
Bahari ya vijana katika mkesha Agosti 5 huko Tejo, Lisbon

Na yote haya yanawezekana, si kwa sababu tunafuata kozi ya kutembea, kwani  hakuna kozi zinazotufundisha jinsi ya kutembea katika maisha, tunajifunza hili, tunajifunza kutoka kwa wazazi wetu, tunajifunza kutoka kwa babu na bibi zetu, tunajifunza kutoka kwa marafiki zetu kwa kupeana mkono. Katika maisha tunajifunza, na hii ni mafunzo ya kutembea. Baba Mtakatifu kwa hiyo amependa kuwaachia vijana hawa katika mkesha huo mawazo haya: “Kutembea na, wakianguka, wasimame tena; kutembea kwa lengo; kufanya mazoezi kila siku ili kuishi. Katika maisha, hakuna kitu cha bure, kila kitu kinalipwa. Kitu kimoja tu ni cha bure: upendo wa Yesu. Kwa hiyo, kwa huru huu tuliyo nayo (upendo wa Yesu) na kwa shauku ya kutembea, tutembee kwa matumaini, tutazame mizizi yetu na kusonga mbele bila hofu, bila woga. Msiogope. Asante. Ciao! Papa amehitimisha.

Hotuba ya Papa wakati wa Mkesho 5 Agosti 2023
06 August 2023, 00:18