Tafuta

2023.06.19 Wanashirika wa Kanoni za Kawaida Laterani na Papa. 2023.06.19 Wanashirika wa Kanoni za Kawaida Laterani na Papa.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ushauri wa Papa:ni busara ya kushirikisha mali za jumuiya na kuepuka muungu pesa

Papa akikutana na Shirika la Kanuni za Kawaida za Mwokozi Mtakatifu sana Laterano wakati wanaadhimisha miaka 200 tangu kuanzishwa aliwashauri wafuate nyota nne katika utume:sala,jumuiya,mali za pamoja na huduma kwa Kanisa huku wakiepuka shetani pesa anayeingia mifukoni.Alitoa onyo wasisengenyane kamwe kwa sababu ni pigo linaloharibu kila kitu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Hivi karibuni Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 19 Juni 2023, alikutana na Shirika la kitawa linaloitwa “Canonici Regolari del Santissimo Salvatore Lateranense” yaani, Wakanoni za Kawaida za Mwokozi Mtakatifu Laterani”, ambalo lilitokana na kuunganishwa mashirika mawili. Katika hotuba yake, akiwatakia matashi mema katika kuadhimisha miaka 200 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo ambalo alisema kuwa asili yao ni ya zamani zaidi kwani lilianza karne ya kumi na tano na lina mizizi yake katika siku za kwanza za Kanisa wakati, kupitia kazi ya wachungaji walioangaziwa, maisha ya kawaida ya makasisi yalianza kuhamasishwa. Hii ni neema kubwa sana, Papa alisisitiza. Kwa hiyo wao ni wa mapokeo ya karne nyingi, yaliyochochewa na jumuiya ya Wakristo wa kwanza  waliojikita mizizi  katika sala, ushirika wa maisha na matumizi ya mali ya jumuiya(Mdo 2:42,47), ili kwamba, kama Mtakatifu Augustino asemavyo, “kuishi ndani ya nyumba na kuwa na nafsi moja na moyo mmoja ili kumfikia Mungu” (Kanuni 1:3). Sala, jumuiya, matumizi ya kawaida ya mali na roho ya huduma kwa Kanisa ndizo Baba Mtakatifu aliwambia kuwa ni nyota   nne ambazo ni  mvuto wa kudumu wa historia yaona  ambazo hazijaisha kamwe na zinazofanya utume wao kuwa mwanga na wa sasa.

Watawa wa Kanoni ya Kawaidia wa Laterano
Watawa wa Kanoni ya Kawaidia wa Laterano

Katika kudadavua hizo nyota Papa alianza na “sala  kwa sababu ni oksijeni ya roho. Usipoomba, utakuwa mungu wako mwenyewe. Ubinafsi wote unatokana na ukosefu wa maombi”.  Papa aliwaomba  wachunguze dhamiri zao, kila mmoja wao na  aseme ni saa ngapi kwa siku ninasali.  Kila moja aliwapatia ushauri kwamba kamwe wasisengenyane kuhusu kila mmoja, kwa sababu masengenyo ni mdudu hatari ambaye anaharibu jumuiya. Jambo jingine lazima kuwa na busara kwa sababu  shetani  huingia kupitia mifukoni, alisisitiza.  Papa alisema wafikirie Yesu aliposema kwamba: “Hamwezi kutumikia mabwana wawili, au kumtumikia Mungu, na Papa aliongeza: “Ningetarajia aseme: au kumtumikia shetani  badala yake hasemi shetani, lakini anasema ‘fedha’, kana kwamba yeye ni mbaya zaidi kuliko shetani”.  Kwa njia hiyo Papa alikazia kusema kuwa hii ni ajabu. Ibilisi daima huingia mifukoni. Na ushauri wa  nne ni kuwa na roho ya huduma kwa Kanisa. Papa alionya watawa hao kuwa wasiishi kwa ajili yao bali kutumikia, na ndizo nyota nne.

Mkutano wa Papa na watawa wa Canonici Regolari Lateranensi
Mkutano wa Papa na watawa wa Canonici Regolari Lateranensi

Karama yao inawataka wawe watu wa kutafakari na wenye bidii kwa wakati mmoja, kwa kujitolea katika maombi na kusoma na pia kwa huduma, tayari kujibu mahitaji ya nyakati zinazobadilika. Mara nyingi wamepata mabadiliko na sikukuu ya miaka mia mbili waliyoadhimisha pia inahusishwa na mojawapo ya haya, wakati, katika wakati wa hali mbaya, waliweza kufanya uchaguzi wa ujasiri, kubadilisha changamoto kuwa fursa ya kuzaliwa upya. Baba Mtakatifu alisema kuwa  walikuwa wakishangaa jinsi ya kuendelea na upya wa maisha yao ya kitawa. Lakini alipenda kuwambia kuwa waache nyota zao nne ziwaongoze. Jina lenyewe la Shirika lao linawachangamotisha: Kanoni za Kawaida za Mwokozi Mtakatifu sana Laterano. Ukweli wa kujitolea kwa Mwokozi unatukumbusha umuhimu wa kusitawisha ukuu wa Kristo kupitia sala. Kisha wana jina la Kanoni na kwamba wanajua vizuri kuwa sio suala la kuwa na  cheo, lakini  ni ishara ya kuwa wa jumuiya. Wanaitwa shirika la kanoni za kawaida, ambazo zimefungwa kwa Kanuni, ambayo inaelezea uaminifu kwa wakfu wao kulingana na nadhiri zao na  juu ya umaskini wote. Hatimaye, jina lao linakufungamanisha na Basilika ya Laterano: hata hii haifanyi kuwa tukio la hali ya juu au kumbukumbu inayoibua mambo ya kale ya utukufu, hapana, bali ni mwaliko wa uaminifu kwa Kanisa, unaoshuhudiwa kimsingi kwa njia ya huduma.

Watawa na Papa
Watawa na Papa

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake aliwaeleza anavyojua  kwamba baadhi yao, mapadre vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wako wanafanya  uzoefu katika miezi ya hivi karibuni ambao, kupitia mikutano, sherehe na ziara muhimu, zinalenga kuwasaidia kujenga mipango na vifungo, na pia kupanua ujuzi wao. Kwao na kwa wote waliokuwapo aliwaeleza waishi tukio hilo kama zawadi, kwa kusikilizana, kutambua katika kila mmoja hazina kwa ajili ya wengine.  Papa aliwashauri wasimuliane na kusikiliza kila mmoja wao, kwa unyofu na uwazi wa moyo, kila mmoja asibaki thabiti katika imani yake, lakini akienenda kwa moyo, kama Mtakatifu Augustino alivyopendekeza kwamba “ Kutembea na mwili ni jambo moja, na lingine tembea kwa moyo: mtu anayetembea na mwili husogea kimwili kutoka sehemu moja hadi nyingine, wale wanaoelekeza mapenzi yao kwa njia tofauti husogea na moyo” (Yohane, 32). Ni kwa moyo unaosonga, wenye nguvu na uliopanuka, tunapokaribisha njia ambazo Roho Mtakatifu anaoneesha. Papa aliwatakia kutoka moyoni mwake, waweze kuendelea vema na aliwabariki huku akizidi kuwashukuru na kuwaomba waendelee kusali kwa ajili yake.

Hotuba ya Papa kwa watawa
01 July 2023, 15:45