Tafuta

Italia imekumbwa na maafa makubwa yanayotokana na mafuriko yaliyojitokeza Kaskazini mwa Italia hususan kwenye mkoa wa Lombardia na Kusini mwa Italia. Italia imekumbwa na maafa makubwa yanayotokana na mafuriko yaliyojitokeza Kaskazini mwa Italia hususan kwenye mkoa wa Lombardia na Kusini mwa Italia.  (ANSA)

Italia Yakumbwa na Maafa Makubwa: Mafuriko na Majanga ya Moto

Hii ni changamoto anasema, Baba Mtakatifu Francisko ya kuweka sera na mbinu mkakati wa muda mrefu na mfupi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, tayari kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote. Baba Mtakatifu anawaweka watu walioguswa na kutikiswa na maafa haya makubwa chini ya ulinzi, tunza na faraja kutoka kwa Bikira Maria. Kwa upande wake, Kardinali Zuppi amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu kwa kuonesha ukaribu wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Italia imekumbwa na maafa makubwa yanayotokana na mafuriko yaliyojitokeza Kaskazini mwa Italia hususan kwenye mkoa wa Lombardia na kwamba, yamepelekea watu watano kupoteza maisha na uharibifu kwa makadirio ya awali wa zaidi ya Euro milioni 40. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Kardinali Matteo Maria Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI, anamwomba, amfikishie salam zake za rambirambi kwa watu walioguswa na maafa haya na kwamba, yuko karibu nao kiroho kwa njia ya sala. Hii ni changamoto anasema, Baba Mtakatifu Francisko ya kuweka sera na mbinu mkakati wa muda mrefu na mfupi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, tayari kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote. Baba Mtakatifu anawaweka watu walioguswa na kutikiswa na maafa haya makubwa chini ya ulinzi, tunza na faraja kutoka kwa Bikira Maria.

Italia imekumbwa na majanga ya moto
Italia imekumbwa na majanga ya moto

Baba Mtakatifu anapenda kuwatia shime wale wote wanaoendelea kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma ya uokoaji na kwa namna ya pekee, Vikozi vya Zima Moto. Mwishoni mwa ujumbe wake, Baba Mtakatifu anapenda kuwapatia baraka zake za Kitume. Kwa upande wake, Kardinali Matteo Maria Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI, kumshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu kwa kuonesha ukaribu wake kwa watu walioguswa na kutikiswa na majanga haya asilia yaliyo sababisha maafa makubwa kwa wat una mali zao. Kardinali Matteo Maria Zuppi anasema, anawataka watu wa Mungu nchini Italia kusimama kidete kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote. Hii ni dhamana shirikishi katika kulinda na kutunza mazingira sanjari na maisha ya watu wote, ili kuacha urithi bora kwa kizazi kijacho!

Papa Maafa Italia

 

29 July 2023, 13:36