Tafuta

Sherehe hii iwe ni fursa kwa waamini kujikita zaidi katika kukuza, kudumisha na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, huku waamini wakijitahidi kuiga mfano wa Watakatifu hawa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu. Sherehe hii iwe ni fursa kwa waamini kujikita zaidi katika kukuza, kudumisha na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, huku waamini wakijitahidi kuiga mfano wa Watakatifu hawa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu.  (Vatican Media)

Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo Mitume! Pyaisheni Imani Yenu Kwa Kristo na Kanisa Lake!

Sherehe hii iwe ni fursa kwa waamini kujikita zaidi katika kukuza, kudumisha na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, huku waamini wakijitahidi kuiga mfano wa Watakatifu hawa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu, kwa maneno, lakini hasa zaidi kwa njia ya matendo adili na manyoofu. Ni siku ya kuonesha upendo, umoja na ukarimu kwa Baba Mtakatifu ili aweze kutenda vyema katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo, Mitume na Miamba wa imani, walioyamimina maisha yao kama sadaka safi na ushuhuda wa upendo na imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake inaadhimishwa na Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 29 Juni.  Baba Mtakatifu Francisko amesema, watakatifu Petro na Paulo, Mitume, walikuwa wamoja, lakini ni watu waliokuwa na taaluma tofauti kabisa. Mtakatifu Petro alikuwa ni mvuvi na muda wake mwingi aliutumia kutengeneza nyavu zake, wakati ambapo Mtakatifu Paulo, Mwalimu wa Mataifa alikuwa anafundisha kwenye Masinagogi. Katika maisha na utume wao, Petro aliwaendea Wayahudi, wakati ambapo Paulo wa Tarso aliyelidhulumu Kanisa, alikutana mubashara na Yesu Kristo Mfufuka akiwa njiani kwenda Dameski, akajiachilia mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na neema na hatimaye akawa ni Mtume na Mwalimu wa Mataifa. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake Jumatano tarehe 28 Juni 2023 amewaambia waamini, mahujaji na wageni kwamba, miili ya watakatifu Petro na Paulo imezikwa mjini Roma, wawe ni chachu ya ari na mwamko mpya wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu na kwamba maisha yao yaliyogeuzwa na kufanana na maisha ya Kristo Yesu, yawe ni chemchemi ya ukuaji na furaha ya Injili kwa watu wote!

Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani.
Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani.

Sherehe hii iwe ni fursa kwa waamini kujikita zaidi katika kukuza, kudumisha na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, huku waamini wakijitahidi kuiga mfano wa Watakatifu hawa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu, kwa maneno, lakini hasa zaidi kwa njia ya matendo adili na manyoofu. Ni siku ya kuonesha upendo, umoja na ukarimu kwa kumwombea Baba Mtakatifu ili aweze kutenda vyema katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.   Katika Ibada ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu Francisko atabariki Pallio Takatifu watakazovishwa Maaskofu wa Majimbo makuu walioteuliwa katika Kipindi cha Mwaka 2022-2023 ambao kwa mwaka huu wa 2023 ni Maaskofu wakuu 32. Pallio takatifu ni kitambaa cha sufi safi kinachotengenezwa na manyoya ya kondoo wachanga; na kinavaliwa na Baba Mtakatifu pamoja na Maaskofu wakuu wa majimbo makuu ya Kanisa Katoliki. Kinavaliwa pia na Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki. Hii ni alama ya Kristo mchungaji mwema aliyesadaka maisha yake kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Pallio takatifu ni alama ya umoja na mshikamano kati ya waamini na Mchungaji wao mkuu, kama Kristo Yesu, anayependa kuwabeba mabegani mwake, ili waendelee kuunganika pamoja naye. Hii ni alama ya umoja wa Maaskofu wakuu pamoja na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Sherehe Miamba
28 June 2023, 17:46