Tafuta

WYD Lisbon 2023: WYD Lisbon 2023:  

Ratiba ya mikutano ya Papa atakayekuwa Ureno kuanzia Agosti 2 hadi 6

Agosti kwa ajili ya toleo la 37 la Siku ya Vijana Duniani imetangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican.Jumamosi 5 mkesha na vijana katika Uwanja wa Tejo pia katika ajenda kuna kutembelea Madhabahu ya Fatima ambapo atasali na vijana wagonjwa.

Na Angella rwezaula, - Vatican.

Siku ya Vijana itafikia kilele jioni, Jumamosi tarehe 5 Agosti 2023 kwa Mkesha pamoja na vijana katika Uwana wa Tejo ya Lisbon, baada ya kutembelea Madhabahu ya Mama Yetu wa Fatima,na kwa Misa Takatifu siku moja baada ya ziara ya Papa nchini Ureno kwa tukio la Siku ya 37 ya Vijana Duniani. Kulingana na ratiba hiyo, iliyotangazwa na Ofisi ya Waandishi wa Habari wa Vatican, tarehe 6 Juni 2023. Kwa hiyo  Baba Mtakatifua Francisko  katika ziara yake hiyo anaterajuwa kutoa hotuba tisa na homilia mbili, kukutana na taasisi, Kanisa mahalia na zaidi ya yote vijana wengi wanaotarajiwa kutoka ulimwenguni kote  kwa tukio hilo.

Jumatano 2 Agosti kuwasili katika Ureno

Papa anatarajia kuondoka saa 1.50 asubuhi siku ya Jumatano tarehe 2 Agosti 2023 kutoka uwanja wa ndege wa Fiumicino wa Roma na atawasili saa 4. 00 asubuhi katika kituo cha anga cha Figo Maduro huko Lisbon. Muda mfupi baadaye, atakaribishwa na Rais wa Jamhuri ya nchi hiyo Marcelo Rebelo de Sousa katika Ikulu ya Kitaifa ya Belèm. Pia katika wilaya ya Belèm, katika kituo cha kiutamaduni, atakutana na mamlaka, mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia. Saa 10.45 jioni katika Ubalozi wa Vatican mkutano na waziri mkuu na saa 11.30 jioni, katika monasteri maarufu ya Jerònimos, ataadhimisha masifu ya jioni pamoja na maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake watawa, waseminari na wachungaji.

Alhamisi tarehe 3 Agosti sherehe za kukaribisha WYD

Siku ya Alhamisi asubuhi,  Papa Francisko atakutana na wanafunzi katika Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno. Kisha ataondoka Lisbon kuelekea Cascais iliyo karibu, ambako atasalimia vijana wa Scholas Occurentes ambao wana makao yao makuu huko. Mchana, kurudi kwa mji mkuu wa Ureno kwa sherehe ya kukaribisha WYD, ambayo itafanyika katika bustani ya Edoardo VII.

Ijumaa 4 Agosti kupitia crucis na vijana

Baadhi ya vijana kutoka WYD watapokea sakramenti ya kitubio  kutoka kwa Papa katika uwanja wa so Impèrio huko Belèm asubuhi ya Ijumaa tarehe 4 Agosti. Papa  Francisko mwenyewe, karibu 3.45 asubuhi, atakwenda kwenye kituo cha parokia ya "de Serafina" kukutana na wawakilishi wa baadhi ya vituo vya usaidizi na misaada. Saa 6,  chakula cha mchana na vijana katika Ubalozi wa Vatican  wakati saa 12 jioni  Papa ataongoza  Njia ya Msalaba pamoja na vijana katika bustani ya Edoardo VII.

Jumamosi tarehe 5 Agosti ziara ya Fatima na mkesha wa WYD

Madhabahu ya Mama Yetu wa Fatima yatatembelewa na Papa asubuhi ya Jumamosi tarehe 5 Agosti 2023. Papa Francisko ataondoka Lisbon kwa helikopta kuelekea uwanja wa Fatima saa 2 na saa 3.30 atasali sala ya Rozari Takatifu pamoja na vijana wagonjwa katika Kikanisa cha Tokeo la Mama Yetu . Karibu saa sita mchana kurudi kwa mji mkuu kunatarajiwa. Miapngo  miwili imepangwa: Saa 12:00 jioni mkutano wa faragha wa kawaida na washiriki wa Jumuiya ya Yesu katika Chuo cha Mtakatifu   João de Brito na saa 2.45 usiku  kama ilivyotajwa, mkesha na vijana katika Uwanja wa Tejo.

Misa Takatifu Dominika   6 Agosti na kurudi mjini Vatican

Misa ya kufunga Siku ya Vijana Duniani itaadhimishwa na Papa tena katika bustani ya Teho siku ya Dominika  tarehe 6 Agosti alasiri kutakuwa na mkutano na watu wa kujitolea wa WYD kwenye passeo marìtimo huko Algès, kabla ya afla ya kumuaga katika uwanja wa Anga wa  Figo Maduro. Ndege ya kurudi itaondoka saa 12.15 jioni na kufika kwenye uwanja wa ndege wa Fiumicino Roma saa 4.15 usiku.

07 June 2023, 17:01