Papa Francisko:ukaribu wa waathirika wa ajali ya treni India
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 4 Juni 2023, ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Utatu Mtakatifu, Baba Mtakatifu amesali na kuonesha ukaribu kwa idadi kubwa ya waathirika wa ajali ya Treni iliyotokea hivi karibu nchini India. Amesema yuko “karibu na waliojaruhiwa na familia: Baba wa mbingu awapokee katika ufalme wake roho za marehemu”.
Amewasalimu warumi na mahujaji kutoka Italia na nchi nyingi, kwa namna ya pekee wanatoka huko Villa Alemana (Chile), vijana wa kipaimara kutoka Cork (Ireland). Salamu kwa makundi ya Poggiomarino, Roccapriora, Macerata, Recanati, Aragona na Mestrino – ambao kwa hakika walionekana katika uwanja, kama hata vijana wa kipaimana na Komunio ya Kwanza kutoka katika Parokia ya Mtakatifu Giustina ya Colle, Italia.
Hatimaye salamu za mwisho za Papa Franciko zimewaendea wawakilishi wa Kikosi cha Askari Polisi Italia ambao wanasheherekea siku yao tarehe 5 Juni, kwamba anawashukuru kwa ukaribu wao wa kila siku kwa watu. Na Virgo Fidelis,(Bikira amini) ambaye ni msimamizi wao, awalinde na familia zao. Kwake yeye Mama mpole ninakukabidhi kwa watu waliojaribiwa na janga la vita hasa nchi pendwa iliyopigika Ukraine. Na vile vile vijana wa Mama safi ambao hawaokosi uwanjani. Amewatakia Dominika njema na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.