Papa Francisko:tusiibie vizazi bali kuwapa tumaini la maisha bora ya baadaye!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Changamoto kubwa na inayodai jitihada kubwa kwa sababu inahitaji kubadili dira, maamuzi stahiki ya mabadiliko katika mtindo wa sasa wa matumizi na uzalishaji ambao mara nyingi hushiriki katika utamaduni wa kutojali na uharibifu wa mazingira na watu. Hata hivyo changamoto hiyo ni fursa ya kusisimua na inayoweza kufikiwa, kwa sababu inakuwezesha kuhama kutoka katika utamaduni huo hadi katika maisha kulingana na heshima na huduma kwa kazi ya uumbaji na jirani. Haya ndiyo ambayo Baba Mtakatifu Francisko amezindua, Jumatatu tarehe 5 Juni 2023 alipokutana na Wahamasishaji wa Tamasha la Kijani na Bluu, lililoandaliwa mjini Roma, tarehe 5 Juni na kuanzia tarehe 6 hadi 8 Juni litafanyika huko Milano Italia ambalo ni mpango wa uchapishaji wa kikundi cha Kiitaliano kiitwacho Gedi kinachojitolea kwa ajili ya uendelevu na mazingira.
Kwa njia hiyo ilikuwa ni fursa ya kupendekeza utamaduni wa malezi na jinsi watoto wanavyotunzwa, ambayo inaweka hadhi ya binadamu na manufaa ya wote katika kitovu hicho cha Siku ya Mazingira Duniani kote ambayo uhadhimishwa kika tarehe 5 Juni katika kumbukumbu siku hiyo iliponzishwa mnamo mwaka 1972 ya Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira ya Binadamu huko Stockholm, Sweden. Katika miaka hii hamsini, Papa Francisko amebainisha, juu ya ufahamu wa masuala haya kuwa “umeongezeka na ujuzi wetu wa athari za matendo yetu kwa nyumba yetu ya pamoja na kwa wale wanaoishi ndani yake na watakaokaa ndani umepanuka, pia kuongezea hisia zetu za uwajibikaji kwa Mungu, ambaye ametukabidhi utunzanji wa kazi ya uumbaji, mbele ya jirani zetu na mbele ya vizazi vijavyo.”
Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu hasa amekumbuka kwamba alitaka kuchapisha waraka wa Laudato si' kabla ya COP 25 huko Paris kuhusu hali ya tabianchi na anasikitika kwamba tukio hilo chanya halikufuatwa na wengine wa kiwango sawa. Imethibitishwa, kwani Papa amesisitiza, huku akinukuu ripoti ya Jopo la Serikali Mbalimbali la Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) kuhusu tabianchi , kwamba chaguo na hatua zinazotekelezwa katika muongo huu zitakuwa na athari kwa maelfu ya miaka, hasa kuhusu athari kwenye sayari. Hali ya mabadiliko ya tabianchi inatukumbusha kwa uthabiti wajibu wetu na inawagusa watu maskini zaidi na walio dhaifu zaidi, wale ambao wamechangia kidogo sana katika mabadiliko yake. Na hivyo awali ya yote ni suala la haki na baadaye mshikamano amesisitiza.
Hii inamaanisha kuegemeza hatua yetu kwenye ushirikiano unaowajibika kwa upande wa wote. Kama janga la Uviko-19 limeonesha, ulimwengu wetu sasa unategemeana sana na hauwezi kumudu kugawanywa katika vikundi vya nchi zinazoendeleza masilahi yao kwa njia ya pekee au isiyo endelevu. Tabia ya kutowajibika kiukweli ni adui halisi na ina athari kwa ubinadamu wetu leo na kesho. Kuhusiana na hilo, Papa Francisko alikumbuka mkutano wake na wavuvi wa Mtakatifu Benedetto wa Tronto, Italia ambao badala ya kurudisha samaki wa siku hiyo kwenye boti zao, walirudi na tani za plastiki, wakipoteza mapato yao ya uvuvi, lakini waliboresha mazingira.
Mabadiliko, amesisitiza, ni ya dharura na hayawezi kuahirishwa tena. Kwa maana hiyo, alikumbuka jinsi hivi karibuni alikutana na watendaji wa migahawa ya chakula cha haraka ya McDonald, ambayo imebadilisha kutoka plastiki kwa ajili ya ufungaji hadi karatasi iliyosindikwa, na jinsi Vatican pia imepiga marufuku plastiki, iliyopunguzwa kwa asilimia 93%. Hatua madhubuti za kuhakikisha kwamba wale waliozaliwa katika miaka 30 hawaishi katika ulimwengu usio na makazi. Papa amesisitiza kwamba “Tusiibe vizazi vipya"” bali kuwapa tumaini la maisha bora ya baadaye.