Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani wa Italia Bwana Silvio Berlusconi kilichotokea tarehe 12 Juni 2023 huko Milano. Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani wa Italia Bwana Silvio Berlusconi kilichotokea tarehe 12 Juni 2023 huko Milano.  (AFP or licensors)

Papa Francisko Asikitishwa na Kifo cha Silvio Berlusconi 1936-12 Juni 2023

Kwa hakika kifo cha Berlusconi ni pigo kubwa kwa nchi ya Italia kwani alikuwa ni mdau muhimu sana katika siasa za Italia kiasi hata cha kuchaguliwa kuwa Waziri mkuu. Baba Mtakatifu anamwombea Hayati Silvio Berlusconi amani na maisha ya uzima wa milele; faraja na matumaini kwa wale wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito. Hayati Silvio Berlusconi alizaliwa tarehe 29 Septemba 1936 na kufariki dunia tarehe 12 Juni 2023 akiwa na umri wa miaka 86.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani wa Italia Bwana Silvio Berlusconi, kilichotokea, Jumanne tarehe 12 Juni 2023 huko Milano akiwa na umri wa miaka 86. Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Maria Elvira Berlusconi, msichana wa kwanza wa Berlusconi, anapenda kuonesha uwepo wa karibu katika msiba huu mzito kwa njia ya sala na sadaka yake. Kwa hakika kifo cha Berlusconi ni pigo kubwa kwa nchi ya Italia kwani alikuwa ni mdau muhimu sana katika siasa za Italia kiasi hata cha kuchaguliwa kuwa Waziri mkuu. Baba Mtakatifu anamwombea Hayati Silvio Berlusconi amani na maisha ya uzima wa milele; faraja na matumaini kwa wale wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito. Kardinali Pietro Parolin, anaunganisha pia salam zake za rambirambi kwa ajili ya kumwombea Hayati Silvio Berlusconi.

Hayati Silvio Berlusconi 1936-2023
Hayati Silvio Berlusconi 1936-2023

Naye Kardinali Matteo Maria Zuppi, kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI, amemtumia salam za rambirambi Maria Elvira Berlusconi kufuatia kifo cha Baba yake mpendwa Silvio Berlusconi, aliyejipambanua kuwa ni mfanyabishara maarufu nchini Italia, akawekeza katika maisha ya kijamii, kitamaduni na kifedha. Katika kipindi cha miaka thelathini akajitokeza kuwa ni kati ya wadau wakuu wa masuala ya kisiasa nchini Italia, akachaguliwa mara nyingi na wananchi kuwa mwakilishi wao kwenye Bunge la Italia. Mara nne akachaguliwa kuiongoza Italia kama Waziri mkuu bila kusahau kwamba, aliwahi kuchaguliwa pia kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya. Kardinali Matteo Maria Zuppi, anapenda kutuma salam za rambirambi sanjari na kuwahakikishia sala na sadaka yake. Hayati Silvio Berlusconi alizaliwa tarehe 29 Septemba 1936 huko Milano na amefariki dunia tarehe 12 Juni 2023 kwenye Hospitali ya “San Raffaele-Milano” alikokuwa amelazwa kwa muda. Ni Muasisi wa Chama cha Kisiasa cha “Forza Italia.” Askofu mkuu Mario Delpin wa Jimbo kuu la Milano ndiye anayeongoza Ibada ya Misa ya Mazishi ya Hayati Silvio Berlusconi, Jumatano tarehe 14 Juni 2023 kwenye Kanisa kuu la Jimbo kuu la Milano.

Rambirambi
13 June 2023, 14:17