Tafuta

Papa Benedikto XVI na Papa Francisko Papa Benedikto XVI na Papa Francisko 

Kard.Herranz:Francisko na Benedikto wamenijenga kwa fadhila zao

Kadinali wa Hispania amechapisha kitabu cha kumbukumbu zake na Mapapa Wawili kwa ajili ya heshima ya urafiki wao wa kibinafsi.Dibaji ni ya Papa Francisko ambaye anamshukuru Kardinali kwa kazi yake na ambaye anamsifu kama mtu wa Kanisa na moyo wa Kanisa.

Na Angella rwezaula, -Vatican.

Mapapa Wawili ni kichwa cha kitabu cha kumbukumbu cha Kardinali Julián Herranz Casado kuhusu uzoefu wake katika huduma ya Papa Benedikto XVI na Papa Francisko kwa ushuhuda wa maendeleo ya Kanisa katika miongo ya hivi karibuni. Katika dibaji iliyotiwa saini na Papa Francisko, anatoa shukrani kwa kazi na juhudi ya kazi kwamba: “Ninavutiwa na kumbukumbu yako na umri wako mdogo. Kuna kumbukumbu ya nyakati zilizoshirikishwa na kardinali ambaye  Papa anamfafanua kama mtu wa Kanisa, na  mtu mwenye moyo wa kikanisa. Papa Francisko katika dibaji hiyo anakumbuka historia kuwa baada ya Mkutano wa uchaguzi ambao ulimchagua Papa Benedikto XVI, Kardinali Herranz aliwaalika Kardinali Hummes na Bergoglio na  hivyo hata  Mikutano ishirini na moja na mchujo kwa upapa wa Benedikto XVI hadi ule wa Papa Fransisko na pia kumbukumbu ya mapapa wengine walioelezea maisha ya mwandishi hyo.

Miongoni mwa mada zilizoshughulikiwa, zipo hata zile zenye utata, kwa mfano wa kuvuja kwa habari, nyanyaso za kijinsia, mageuzi, kujiuzulu kwa upapa, hata uadui dhidi ya Papa. “Kwa moja ya mabembelezo ya Mungu mpaji ambapo ninashukuru kwa moyo wote kila siku, nilipata bahati nzuri isiyoweza kufikiria ya kuwatumikia mapapa sita mjini Vatican, kuanzia mwaka huo wa mbali 1960 hadi leo hii. Si chini ya miongo sita ... na hasa haijachapishwa na mbili za mwisho”, anaandika Kardinali katika kitabu chake. Kardinali Herranz anaeleza hasa kwamba, “Benedikto XVI na Fransisko kila mmoja anatafakari, kwa namna yake na kwa kutumia Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican,  uso wa kirafiki na mafundisho ya furaha ya Yesu wa Nazareti, bila kujali tofauti zinazodhaniwa kuwa za kimafundisho, ambazo wengine wanazitia chumvi kwa kuanza na itikadi zinazopingana na itikadi kali, au kwa sababu tu ya maslahi ya muda ya asili ya kijamii na kisiasa,” anasema. “Binafsi nilikutana na askofu mkuu wa Munich, Joseph Ratzinger, mnamo Juni 1977, mara tu alipoteuliwa kuwa Kardinali.”  Kwa upande wake, urafiki wangu na Kardinali Bergoglio, askofu mkuu wa Buenos Aires, ulianza wakati wa Mkutano Mkuu 2005, ambao ulimchagua Kadinali Ratzinger kuwa Papa Benedikto  XVI, anakumbuka mwandishi huyo na kwamba “ waliniheshimu kwa urafiki wao na imani yao ya kibinafsi, zaidi ya ninavyostahili na kwa ishara za kugusa.”

Kardinali Julián Herranz, akimwelezea Papa Benedikto wa kumi na sita anasema ni kama Baba wa Kanisa wa karne ya 21 na  anataja ukweli kwamba sifa zake za kibinafsi “zinamuunganisha tena, katika mwelekeo wa kiakili na kichungaji, na Mababa wa Kanisa, walioishi kwa njia ya kikanisa, matukio na nyanja za kijamii za karne za kwanza za Ukristo zenye uwazi maalum wa kimafundisho na hisia kubwa ya uwajibikaji wa kichungaji.” Mwandishi pia anatambua kwa Papa  Benedikto XVI  kama mchungaji wa ulimwengu wote ambaye alishughulikia kwa dhati uhalifu mbaya sana wa unyanyasaji wa watoto. “Ratzinger aliinua kwa mara ya kwanza katika Vatican  nafasi ya kufikiria upya kanuni za kisheria na za kichungaji dhidi ya uhalifu huu mbaya sana , ili kuwezesha matumizi yake na kuepuka tabia mbaya iliyofuatwa hadi wakati huo”.  Pia alikuwa Papa wa kwanza,  Kardinali Herranz anashuhudia, kwamba  ambaye alitaka kukutana na kusikiliza waathirika  wa uhalifu huo katika safari zake za kichungaji”. Na anaongeza: “Kwa bidii na ushupavu ulioje, kwanza Kardinali Ratzinger na kisha Benedikto wa kumi na sita, wamedumisha wajibu wao wa kichungaji kuangazia na kuponya jeraha hili kubwa katika roho ya wahanga na katika Watu wote wa Mungu”.

Katika kitabu chake chenye kichwa: “Mapapa Wawili,” Kardinali Herranz Casado pia anasisitiza ukaribu na mwendelezo wa majisterio ya Papa Benedikto  XVI kwa Papa Francisko kwamba: ni  “Hasa katika Waraka wa Laudato si' na Fratelli tutti, Yeye anaendana na usikivu na kujali kwa Papa Benedikto XVI. Mungu Muumba na Baba ndiye wakati huo huo yule anayeipatia  hadhi ya kitaalimungu kwa maumbile yaliyoumbwa na anayetufanya kuwa kaka na dada. Hivyo  ni uchungu mkubwa wa Papa katika uso wa 'vita vya kufuru' huko Ukraine  na wengine wengi wanaofanya itikadi ya Ukaini kuwepo duniani ushetani", anaandika Kadinali huyo, akigusia wasiwasi mkubwa wa Papa Francisko  na kujitolea kwake katika utafutaji wa amani.

Kuanzia kwenye  mikutano ya kibinafsi na Francisko, na vile vile kutoka kwa kubadilishana barua za kibinafsi, Kardinali wa Hispania anamkumbuka kwa hisia Papa kwa upendo ambaye katika siku za kwanza za upapa wake alitaka kwenda Lampedusa kusindikizana  na wale walioteseka kutokana na ajali ya meli ya wahamiaji. “Binafsi, nilisifu kwa shauku wazo kwamba safari yake ya kwanza ya kichungaji pendwa hakuwa kama mkuu wa nchi,  bali alikwenda kama 'wakili wa Kristo', ambaye alitanguliza huduma yake kwa maskini, ambao waliondoka kutokana na kuteseka pamoja nao uchungu na maumivu ya Kristo kwa  wengi sana waliopigwa na ukosefu wa amani na kazi. Na pia kumbuka sala ya dhati katika uwanja wa Mtakatifu Petro , ambayo Papa aliongoza kwa watu walioathiriwa na janga la Uviko  katika miji yote ulimwenguni.

Kitabu cha Kardinali Herranz kuhusu "Mapapa wawili"
04 June 2023, 11:49