Tafuta

Papa akifikiri juu ya utata wa hali ya mtiririko mkubwa wa wahamiaji na wakimbizi leo hii, anatoa wito wa juhudi za pamoja ya jumuiya ya kimataifa. Papa akifikiri juu ya utata wa hali ya mtiririko mkubwa wa wahamiaji na wakimbizi leo hii, anatoa wito wa juhudi za pamoja ya jumuiya ya kimataifa.  (Vatican Media)

Ujumbe wa Siku ya 109 ya Wahamiaji duniani:Huru wa kuchagua kuhama au kubaki

Kusindikiza na kutawala vizuri zaidi mtiririko wa wahamiaji na wakimbizi kwa kujenga madaraja na sio kuta,kupanua njia za uhamiaji salama na wa kawaida,ndiyo maombi ya Papa katika ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi,itakayofanyika tarehe 24 Septemba ijayo na kwamba popote pale pawe na jumuiya iliyo tayari kukaribisha,bila kumwacha mtu yeyote nyuma.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 11 Mei 2023 katika ujumbe uliochapishwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya 109 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani, unaoongozwa na kauli mbiu: “Uhuru wa kuchagua kuhama au kubaki”, itakayo adhimishwa tarehe 24 Septemba 2023, ni mwaliko wa kumtaka kila mtu ajitolee kadiri awezavyo kwa uwajibu wake katika kufanya uhamiaji. Kwa kauli mbiu hiyo ni kwamba uhamiaji uwe chaguo la bure na la kweli, huku  akifikiri juu ya utata wa hali ya mtiririko mkubwa wa wahamiaji na wakimbizi leo hii, anatoa wito wa juhudi za pamoja ya jumuiya ya kimataifa ili kuhakikisha kila mtu anashiriki sawa katika manufaa ya wote, heshima kwa haki za msingi na upatikanaji wa maendeleo  fungamani ya binadamu. Ni kwa kutembea pamoja tu ndipo tutaweza kufika mbali na kufikia lengo la pamoja la safari yetu.

Mtiririko wa uhamiaji ni jambo gumu

Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwmba: “Mitiririko ya uhamiaji leo hii ni usemi wa jambo gumu na lililoelezwa, ufahamu ambao unahitaji uchambuzi wa uangalifu wa vipengele vyote vinavyoonesha hatua mbalimbali za uzoefu wa uhamiaji, kuanzia kuondoka hadi kuwasili, ikiwa ni pamoja na kurudi iwezekanavyo”. Kwa njia ya kuchangia juhudi hii ya kutafsiri ukweli, nimeamua kujikita katika Ujumbe wa Siku ya 109 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani kwa ajili ya uhuru ambao unapaswa kutofautisha kila wakati uchaguzi wa mtu mwenyewe kuondoka kwenye ardhi yake.”

Familia Takatifu ilihamia Misiri

Kwa hiyo Baba Mtakatifu katika ujumbe huo uliochapisha tarehe 11 Mei, anafafanua kuwa “uhuru wa kuondoka, na uhuru wa kukaa”, kilikuwa ni kichwa cha mpango wa mshikamano uliohamasishwa miaka michache iliyopita na Baraza la Maaskofu wa Italia kama jibu madhubuti kwa ajili ya changamoto za uhamiaji wa kisasa. Na kutokana na usikilizaji wangu wa mara kwa mara kwa Makanisa mahalia nimeweza kuthibitisha kwamba dhamana ya uhuru huu inajumuisha wasiwasi ulioenea na wa pamoja wa kichungaji”. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amebainisha kuwa ““Malaika wa Bwana akamtokea Yusufu katika ndoto, akamwambia, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuonye; kwa maana Herode anamtafuta mtoto na kumwua”(Mt 2,13). Kukimbia kwa Familia Takatifu hadi Misri sio matokeo ya uchaguzi huru, kama kweli hawakuwa wengi wa wahamiaji ambao wameweka alama ya historia ya watu wa Israeli. Uhamiaji lazima iwe chaguo la bure, lakini kiukweli katika hali nyingi, hata leo, sivyo. Migogoro, majanga ya asili, au zaidi kutowezekana kwa kuishi maisha yenye heshima na mafanikio katika nchi yao huwalazimisha mamilioni ya watu kuondoka. Tayari mwaka wa 2003, Mtakatifu Yohane Paulo II alithibitisha kwamba “kujenga mazingira madhubuti ya amani, kwa kadiri wahamiaji na wakimbizi wanavyohusika, kunamaanisha kujitolea kwa dhati kulinda zaidi ya yote haki ya kutohama, yaani, kuishi kwa amani na heshima katika nchi ya mtu mwenyewe.”

Uporaji wa rasilimali na taabu ni vyanzo vya uhamiaji

Mateso, vita, matokea ta mabadiliko ya tabianchi na taabu ni kati ya sababu zinazoonekana za uhamiaji wa kisasa. Ili kuyaondoa yote ni lazima tujiulize tufanye nini na tuache kufanya nini, tukifanya kila tuwezalo kuzuia mbio za silaha, ukoloni wa kiuchumi, uporaji wa rasilimali za watu wengine, uharibifu wa nyumba yetu ya pamoja”. Papa anatoa wito kwa uwajibikaji katika nafasi ya kwanza ya nchi asilia na watawala wao walioitwa kutekeleza siasa nzuri, uwazi, uaminifu, kuona mbali na huduma ya kila mtu, hasa wale walio katika mazingira magumu zaidi. Sambamba na hilo, Baba Mtakatifu Francisko anaomba nchi za asili zenyewe ziwekwe katika nafasi ya kufanya hivyo, bila kujikuta zikiibiwa maliasili na watu na bila kuingiliwa na nje kwa lengo la kupendelea maslahi ya wachache.

Ujumbe wa Papa wa Siku ya 109 ya Uhamiaji na wakimbizi duniani

Ili kuhakikisha kwamba mtua anafanya chagua chaguo huru la kuacha nchi yake  “elimu na kuzingatiwa, ni muhimu kuzuia wanaume, wanawake na watoto wengi katika mikono ya  waalifu  wa udanganyifu hatari au wasafirishaji wasio waaminifu. Katika kila mhamiaji hakuna kaka au dada tu katika shida. Kuna Kristo mwenyewe anayebisha mlango wetu”, anaandika Papa Francisko akinukuu baadhi ya mistari kutoka sura ya 25 ya Injili ya Mathayo: “Nalikuwa na njaa mkanipa chakula; nalikuwa na kiu mkaninywesha; alinikaribisha…”. Kutokana na ufahamu huu ndipo kuna wito wa kuwa na heshima kubwa kwa hadhi na utu wa  kila mhamiaji, kumsindikiza na kudhibiti mtiririko kwa njia bora, ili kujenga madaraja na sio kuta, kupanua njia za uhamiaji salama na wa kawaida. 

Uwepo wa Jumuiya inayokaribisha kila mahali

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anabainisha kwamba popote tunapoamua kujenga maisha yetu ya baadaye, katika nchi tuliyozaliwa au kwingineko, jambo la muhimu ni kwamba siku zote kuna jumuiya iliyo tayari kukaribisha, kulinda, kukuza na kuunganisha kila mtu, bila ubaguzi na bila kumwacha mtu yeyote. Mchakato wa Safari ya sinodi ambayo tumeifanya kama Kanisa inatuongoza kuona katika watu walio hatarini zaidi  na miongoni mwao wahamiaji na wakimbizi wengi  kuwa wenzi maalum wa kusafiri, kupendwa na kutunzwa kama kaka na dada. Ni kwa kutembea pamoja tu ndipo tutaweza kufika mbali na kufikia lengo la pamoja la safari yetu, Papa anahitimisha ujumbe wake kwa sala:

Sala:

Ee Mungu, Baba mwenyezi, utupe neema ya kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya haki, mshikamano na amani, ili watoto wako wote wahakikishiwe uhuru wa kuchagua kuhama au kukaa. Utupe ujasiri wa kukemea mambo yote ya kutisha ya ulimwengu wetu, kupambana na kila dhuluma ambayo inaharibu uzuri wa viumbe wako na maelewano ya nyumba yetu ya kawaida. Utusaidie kwa nguvu ya Roho wako, ili tuweze kuonesha huruma yako kwa kila mhamiaji unayemweka kwenye njia yetu na kuieneza mioyoni na katika kila mazingira, utamaduni wa kukutana na kujali mioyoni na katika kila mazingira.”

11 May 2023, 16:54