Tafuta

2023.05.13 Papa Francisko amekutana na wajumbe wanachama cha kilimo cha vijana wakulimba kutoka Hispania. 2023.05.13 Papa Francisko amekutana na wajumbe wanachama cha kilimo cha vijana wakulimba kutoka Hispania.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Wakulima ni wanaikolojia halisi kufanya kazi na wanyama na mimea

Papa akikutana mjini Vatican na Wanachama wa Kilimo cha vijana wakulima kutoka Hispania amewatia moyo wasikate tamaa,kwa sababu kila wito hupelekea msalaba.Mtu anakubali juhudi ya kufanya kazi ngumu na kufanya kazi na wanyama na hivyo hakuna siku ya siku kuu na wala mgomo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na  Wajumbe wa Chama cha Kilimo cha Vijana wakulima kutoka Hispania tarehe 13 Mei 2023 akianza houba yake amewashukuru kwa kwa shauku ambayo wameonesha katika ziara yao na shauku unayoonesha kwa kazi yao mashambani, kwa ajili ya mifugo yao na kwa huduma wanayotaka kutoa kwa ajili ya jamii. Kama ilivyo katika maeneo mengine mengi ya maisha, elimu ya ikolojia haijumuishi hasa ripoti za kejeli za wataalamu, wala habari na mipango maarufu inayowafikia watu wa kawaida kupitia njia za mawasiliano ya kijamii. Wanaweza kuwa wa lazima na wenye manufaa, ikiwa wanafanywa kwa uangalifu, lakini sio mahali pa kwanza. Wao aidha wanajua kwamba Argentina ni nchi inayojitolea hasa kwa ajili ya ufugaji na, ingawa yeye alitoka mjini, alipata fursa ya kujua ukweli wa mashambani.

Papa Francisko amebainisha kwamba hiyo ilimwezesha kutambua kwamba wao ni wanaikolojia wa kwanza, watu wanaofanya kazi na wanyama, na mimea, wao wanaoishi pamoja kila siku na kujua nini matatizo yao na mafanikio yao. Amewaomba wasirudie kauli mbiu kutoka katika kumbukumbu, bali waishi akitazama juu angani na tena wanapoamka hadi wanapolala, wakitambua kwa milio ya ndege, kelele au mlio wa furaha au woga, shauku au utimilifu wa maumbile ambayo yanawazunguka. Hiyo ni heshima na, kwa wazi, jukumu kubwa. Baba Mtakatifu hata hivyo amesema kwamba wakitafakari kwa makini, wito ambao Mungu amewaita unawafanya kuwa mashahidi wa ikolojia fungamani ambayo ulimwengu unahitaji. Wito wa kwanza kwa sababu umejikita katika maneno ya Mungu katika Mwanzo alipowaalika wanadamu kushirikiana katika kazi ya uumbaji kupitia kazi yake (taz. Mwa 1:28-31).

Papa na wajumbe wa wakilishi wa wakulima vijana wa Hispania
Papa na wajumbe wa wakilishi wa wakulima vijana wa Hispania

Ni wito wa taaluma nyingi, kwa sababu  unachanganya uhusiano wa moja kwa moja na ardhi, utunzaji wake na kilimo, na huduma wanayotoa kwa jamii. Kwa hivyo Mungu anawaomba nini kwao katika kazi hiyo? Anawaomba wafikirie mashambani kama zawadi, kama kitu ambacho wamepewa na ambacho watawarithisha watoto wao; wafikirie uzalishaji kama zawadi ambayo Bwana, kupitia wao, anatuma kwa watu wake ili kukidhi njaa yao na kuzima kiu yao. Njaa isiyo ya mkate tu, bali na ya Mungu pia, ambaye, ili kushiba, hakusita kujitengenezea chakula cha mwili na hivyo kuufikia moyo wa mwanadamu (Mt 4, 3-4; Gv 6, 55-57).

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba kutokana na thamani hizi msingi ambazo amewashukuru, inazaliwa uwajibikaji waliokabidhwa wao binafasi, lakini hawa wale ambao kwa namna moja wanashiriki katika uzalishaji, katika kazi na katika kugawnya vyakula. Ni lazima kufanya kazi ili wema huo ambao Mungu anatupatia husibalishwe kuwa silaha, kwa mfamono kizuishi cha kufika kwa vyakula kwa watu katika migogoro; au havigeuki kuwa utaratibu wa kubahatisha, kuchezea bei na uuzaji wa bidhaa kwa madhumuni pekee ya kupata faida kubwa zaidi. Hili ndilo tunalopaswa kukemea, ambalo lazima liumize mioyo yetu; Wanyama wanaowachunga kwa kujitolea namna hiyo hawastahili, watu unaowafanyia kazi kwa ari hawastahili, Mungu hastahili. Inawaudhi na inakukera.

Mkutano wa wajumbe wanachama wakulima vijana wa Hispania
Mkutano wa wajumbe wanachama wakulima vijana wa Hispania

Papa amewaomba wasikate tamaa, kwa sababu amesema kila wito hupelekea msalaba na mtu anakubali juhudi ya kufanya kazi ngumu na kwa kufanya kazi na wanyama hakuna siku ya siku kuu na wala mgomo. Na bado kazi ngumu ni ile ya kukubali kutoeleweka kwa wale ambao hawatoi thamani kwa kitu moja ambacho ni muhimu kwa ajili ya maisha na mbacho ni uzalishaji wa chakula au kupendelea kutafuta makosa badala ya suluhisho. Baba Mtakatifu amewakabidhi kwa Bikira Maria kazi yao wanayotenda ili wahisi daima ukaribu wa Yesu ambaye akiwa juu msalabani alijitoa mwili wake na kujifanya chakula,  na alijifanya maisha akiwa anayatoa tele.

13 May 2023, 13:59