Papa:Tutajifunza lini kuwekeza katika ustawi wa watu kuliko silaha?
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 13 Mei 2023 amekutana na Mabalozi wa nchi ya Island, Bangladesh, Siria, Gambia ma Kasakhstan wanaowakilisha nchi zao na ambao wamewakilisha hati na utambulisho wao kwa Papa. Katika hotuba yake, Baba Myakatifu Francisko ameomba wamfikishie salamu zake kwa viongozi wa nchi zao na kuwaomba waweleze anavyo sali ajili ya utimilifu wa huduma yao. Wazo la Baba Mtakatifu kwa namna ya pekee ni kwa ajili ya nchi pendwa ya Siria, ambayo bado inateseka, kuanza kwa upya kutokana na tetemeko la nguvu lililoikumba, na kati ya mateso yao yanayo endelea yaliyosababishwa na migogoro ya silaha. Baba Mtakatifu Francisko, amesema ikiwa tunatazama kwa uangalifu hali ya sasa ulimwenguni, hata kwa mtazamo mmoja wa kijujuu, inawezekana kutuacha na shaka na kukata tamaa. Tufikirie sehemu nyingi kama Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mynamar, Lebanon na Yerusalme ambao wanakabiliana na mapigano na ghasia.
Haiti ambayo inaendelea kugubikwa na mgogoro mkubwa wa kijamii, kiuchumi na kibinadamu. Baadaye kwa ujumla kuna vita vinavyoendelea nchini Ukraine ambavyo vinamesababisha mateso na vifo visivyo semekana. Na zaidi, tunaona ongezeko la wimbi wa uhamiaji wa kulazimishwa, matokeo mabaya ya mabadiliko ya tabianchi na idadi kubwa ya kaka na dada ulimwenguni ambao wanaishi bado kwenye umaskini kwa sababu ya kukosa hasa maji salama ya kunywa, chakula, matibabu msingi, elimu na kazi yenye hadhi. Bilashaka kuna kuongezeka ukosefu wa msimamo katika mfumo wa kiuchumi ulimwenguni. Kutokana na hayo, basi, Baba Mtakatifu anajiuliza maswali: je ni lini tutajifunza kutokana na historia ambayo njia za vurugu, ukandamizaji na ya tamaa isiyozuilika ya kuteka ardhi haitumiki kwa manufaa ya wote? Je ni lini tutajifunza kuwa, kuwekeza katika usitawi wa watu daima ni bora kuliko kutumia rasilimali katika utengenezaji wa silaha za maangamizi? Je ni lini tutajifunza kuwa masuala ya kijamii, kiuchumi na usalama vyote vinahusiana moja na jingine? Je ni lini tutajifunza kuwa tupo katika familia moja ya kibinadamu ambayo inawezekana kabisa kutazamia tu ikiwa wajumbe wote wanaheshiamiana na wanatunzana. Na wana uwezo wa kutoa mchango wao kwa njia asili? Ikiwa hatutafikia utambuzi huo, tutaendelea kuishi kile ambacho Baba Mtakatifu ametaja kuwa ni vita ya tatu ya dunia ambayo imegawanyika vipande vipande.
Labda maelezo haya Papa amesema utafikiri yanatia shaka hisia zetu hasa kwa kuridhika kwa ajili ya maelendeleo maalum ya kiteknolojia na kisayansi yaliyofikiwa au kwa ajili ya hatua ambazo tayari zimefikiwa ili kukabiliana na masuala ya kijamii na maendeleo kwa haki ya juu kimataifa. Ikiwa matokeo yote haya yatafikiwa katika hali ya sasa ya ulimwengu hatupaswi kamwe kuhisi kutosheka au kutojali zaidi kuhusu hali ya sasa ya ulimwengu, wala kushindwa kuhakikisha kwamba kaka na dada zetu wote wanaweza kufaidika na mafanikio na maendeleo haya. Na wakati huo huo lazima hata kubaki na msimamo katika kuamini kuwa familia ya kibinadamu ina uwezo wa kukabiliana kwa ufanisi changamoto za wakati wetu. Katika pendekezo hilo, Baba Myakatifu amesema tutazame huduma ambayo wao kama mabalozi wameitwa kujikita nayo. Kama wajuavyo kazi ya Balozi ni ya kizamani na adimu. Hiyo iliandikwa hata katika Maandiko ya Kikristo na Mtume Paulo alipotumia neno kwa ajili ya kuelezea watangazaji wa Yesu Kristo (2 Cor 5,20). Kiukweli nafasi chanya ya Balozi imewekwa kila kipinidi na katika hali nyingi. Kutokana na hiyo Papa amependa kushirikishana kwa ufupi tafakari kuhusu suala la nini maana ya kuwa Balozi.
Baba Mtakatifu amesema kama mwanamume au mwanamke wa mazungumzo na mjenzi wa daraja, Balozi anaweza kuwa mtu wa matumaini. Matumaini katika wema wa mwisho wa ubinadamu. Ni matumaini kwamba jambo la pamoja linawezekana kwa sababu sisi sote ni sehemu ya familia ya kibinadamu. Tumani ambalo neno la mwisho halitasemwa kamwe ili kuepusha mzozo au kuutatua kwa amani. Natumaini kuwa amani sio ndoto tu. Huku akiwa anaendelea kuitumikia nchi yake ya asili kwa uaminifu, Balozi anajaribu kuweka kando hisia zisizo za lazima na kushinda misimamo isiyojengeka ili kupata suluhisho zinazo kubalika. Papa amethibitisha kwamba kazi hiyo sio rahisi. Sauti ya sababu na wito wa amani mara nyingi huangukia kwenye masikio ya viziwi. Hali ya sasa ya ulimwengu, hata hivyo, inasisitiza zaidi haja ya Mabalozi kuwa watetezi wa mazungumzo, mabingwa wa matumaini. Vatican inathamini jukumu lao muhimu, kama inavyooneshwa na ushirikiano wake wa kidiplomasia katika ngazi ya nchi mbili na kimataifa.
Kwa upande wake, Papa amesisitiza kuwa Vatican, kwa kuzingatia asili yake na utume wake maalum, linajizatiti kulinda utu na hadhi isiyo vunjwa wa kila mtu, kuendeleza manufaa ya wote na kukuza udugu wa kibinadamu kati ya watu wote. Juhudi hizi, ambazo hazihusishi kutafuta malengo ya kisiasa, kibiashara au kijeshi, hukamilishwa kupitia utekelezaji wa kutoegemea upande wowote. Mbali na kutotegemea upande wowote kimaadili, hasa katika kukabiliana na mateso ya binadamu, hii inaipatia Vatican nafasi iliyoainishwa vyema katika Jumuiya ya Kimataifa ambayo inaruhusu kuchangia vyema katika utatuzi wa migogoro na masuala mengine. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa kwa kuzingatia uchunguzi huo, ana hakika kwamba kutakuwa na fursa nyingi kwao za kushirikiana na Vatican juu ya mada za maslahi ya pamoja. Kwa maana hiyo, Papa amehakikisha kwamba, Sekretarieti ya Nchi, pamoja na Idara na Ofisi za Vatican, wako tayari zaidi kushirikiana nao katika mazungumzo ya wazi na ya uaminifu, kwa kushirikiana kwa ajili ya kuboresha familia ya binadamu. Kwa hiyo wanapoanza huduma hiyo mpya, Mabalozi hao, Papa amewaombea furaha na baraka nyingi za kimungu juu yao, familia zao washiriki wao wa kidiplomasia na wafanyakazi wao.