Tafuta

Inahitaji majibu madhubuti ya kiubunifu na ya ujasiri katika eneo la elimu ya ngono.Ni nani anayewasaidia kujiandaa kwa dhati kwa upendo mkubwa na wa ukarimu?(AL. 284). Inahitaji majibu madhubuti ya kiubunifu na ya ujasiri katika eneo la elimu ya ngono.Ni nani anayewasaidia kujiandaa kwa dhati kwa upendo mkubwa na wa ukarimu?(AL. 284).  

Papa:ni haramu kuunda viinitete vya bomba la majaribio na kuamua uzazi wa kukodi

Katika ujumbe kwa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la WOOMB kuhusu “mapinduzi ya Billings”,(Aprili 28-29)Papa alijikita juu ya thamani ya ushirika,maono jumuishi na umuhimu ya kujamiana kwa binadamu,kutunza uzazi wa upendo hata wakati hakuna rutuba na utamaduni wa maisha.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tunachapisha ujumbe Baba Mtakatifu Francisko ambao aliutuma kwa washiriki wa Kongamano la kimataifa WOOMB lililioongozwa na kauli mbiu: “Mapinduzi ya Billings” Miaka 70 Baadaye: Kutoka katika Maarifa ya Uzazi hadi Dawa ya Kubinafsishwa” lililofanyika tarehe  28 -29 Aprili 2023. Baba Mtakatifu katika ujumbe huo alitoa salamu zake za joto “kwa waandaaji na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la WOOMB. “Ninathamini sana mpango huu, ambao unatukumbusha tena uzuri na heshima ya ujinsia wa kibinadamu. Katika nusu ya pili ya karne iliyopita, utafiti wa kifamasia wa udhibiti wa uwezo wa kushika mimba ulipopanuka na utamaduni wa uzazi wa mpango ulipokuwa ukiongezeka, John na Evelyn Billings walifanya utafiti makini wa kisayansi na kubuni mbinu rahisi, inayoweza kupatikana kwa wanawake na wanandoa, kwa ajili ya ujuzi wa asili wa uzazi inayowapatia zana muhimu kwa usimamizi unaowajibika wa chaguzi za uzazi.”

Kasi ya awali ya kile cha 'mapinduzi ya Billings' haijapungua

Baba Mtakatifu Francisko anafafanua kuwa katika miaka hiyo, mbinu yao inaweza kuonekana kuwa ya kizamani na isiyotegemewa sana ikilinganishwa na upesi unaodaiwa na usalama wa afya za kifamasia. Bado kiukweli, mbinu yao imeendelea kuthibitisha kwa wakati na changamoto, kwani imesababisha kutafakari kwa kina juu ya idadi ya maeneo muhimu. Mambo hayo ni pamoja na hitaji la elimu juu ya thamani ya mwili wa binadamu, maono jumuishi na shirikishi ya ujinsia wa binadamu, uwezo wa kuthamini kuzaa matunda ya upendo hata kama hayana rutuba, kujenga utamaduni unaokaribisha maisha na njia za kukabiliana na Maisha, tatizo la kuporomoka kwa idadi ya watu. Katika suala hili, kasi ya awali ya kile kinachoitwa “mapinduzi ya Bilings” haijapungua, lakini inaendelea kuchangia katika uelewa wa jinsia ya binadamu na kuthamini kikamilifu vipimo vya uhusiano na uzazi vya wanandoa.

Uhusiano usioweza kutengenishwa

Katika ulimwengu unaotawaliwa na mtazamo wa kimahusiano na usio na maana wa kujamiiana kwa binadamu, elimu ya kina katika eneo hili inaonekana kuwa muhimu zaidi, inayohitaji mafunzo ya kianthropolojia na kimaadili ambamo masuala ya mafundisho yanachunguzwa bila kurahisisha isivyofaa au hitimisho lisilobadilika. Na zaidi  kuna haja daima kukumbuka uhusiano usioweza kutenganishwa kati ya maana ya umoja na uzazi ya tendo la ndoa (rej. PAUL VI, Humanae Vitae, 12). Kielelezo cha kwanza kinaonesha shauku ya wanandoa kuwa kitu kimoja, maisha ya kipekee; mwisho unaonesha tamaa ya pamoja ya kuzalisha maisha, ambayo hudumu hata wakati wa utasa na katika uzee. Maana hizi mbili zinapothibitishwa kwa uangalifu, ukarimu wa upendo huzaliwa na kuimarishwa katika mioyo ya wanandoa, na kuwafanya kukaribisha maisha mapya. Ukosefu huu,  na uzoefu wa kujamiiana unapokuwa duni, hupunguzwa kwa hisia ambazo baadaye zinakuwa za kujitegemea, na vipimo vyake vya ubinadamu na uwajibikaji vinapotea.

Haja ya majibu madhubuti,ya kiubunifu na ujasiri wa elimu ya ngono

Janga la unyanyasaji kati ya washirika wa ngono, ikiwa ni pamoja na mauaji ya wanawake hapa hupata moja ya sababu zake kuu. Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha kuwa hakika, tunaelekea kupoteza muunganisho kati ya kujamiiana na wito wa kimsingi wa kila mtu, zawadi ya ubinafsi, ambayo hupata utimilifu wa pekee katika upendo wa ndoa na familia. Ukweli huu, wakati upo ndani ya moyo wa kila mwanadamu, unahitaji elimu ili kufikia usemi kamili. Hili linahitajika haraka, na linawakilisha changamoto kwa Kanisa na wale wote walio na majukumu ya watu na jamii moyoni. Papa anataja kama alivyodokeza katika Amoris Laetitia, kwamba “inahitaji majibu madhubuti, ya kiubunifu na ya ujasiri katika eneo la elimu ya ngono: “Lugha ya mwili inahitaji uanafunzi wa subira katika kujifunza kutafsiri na kuelekeza matamanio kwa mtazamo wa kujitolea halisi”.

Nani anawasaidi vijana kijiandaa kwa upendo mkubwa na wa ukarimu?

Tunapofikiria kutoa kila kitu kwa wakati mmoja, inaweza kuwa kwamba hatutoi chochote. Ni jambo moja kuelewa jinsi vijana wanavyoweza kuwa dhaifu na waliochanganyikiwa, lakini jambo lingine kabisa kuwatia moyo kurefusha ukomavu wao katika njia ya kuonesha upendo. Lakini ni nani anayezungumza juu ya mambo haya leo? Nani ana uwezo wa kuchukua vijana kwa umakini? Ni nani anayewasaidia kujiandaa kwa dhati kwa upendo mkubwa na wa ukarimu?” (AL. 284). Baada ya yale yanayoitwa mapinduzi ya ngono na kuvunjika kwa miiko, tunahitaji mapinduzi mapya katika njia yetu ya kufikiri. Tunahitaji kugundua uzuri wa kujamiiana kwa binadamu kwa mara nyingine tena kugeukia kitabu kikuu cha asili, kujifunza kuheshimu thamani ya mwili na kizazi cha maisha, kwa lengo la uzoefu halisi wa upendo wa ndoa”.

Njia za Billings na kama hiyo zinaandaa kutambua uwajibikaji wa hamu ya uzazi

Mwelekeo mwingine wa kujamiiana, usio na changamoto kidogo katika wakati wetu, ni uhusiano wake na uzazi. Ujuzi wa uzazi, ingawa una umuhimu wa jumla kwa elimu, unakuwa muhimu zaidi wakati wanandoa wanachagua kuwa tayari kukubali watoto. Mbinu ya Billings, pamoja na nyingine kama hiyo, inawakilisha mojawapo ya njia zinazofaa zaidi za kutambua kwa uwajibikaji hamu ya kuwa wazazi.  “Leo, utengano wa kimawazo na kivitendo wa uhusiano wa kimapenzi kutoka katika uwezo wake wa kuzaliana umesababisha utaftaji wa aina mbadala za kupata mtoto, na sio tena kupitia uhusiano wa ndoa bali kwa kutumia michakato ya bandia”. Hata hivyo, “ingawa inafaa kusaidia na kuunga mkono nia halali ya kupata mimba kwa ujuzi na teknolojia ya hali ya juu zaidi ya kisayansi ambayo inaweza kuongeza uzazi, ni makosa kuunda viinitete kupete  kwenye bomba na kisha kuvipandikiza, kufanya biashara ya gametes na kuamua kutumia mazoezi ya uzazi kwa uzazi.

Mgogoro wa idadi ya watu na ukosefu wa usawa

Msingi wa mgogoro wa sasa wa idadi ya watu ni pamoja na mambo mbalimbali ya kijamii na kiutamaduni, kukosekana kwa usawa katika mtazamo wa kujamiiana”. Kwa hivyo, Papa amesisitiza kuwa mbinu ya Billings pia hutumika kama nyenzo ya kushughulikia matatizo ya utasa kwa kawaida na kuwasaidia wenzi wa ndoa kuwa wazazi kwa kutambua vipindi vingi vya rutuba. Katika uwanja huu, uelewa mkubwa wa michakato ya uzazi, kwa kutumia matokeo ya kisasa ya kisayansi, inaweza kusaidia wanandoa wengi kufanya maamuzi sahihi na ya kimaadili ambayo yanaheshimu zaidi mtu na utu wake. Hili ni jukumu kwa vyuo vikuu vya Katoliki, na Vitivo vya Tiba hasa, kuchukua jitihada mpya. Ilikuwa muhimu kwamba John na Evelyn Billings waliweza kufanya kazi katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Melbourne. Vile vile ni muhimu kwamba Kituo cha Utafiti na Udhibiti wa Asili wa Uzazi, kilichopo tangu 1976 katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu, kiwe sehemu ya moja ya taasisi za kitaaluma za Italia na hivyo kufaidika na ujuzi wa juu zaidi wa kisayansi kama inatekeleza dhamira yake ya utafiti na mafunzo. Mbinu ya kisayansi ya Kongamano hilo la Kimataifa inaambatana na utambuzi wa umuhimu wa kuzingatia upekee wa kila wanandoa na kila mtu, na hasa wanawake.

Kuna haja ya kufanya kazi kwa uvumilivu na kujitolea katika muktadha huo

“Dawa ya kibinafsi” inatukumbusha kwa usahihi kwamba kila mtu ni wa kipekee na hawezi kurudiwa na kwamba, kabla ya kuwa kitu cha matibabu na magonjwa, lazima asaidiwe kueleza uwezo wake kwa njia bora zaidi, na mtazamo wa ustawi ambao ni juu ya matunda yote ya maisha yenye usawa. Hatimaye, kukuza ujuzi wa uzazi na njia za asili pia kuna thamani kubwa ya kichungaji, kwa vile huwasaidia wanandoa kutambua zaidi wito wao wa ndoa na kushuhudia tunu za Injili za kujamiiana kwa binadamu. Umuhimu wa hili unaonekana katika idadi kubwa ya washiriki katika Kongamano hilo, huku watu kutoka nchi nyingi na kila bara wakikusanyika Roma au kujiunga kwa njia ya mtandao. Maoni chanya ambayo yamejitokeza kutokana na uzoefu wao mbalimbali, mara nyingi matunda ya kazi yao katika mazingira magumu sana ya kijamii na kiutamaduni, yanathibitisha umuhimu wa jitihada zao za kufanya kazi kwa uvumilivu na kujitolea katika uwanja huo, na sio muhimu tu kukuza utu wa wanawake na utamaduni unaotambulika kwa kukubalika kwa maisha. Haya, kiukweli ni maadili ambayo tunashiriki na dini zingine.

Basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu(1Kor 6:20)

Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amebainisha kazi yao kuwa “ilichangia katika kipengele cha msingi cha huduma ya Kanisa kwa familia, kama Watangulizi wake ambao wamefundisha pia  nay eye amejikita kutoa Wosia wa Amoris Laetitia: “Kwa maana hiyo, mafundisho ya Waraka wa Humanae Vitae rej. 10-14) na Familiaris Consortio (rej. 14; 28-35) vinapaswa kuchukuliwa kwa upya” (Kifungu cha. 222). Matumizi ya mbinu zinazotegemea midundo ya asili ya uzazi yapaswa kuhimizwa, ikisisitiza ukweli kwamba “wanaheshimu miili ya wenzi wa ndoa, wanahimiza upole kati yao, na kupendelea elimu ya uhuru wa kweli”(Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2370).  Baba Mtakatifu Francisko aliwatakia kila la kheri kwa matunda ya kazi yao na aliwashukuru kwa yote wanayofanya. Waendelee kwa ari na ukarimu katika huduma yao ya thamani kwa jumuiya ya kikanisa na wale wote wanaotafuta kukuza maadili ya kibinadamu ya kujamiiana. Na wakumbuke kila wakati kwamba baraka za awali za Mungu zinaakisiwa kwa fahari maalum katika eneo hilo la maisha (rej. Mwa 1:26-30), na kwamba tunaitwa kuheshimu katika eneo hilo pia, kama vile Mtakatifu Paulo anavyotuhimiza: “Basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”(1Kor 6:20). Alihitimisha ujumbe huo kwa kuwatakia baraka kutoka moyoni mwake na kuwaomba tafadhali wasali kwa ajili yake.

Ujumbe wa Papa kwa Kongamano la WOOMB
02 May 2023, 14:51