Tafuta

2023.05.13 Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wanawake Wakatoliki  Duniani WUCWO. 2023.05.13 Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wanawake Wakatoliki Duniani WUCWO.  (Vatican Media)

Papa kwa WUCWO:endelezeni shauku ya Injili katika Kanisa na jamii!

Papa akikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wanawake Wakatoliki Duniani WUCWO,amewaeleza kuwa siri ya ufuasi wote na utayari wa utume huko katika kukuza umoja huo na umoja kutoka ndani na mgeni mtamu wa roho ambaye huwasindikiza kila wakati kumpenda Mungu na kubaki katika umoja naye,kama matawi kwenye mzabibu.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Jumamosi tarehe 13 Mei 2023 asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa  Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wanawake Wakatoliki Duniani WUCWO, UMOFC, uliofunguliwa Assisi na utaendelea mjini Asisi. Hawa ni wanawake 1500 kutoka duniani kote ambao wamewakilisha umoja huo wa wanawake katika makanisa yote katoliki ulimwenguni. Shirikisho hili linawaunganisha wanawake wakatoliki zaidi ya milioni 8 kwa kadiri ya hotuba ya Bi  Maria Lìa Zervino, Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wanawake Wakatoliki Duniani. Kwa hiyo katika hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko amewakaribisha waliokuwapo na wale ambao walikuwa wanafuatialia moja kwa moja  kwa njia ya Mtandao na ambao ni sehemu ya umoja huo kutoka sehemu mbali mbali za dunia na familia zao, kwa kujikita katika roho ya kikanisa na iliwarudi na shauku kubwa katika sehemu wanakotokea. 

Furaha ya wanawake kukutana na Papa
Furaha ya wanawake kukutana na Papa

Papa amewapa salamu na kuwashukuru kwa hotuba yao ambayo ilitangulia ikielezea kazi zao na mipango ambayo wanapeleka mbele. Baba Mtakatifu amebainisha kuwa kwa uwepo wao wanataka kujiandalia mkutano wao Mkuu ambao utafanyika huko Asisi. Wanaweza kuufanya wote kwa kusindikizwa kwa sala ili waache waongozwe na Roho na iwe fursa ya kupyaishha njia yao ya kimisionari kwa kufuata misingi asili ya waanzilishi wa Umoja huo na wakati huo huo kwa kutazama wakati ujao kwa matumaini na mtazamo wa macho na ufunguzi wa mioyo katika ulimwengu, kwa ajili ya kusikiliza kilio cha wanawake wengine ulimwenguni ambao wanateseka na ukosefu wa usawa, ubaguzi na umaskini.

Washiriki wa Mkutano wa Shirikisho la Umpja wa wanawake katoliki duniani
Washiriki wa Mkutano wa Shirikisho la Umpja wa wanawake katoliki duniani

Uchunguzi wa Wanawake ulimwenguni ambao walianzisha utawapatia maelekezo kwa ajili ya kubainisha mahitaji na kuweza kuwa wa wasamaria, wasindikizaji wa safari ambao wanadumisha matumaini na utulivu katika mioyo kwa kusaidia na kufanya namna ambayo wengine wanawasaidiwa kutuliza mahitaji ya mwili na kiroho ya ubinadamu. Kila siku kuna dharura ya hitaji la kupata amani duniani, amani ambayo inaanzia kwanza ndani ya moyo, yaani moyo wa mgonjwa, uliochanika na migawanyiko, chuki na hasira. Zaidi ya amani, kuna  hatari za utambulisho wa kibinadamu wa mwanamke kwa sababu anatumia kama mada ya mabishano ya kisiasa na itikadi za kiutamaduni ambazo hupuuza uzuri ambao aliumbwa nao.

Ni lazima kuthamanisha kwa kiasi kikubwa cha uwezo wake wa uhusiano na kujitoa na kwamba wanaume wanaweza kuelewa vema utajiri wa pamoja walio nao wanawake, ili kurudisha yale mafundisho ya ubinadamu ambao una tabia ya utamaduni wa kibinadamu na ule  wa mwanamke na nafasi yake katika familia na katika jamii, mahali ambapo hauzimwi ndani ya moyo unaodunda.  “Na ikiwa tunataka kujua ubinadamu ni nini bila wanawake, mwanaume ni nini bila wanawake, tunayo kwenye ukurasa wa kwanza wa Bibilia kwamba kuna upweke. Mwanaume bila mwanamke yuko peke yake. Ubinadamu bila mwanamke uko peke yake. Utamaduni bila wanawake uko peke yake.  Kwa hiyo mahali ambapo hakuna mwanamke, kuna upweke, ambao huzalisha huzuni na kila aina ya madhara kwa wanadamu. Pasipo mwanamke, kuna upweke.”  Papa amekazia kusema.

Mkutano wa papa na Wanawake wa Umoja Katoliki duniani
Mkutano wa papa na Wanawake wa Umoja Katoliki duniani

Baba Mtakatifu amekumbusha juu ya siku ya maadhimisho ya matukio ya Bikira Maria kwa watoto wachungaji wa Fatima. Papa amesema: “Na hata leo nina huzuni sana, kwa sababu katika nchi ambapo Bikira alionekana sheria ya kuua imetangazwa, hatua zaidi katika orodha ndefu ya nchi zilizo na euthanasia.” Kwa hiyo "leo tukimfikirie Bikira, tumuangalie Maria kama kielelezo cha mwanamke bora, ambaye anaishi zawadi na kazi kwa ukamilifu: zawadi ya umama na kazi ya kutunza watoto wake katika Kanisa.” Papa akiwatazama amewaleza wao kama wanawake: “mnamiliki karama hii na kazi hii, katika kila eneo mlipo, mkijua kwamba bila ninyi maeneo haya yako peke yake. Si vyema kwa mwanamume kuwa peke yake, kwa maana hiyo yupo mwanamke”. Baba Mtakatifu akitazama sura ya Mama Yetu amesema: “Maria anafundisha kuzalisha uhai na kuulinda daima, kuhusiana na wengine kuanzia na upole na huruma na kuchanganya lugha tatu: ile ya akili, ya moyo na ya mikono, ambayo inapaswa kuratibiwa, kama kichwa kinafikiri basi, moyo unahisi na mikono inafanya hivyo, kile ambacho moyo unahisi na kinaendena na kile ambacho mtu anafikiri kichwani na mikono hufanya, kile kinachofanywa na mikono kinapatana na kile mtu anachohisi na kile anachofikiri.

Mkutano wa Papa na wanawake katoliki
Mkutano wa Papa na wanawake katoliki

Papa amekumbusha kama alivyosema katika matukio mengine, anaamini kwamba wanawake wana uwezo huu wa kufikiri kile wanachohisi, kuhisi kile wanachofikiri na kufanya, kile wanachohisi na kufikiria.  Kwa hiyo amewahimiza wanawake hao kuendelea kutoa usikivu huu katika huduma ya wengine. Kwa kurudi tena suala la Fatima, Papa amesema  katikati ya ukimya na upweke wa mashamba, mwanamke mzuri aliyejaa mwanga alikutana na watoto maskini na wa kawaida. Kama katika mambo yote makuu ambayo Mungu hufanya, umaskini na unyenyekevu hunaoneshwa katika tukio hilo. “Katika wale wachungaji wadogo sisi pia tunawakilishwa  yaani wanadamu wote wadhaifu na wadogo,na tunaweza hata kusema kwa kushangaa na kuogopa kabla ya matukio yanayotokea katika maisha na ambayo wakati mwingine tunashindwa kuelewa, kwa sababu matukio hayo yanatuzidi na kuweka sisi katika mgogoro”.

Umoja wa wanawake katoliki duniani
Umoja wa wanawake katoliki duniani

Katika muktadha huo uliomulikwa na udhaifu, amesema ni lazima tujiulize: “ni nini kilimfanya Maria kuwa na nguvu? Ni nini kiliwapa nguvu wachungaji wadogo kufanya walichoombwa? Je, ni siri gani iliyowageuza wale watu dhaifu na wadogo kuwa mashahidi wa kweli wa furaha ya Injili? Katika kujibu Papa amesema siri ya ufuasi wote na utayari wa utume huko katika kukuza umoja huu, umoja kutoka ndani, ndani na mgeni mtamu wa roho ambaye hutusindikiza kila wakati: kumpenda Mungu na kubaki katika umoja naye, kama matawi kwenye mzabibu (rej. Yn 15, 1-11). Kwa hiyo ni kuishi kama Maria utimilifu wa kuwa wanawake na ufahamu wa kujisikia waliochaguliwa na wahusika wakuu katika kazi ya kuokoa ya Mungu. Lakini hiyo tu haitoshi. Muungano huo wa ndani na Yesu lazima ujionesha kutoka ndani kwa kubaki na umoja na Kanisa, familia binafsi au katika shirika binafsi, ambayo inasaidia kukomaa katika imani.

Mwenyekiti wa Umoja huo wa Wanawake akitoa hotuba yake
Mwenyekiti wa Umoja huo wa Wanawake akitoa hotuba yake

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa h iyo ndio maana ya kutoa thamani kwa mipango yote inayoanzishwa na ambayo wao wanapeleka mbele. Lazima kusali kwa ajili ya kazi na kutenda kwa kile ambacho kimeonekana katika sala  ili kuingia katika maelewano na utume wa Kanisa zima.  Sinodi pia ni muhimu ambayo inafanya kuwa mstari wa mbele na kuwajibika katika kuwa mwema kwa Kanisa, na kwa kujua kufungamanisha tofauti na kufanya kazi kwa maelewano ya kikanisa. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa kila watendalo na kuwatia moyo wa kuendelea mbele kwa shauku katika mipango yao na shughuli kwa ajili ya kusaidia uinjilishaji, kwa kufuata sauti ya ndani ya Roho Mtakatifu, nyororo, kwa miguso ya ndani. Na kwamba Yesu awabariki na Bikira Maria wa Fatima awalinde wao na familia zao. Papa anasali kwa ajili ya matunda ya Mkutano wao. Amehitimisha kwa kuwaomba wasisahu kumsindikiza katika sala zao.

Hotuba ya Papa kwa wanawake wakatoliki duniani
13 May 2023, 14:19