Tafuta

Mazungumzo ya Papa Francisko na wanashirika wa kijesuit. Mazungumzo ya Papa Francisko na wanashirika wa kijesuit.  (ANSA)

Papa kwa Wajesuit wa Hungaria

Umuhimu wa ushuhuda,zawadi ya huruma,mazungumzo kati ya vizazi.Ni baadhi ya mada ambazo Papa alizungumza mwishoni akiwa huko Budapest katika mkutano wa faragha na Wajesuit katika ziara yake ya 41 ya kitume.Mahojiano kamili yamechapishwa katika tovuti ya 'La Civiltà Cattolica'.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa vijana inahitajika kuzungumza nao kama watu wazima, sio kama watoto, kwa sababu wanahitaji ushuhuda na ukweli. Hata katika Kanisa ni muhimu ili kukabiliana na kuzungmza nyuma nyuma, kutoa majibu dhidi ya usasa, ambayo yanageuka kuwa ugonjwa wa kujutia. Haya na mengine ni baadhi ya tafakari ambazo Papa alikuwa nazo katika mkutano wake wa faragha na Wajesuit wa Hungaria, uliofanyika katika makao ya watawa hao huko Budapest, Jumamosi tarehe 29 Aprili 2023, siku moja baada ya kuwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo (Magyar.) Mazungumzo ya Askofu wa Roma na Wajesuit yameripotiwa katika makala ya  gazeti la La Civiltà Cattolica, ( un articolo della rivista La Civiltà Cattolica) iliyotiwa saini na mkurugenzi wake Padre Antonio Spadaro , tarehe 9 Aprili 2023.

Papa Francisko alijibu maswali saba yaliyoulizwa na baadhi ya Wajesuit 32 waliokuwepo katika mkutano huo wa faragha ambao kama utamaduni wake, kila ziara yake ya kitume, hukutana na jumuiya ya shirika lake. Swali la kwanza lilihusu vijana hasa uchungaji unaotolewa kwao na jinsi ya kuishi na waamini hao. Papa alipendekeza neno la kutoa ushuhuda, ambalo linamaanisha mshikamano wa maisha, vinginevyo  alisema: “tunaishia kama wimbo wa Mina, usemao ‘maneno, maneno, maneno’, lakini bila ushuhuda, hakuna kinachofanyika! Kwa hivyo ushuhuda pia unamaanisha uthabiti, kwa sababu vijana hawavumilii lugha mbili, vile vile  pamoja na vijana katika mafunzo lazima mtu azungumze kama mtu mzima, kama wasemavyo kuwa na  watu wazima na sio watoto. Kisha Papa alisisitizia umuhimu wa mazungumzo kati ya vijana na wazee, kwa sababu alisema unabii wa kijana ni ule unaotokana na uhusiano mpole na wazee.

Wakiendelea na mazungumzo yao, mmoja wa Padre Mjesuit alimuuliza Papa Francisko ni nini kilimsukuma kurudi Budapest. Kwa jibu lake alisema “Kwa  sababu ukweli ni kwamba mara ya kwanza alilazimika kwenda Slovakia, lakini alipitia hapo katika Kongamano la Ekaristi lililokuwa linafanyika Budapest. “Kwa hivyo nilikuja hapa kwa masaa machache. Lakini niliahidi kurudi na nimerudi” alisema askofu wa Roma. Katika kuzungumza tena juu ya vijana, umakini ulikwenda kwa maneno mawili kuhusu uhalisi na huruma. Papa alisema hata hivyo maneno yao ni mojawapo ya maneno muhimu ya Mungu  yaani ukaribu, huruma na upole. Huu ndiyo mtindo wa Mungu.  Na kisha kuwaacha vijana wawe huru wa kuwa wa kweli, kuzungumza ni nini wanahisi."

Papa aliulizwa jinsi ya kupenda kama ndugu hata wale ambao wamefanya unyanyasaji wa kijinsia, kutoa huruma ambayo Injili inaomba kwa kila mtu, hata wale ambao wamehukumiwa.  Katika suala hilo “Sio rahisi hata kidogo, swali lako ni kali sana, Papa Francisko alijibu, akielezea jinsi ambavyo “mnyanyasaji lazima ahukumiwe, lakini kama ndugu”. Kwa maana hiyo, “kumhukumu ni kueleweka kuwa ni tendo la hisani”, kwa sababu “kuna mantiki, njia ya kumpenda adui ambayo inaoneshwa hata kwa namna hiyo” ingawa si rahisi kueleweka.  "Wao pia  ni watoto wa Mungu. Na tunahitaji huduma ya kichungaji. Wanastahili adhabu, lakini pia uchungaji," Papa alisisitiza.

Papa pia aliombwa kuzungumzia uhusiano wake na Padre Ferenc Jálics, Mjesuit ambaye mnamo mwaka 1976, huko Argentina, alifungwa ndani ya shimo la ESMA, mojawapo ya vituo vikubwa vya vifungo, mateso na kutokomeza udikteta wa Argentina. Utawala wa kijeshi ulijaribu kumshirikisha Askofu wa jimbo wakati huo Askofu Bergoglio akiwa mkuu wa Shirika ambaye badala yake alifanya kila awezalo kumuokoa. Papa alisema: “Jálics alikuja kwangu mara moja na tukazungumza” huku akikumbuka kuachiliwa kwake, ambako ilifanyika baada ya kupata “vitisho na mateso”. Papa aliongeza kusema kuwa: “Nilimshauri aende kwa mama yake Marekani, lakini kulikuwa mbali sana na  kuchanganyikiwa na uhakika.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kwamba  lakini "waliendelea kusema kuwa ni mimi niliyewakabidhi ili afungwe". Jueni kwamba mwezi mmoja uliopita Baraza la Maaskofu wa Argentina lilichapisha vitabu viwili kati ya vitatu vilizopangwa na nyaraka zote zinazohusiana na kile kilichotokea kati ya Kanisa na jeshi. Tafuteni kila kitu hapo.” Papa Francisko aidha alimkumbuka Mjesuit mwingine aliyekamatwa, Orlando Yorio. “Ninataka kuongeza kwamba wakati Jálics na Yorio walipo chukuliwa na jeshi, hali nchini Argentina ilichanganyikiwa na haikuwa wazi hata kidogo nini kifanyike. Nilifanya nilichojisikia kuwatetea. Ilikuwa historia chungu sana”, Papa alisema.

Hatimaye swali liliulizwa juu ya Mtaguso wa II wa Vatican kwa namna ya pekee namna ya kupata sauti ya Mungu kwa kupenda wakati wake. Papa alisema: “Baraza bado linatumika na anajua kuwa upinzani ni mbaya. Kuna marejesho ya ajabu". Kwa hivyo mwaliko wa kutoogopa kubadilika, kwa sababu kurudi nyuma hautawahi kuweka maisha, mema kamwe. Lazima ibadilishwe, wakati leo hii kuna hatari  ya kutaka kurudi nyuma,  majibu dhidi ya kisasa , ndiyo hayo ya  gonjwa wa kujutia yaliyopita. Hii ndio sababu Papa aliezeliza: “niliamua kwamba sasa ni lazima kupata makubaliano ya kusherehekea  maahdimisho kulingana na Misale ya Kirumi ya 1962 kwa makuhani wote wapya ambao wanawekwa wakfu. Baada ya mashauriano yote muhimu, niliamua kwa sababu niliona kwamba hatua hiyo ya kichungaji iliyotengenezwa vizuri na Yohame Paulo II na Benedikto XVI ilitumiwa kiitikadi ya kutaka kurudi nyuma”.

09 May 2023, 18:18