Tafuta

2023.05.11 Wajumbe wa Mkutano wa Taasisi za Kimisionari Italia wamekutana na Papa Francisko. 2023.05.11 Wajumbe wa Mkutano wa Taasisi za Kimisionari Italia wamekutana na Papa Francisko.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Taasisi za kimisionari anasema Utume ni Oksijeni kwa maisha ya kikristo!

Utume ni oksijeni katika maisha ya Kikristo,ambayo bila hiyo hupata ugonjwa na kunyauka na kuwa mbaya sana.Ni kutokana na mtazamo huu kwamba mnafanya kazi,kupitia kubadilishana uzoefu,uhuishaji wa kimisionari wa jumuiya za mahalia.Ni katika hotuba ya Papa alipokutana Taasisi za Kimisonari Italia wakiadhimisha miaka 50 tangu kuanza umoja.

Na Angella Rwezaula, -  Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 11  Mei 2023, amekutana mjini Vatican na Washiriki wa Mkutano wa Taasisi za Kimisionari  nchini Italia ambapo katika hotuba yake ameonesha furaha ya kukukaribisha kwenye kumbukumbu ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo. Kwa muda wa nusu karne wamejitolea kutangaza utume huko Italia, na kukufanya sauti ya maelfu ya wamisionari wanaume na wanawake ambao, wakijitoa wenyewe kwa utangazaji wa Kristo, walizungumza na kila mtu kuhusu hali ya maisha ya Kikristo, mwelekeo wa kimisionari, unaofaa kwa kila mtu aliyebatizwa kwa nguvu ya Ubatizo. Mtaguso wa Pili wa Vatican unasema waziwazi kwamba: “Kanisa zima ni la kimisionari, na kazi ya uinjilishaji ni wajibu wa kimsingi wa Watu wa Mungu” (Ad gentes, 35). Kwa sababu hiyo, katika Wosia wake wa Kitume wa Evangelii gaudium, aliwaalika Wakristo kujiimarisha katika maeneo yote ya dunia katika 'hali ya kudumu ya utume'” (n. 25). Tangazo kwa ajili ya Kanisa si jambo la hiari au la pembeni, bali ni mwelekeo muhimu, kwa vile lilizaliwa la kitume na kimisionari, lililoundwa na Roho Mtakatifu kama jumuiya inayotoka nje (taz. Katekesi, 15 Machi 2023). Utume ni oksijeni kwa maisha ya Kikristo, ambayo bila hiyo hupata ugonjwa na kunyauka (tazama ibid.), na kuwa mbaya sana.

Papa amekutana na wamjumbe wa Mkutano wa Taasisi za kimisionari Italia
Papa amekutana na wamjumbe wa Mkutano wa Taasisi za kimisionari Italia

Ni kutokana na mtazamo huu kwamba wanafanya kazi, kupitia kubadilishana uzoefu, uhuishaji wa kimisionari wa jumuiya za mahalia, uhamasishaji wa vijana katika seminari, uhuishaji wa ufundi, mchango wao katika kuandaa hati za kimisionari katika ngazi mbalimbali, harambee pamoja na ukweli mwingine wa kikanisa kama vile Caritas, Missio na Wahamiaji kwa ajili ya kukuza kukubalika kati ya watu na tamaduni na kwa ajili ya hadhi ya  mtu katika kila sehemu ya dunia. Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo waendelee kwa ujasiri, ili nguvu za Roho daima ziwe katika Kanisa na katika ulimwengu kwa  akili na mioyo yenye shauku ya kupanda Neno na kuleta furaha ya Yeye Mfufuka kwa wote, kuvunja vizuizi na kutia moyo katika ujenzi wa jamii inayosimikwa katika kanuni za Kiinjili za upendo, haki na amani. Kwa hakika katika miaka ya shirika lao , Mtakatifu Paulo wa Sita, akizungumzia utume, alikumbuka baadhi ya mambo ya msingi: ushuhuda wa maisha, mahubiri ya Neno, katekesi na adhimisho la sakramenti (taz. Evangelii nuntiandi, 40-48). Ikijengwa juu ya nguzo hizi na kuhuishwa na Roho Mtakatifu, jumuiya ya kwanza ya Kikristo ilichota maongozi na nguvu kwa ajili ya kutangaza Injili (Mdo 2:42-47).  Papa amewaomba uwe ndio  mtindo wao pia. Na sio juu ya kugeuza imani kwa sababu hiyo  sio ya Kikristo. Mtindo wao wa kumtangaza Kristo kwanza kabisa ni  kwa ushuhuda wa maisha ya mtu. Kwa hili amependekeza kwamba kwanza kabisa wakeze upendo ndani na kati ya jumuiya zzp, ndani na kati ya Taasisi zao  wakipatanisha tofauti za tamaduni, umri, mawazo, ili katika shirika kila karama iwe katika huduma ya wote (taz. 1 Kor. 12:4-7; Katekesi, 1 Oktoba 2014).

Papa na Taasisi za Kimisionari Italia
Papa na Taasisi za Kimisionari Italia

Na iweni moyoni mwa kuwakaribisha maskini na wadogo, baina yao na kwa watu wanaowahudumia katika huduma yao, kwa roho ya ushirikishwaji na huduma. Na hilo liwe tangazo lao la kwanza la furaha ya Pasaka. Kwa kusudi hili, kama wanafunzi wa kwanza, wasikose kumwilisha maisha yao na utume wao kwa Neno la Mungu, Ekaristi na sala. Kiukweli, utume, kama umoja, juu ya yote  ni fumbo la neema. “Si kazi yetu, bali ni ya Mungu; hatufanyi hivyo peke yetu, bali tukiongozwa na Roho na kuwa wanyenyekevu kwa utendaji wake. Utume na ushirika huchipuka kutokana na maombi, hutengenezwa siku baada ya siku kwa kusikiliza Neno la Mungu,  tunasikikizwa wakati tuna Sali na kuwa lengo lao kuu la wokovu wa kaka na dada ambao Bwana anatukabidhi. Bila misingi hiyo huwa tupu na kuishia kupunguzwa kwa mwelekeo wa kijamii au ustawi tu. Na Kanisa halipendezwi na ustawi... Inasaidia ndiyo, lakini kwanza kabisa kuinjilisha, kutoa ushuhuda: ikiwa unafanya ustawi, basi itokee kwa ushuhuda, lakini sio kutoka kwa njia za kugeuza watu imani. Kwa hiyo, si tu maisha yako na kazi yako ya kiutume, bali pia mipango yako, mikutano na maamuzi yako daima yawe alama kwa kusikiliza Neno, kwa adhimisho la Ekaristi na kwa sala. Kwa pamoja na kibinafsi, mkabidhi Mungu kila kitu, mkisafisha mioyo yenu na taasisi ambazo mnafanyia kazi kila kitu ambacho kinaweza kuzuia utendaji wa bure na wa ubunifu wa Roho”.

Papa na Taasisi za Kimisionari
Papa na Taasisi za Kimisionari

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha amekumbusha kifungu kingine kutoka kwa Waraka wa Evangelii gaudium, ambapo inakumbukwa kwamba utume si biashara au mradi wa kampuni, wala shirika la kibinadamu au uongofu. Ni “jambo la ndani zaidi, lisiloepuka kipimo chote” (taz. n. 279). Huu ni mwaliko wa kutumika  kujitolea, kwa ubunifu na ukarimu, lakini bila kukata tamaa ikiwa matokeo hayalingani na matarajio; kujitolea kilicho bora zaidi, bila kujihurumia, lakini baadaye kukabidhi kila kitu kwa uaminifu katika mikono ya Baba; kutoa kila kitu, lakini kumwachia  awez yeye ambaye anazalisha matunda ya juhudi zetu kama anavyotaka. Hayo ndiyo yamekuwa matashi mema aliyowatakia kwa kazi yao. Amewashurku tena kwa huduma yao ya utume na umoja. Mama yetu wasindikiza. Amewabariki kutoka moyoni mwake na tafadhali ameomba wamwombee.

Hotuba ya Papa kwa taasisi za kimisionari
11 May 2023, 17:33