Tafuta

2023.05.11 Mkutano wa Papa Tawadros II, Patriaki wa kikopti kiortodhox wa  Alessandria na Papa Francisko na kuhitimisha kwa sala ya pamoja. 2023.05.11 Mkutano wa Papa Tawadros II, Patriaki wa kikopti kiortodhox wa Alessandria na Papa Francisko na kuhitimisha kwa sala ya pamoja.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa: Wakristo 21 wa Kikopti wajumuishwa katika kitabu cha Mashahidi

Mazungumzo ya faragha na sala ya pamoja tarehe 11 Mei kati ya Papa na Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la Kopti la Alexandria,katika Jumba la Kitume,miaka 50 tangu mkutano wa kwanza wa kihistoria kati ya Paulo VI na Shenouda III:“kuna matunda mengi ya uhusiano na Makanisa ya Mashariki.Shukrani kwa Mungu kwa hatua zilizochukuliwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu katika hotuba yake, Alhamisi tarehe 11 Mei 2023 alipokutana na ugeni ambao  tayari alikuwa ameunganika nao katika Katekesi yake ya Jumatano tarehe  10 Mei alisema “Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, na tushangilie na kuifurahia! Miaka hamsini iliyopita, ilikuwa ni kwa matamko haya ya Pasaka ambapo Papa Mtakatifu Paulo wa Sita alimkaribisha mtangulizi wako mwenye heshima, Papa Shenouda III, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Ni kwa shangwe kama hizo ninakukaribisha leo, ndugu yangu mpendwa na rafiki mpendwa Tawadros. Ninakushukuru kwa dhati kwa kukubali mwaliko wangu wa kuadhimisha pamoja jubilei ya tukio hili la kihistoria mwaka wa 1973, pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya mkutano wetu wa kwanza mwaka wa 2013.” Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema katika safari ya kiekumene, ni muhimu kutazama mbele daima.

Mgeni wa Papa Tawadros
Mgeni wa Papa Tawadros

Kwa kusitawisha mioyoni mwetu ili kwezesha subira yenye afya na hamu ya dhati ya umoja, ni lazima tuwe, kama Mtume Paulo,  asemaye tukitazama wakati ujao (rej. Fl 3:13) na kujiuliza mara kwa mara: “Quanta est nobis via?” Je, ni umbali gani umesalia kufika? Hata hivyo, ni lazima pia kukumbuka, hasa katika nyakati za kuvunjika moyo, kushangilia katika njia ambayo tayari imefunikwa na kutegemea bidii ya mashujaa waliotutangulia. Kuangalia mbele na kukumbuka. Na bado, bila shaka ni muhimu hata zaidi kutazama juu, kumshukuru Bwana kwa hatua zilizochukuliwa na kumsihi atupatie zawadi ya umoja unaotamaniwa.

Baba Mtakatifu Francisko ameshukuru kwa kusali pamoja na kwamba hilo ndilo dhumuni la ukumbusho wao. Kwa kuongeza alisema Mkutano wa Watangulizi wao ambao ulifanyika Roma kuanzia tarehe 9 hadi 13 Mei 1973, uliashiria hatua ya kihistoria katika uhusiano kati ya Kiti cha Mtakatifu Petro na Kiti cha Marko. Ilikuwa ni mkutano wa kwanza kati ya Papa wa Kanisa la Kikoptic kiorthodox na Askofu wa Roma. Pia iliashiria mwisho wa mabishano ya kitaalimungu  ya Baraza la Chalcedon, shukrani kwa kutiwa saini, mnamo tarehe 10 Mei 1973, kwa tamko la kawaida la Kikristo la kukumbukwa, ambalo baadaye lilitumika kama msukumo wa makubaliano sawa na Makanisa mengine ya kiorthodox ya Mashariki.

Mgeni wa Papa wakati wa maombi
Mgeni wa Papa wakati wa maombi

Mkutano huo ulipelekea kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Kimataifa kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodox la kikoptic, ambalo mwaka 1979 lilipitisha Kanuni za utangulizi kuongoza utafutaji wa umoja kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodox la kikopti, lililotiwa saini na Papa Mtakatifu Yohane Paulo II na Papa Shenouda III, ambamo alithibitisha, kwa maneno ya kinabii, kwamba umoja tunaouwazia haumaanishi kunyonywa kwa mmoja kwa mwingine au kutawala kwa mtu juu ya mwingine. Ni katika huduma ya kila mtu kuwasaidia kuishi vyema zaidi karama mahususi walizopokea kutoka kwa Roho wa Mungu.” Tume hii iliyochanganyika ilifungua njia ya kuzaliwa kwa mazungumzo ya kitaalimungu yenye matunda kati ya Kanisa Katoliki na familia nzima ya Makanisa ya Kiorthodox la Mashariki, ambayo yalifanya mkutano wake wa kwanza mwaka 2004 huko Cairo, ulioandaliwa na Mtakatifu Shenouda. Papa ameshukuru Kanisa la Kiorthodox la kikoptic kwa kujitolea kwake kwa mazungumzo haya ya kitaalimungu.

Papa amemshukuru kwa  kwa umakini  wake wa kidugu unaoendelea kulipa kwa Kanisa Katoliki la Kikoptic, ukaribu ambao umepata usemi wa kupongezwa katika kuundwa kwa Baraza la Kitaifa la Makanisa ya Kikristo nchini Misri. Kama inavyoonekana, mkutano wa Watangulizi wao mashuhuri haujakoma kuzaa matunda katikamchakato wa safari ya Makanisa yao kuelekea ushirika kamili. Pia ni katika kumbukumbu ya mkutano wa 1973 ambapo yeye a likutana na Papa mjini Vatican kwa mara ya kwanza tarehe 10 Mei 2013, miezi michache baada ya kuchanguliwa kwake n ana baada ya kuanza upapa. Katika hafla hiyo, alipendekeza kusherehekea Siku ya Urafiki kati ya Wakopti na Wakatoliki kila Mei 10, ambayo imekuwa ikisherehekewa kwa wakati na Makanisa yao tangu wakati huo.

Baba Mtakatifu amebainisha kuwa linapokuja suala la urafiki, sura maarufu ya kikoptic ya karne ya nane inakuja akilini ikionesha Bwana akiweka mkono wake begani mwa rafiki yake, mtawa mtakatifu Mena wa Misri. Sura   hii wakati mwingine inaitwa picha  ya urafiki kwa sababu Bwana anaonekana kutaka kuandamana na rafiki yake na kutembea naye. Vile vile, vifungo vya urafiki kati ya Makanisa yetu yanatokana na urafiki wa Yesu Kristo mwenyewe na wanafunzi wake wote ambao yeye mwenyewe anawaita"rafiki" (rej. Yn 15:15), na ambao anafuatana nao katika safari yao, kama alivyofanya nao. Emmaus mahujaji. Katika safari hii ya urafiki pia Papa amesema tunasindikizwa na wafiadini, ambao wanashuhudia kwamba “hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yn 15:13).

Picha ya Pamoja na ugeni wa mkuu wa Kanisa ka Kikopti na Papa
Picha ya Pamoja na ugeni wa mkuu wa Kanisa ka Kikopti na Papa

Zaidi ya hayo  Papa amekazia kusema kuwa zaidi ya neno la kueleza shukrani zake kwa zawadi ya thamani ya masalio ya mashuhuda wa Kikopti waliouawa nchini Libya mnamo tarehe 15 Februari 2015. "Wafiadini hao hawakubatizwa tu kwa maji na Roho, bali pia katika damu, kwa damu ambayo ni mbegu ya umoja kwa wafuasi wote wa Kristo". Papa Francisko kwa njia hiyo amesema kuwa na “furaha kutangaza leo hii kwamba, kwa ridhaa ya Utakatifu wafiadini hawa 21 watajumuishwa katika Kitabu cha Mashahidi wa Kirumi kama ishara ya ushirika wa kiroho unaounganisha Makanisa yetu mawili”.  Kwa kuongezea amesema "Sala ya mashuhuda wa Kikopti, pamoja na ile ya Theotokos,(Mama wa Mungu) iendelee kuyafanya Makanisa yetu kukua katika urafiki, hadi siku yenye baraka ambapo tutaweza kusherehekea pamoja katika alatare  moja na kkumwilishwa kwa Mwili na Damu moja ya Mungu.Mwokozi, ili ulimwengu uamini (Yh 17,21)! Ameihitimisha.

Hotuba ya Papa na Tawadros
11 May 2023, 17:15