Tafuta

2023.05.09  Tarehe 10 Mei 1973,ulifanyika Mkutano kati ya Mtakatifu Paulo VI na Patriaki wa Kikiptiki Shenuda III  mjini Vaticani. 2023.05.09 Tarehe 10 Mei 1973,ulifanyika Mkutano kati ya Mtakatifu Paulo VI na Patriaki wa Kikiptiki Shenuda III mjini Vaticani. 

Papa Francisko na Tawadros II:Ni kuwa na subira ili kufikia umoja!

Papa na Patriaki wa Kiorthodox wa kikoptic kwa pamoja wametia saini ya utangulizi wa kitabu cha kumbukumbu kilichochapishwa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo wakati wa kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya mkutano wa kihistoria kati ya Papa Paulo VI na Patriaki Shenouda III.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kuna historia nyuma ya historia kuu ambayo mnamo tarehe 10 Mei 1973 iliongoza mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Paul VI, na lile la Kanisa la Kiorthodox la Kikoptic, Patriaki Shenouda III, ili kutoa nguvu mpya kwa ajili ya majadiliano na mchakato wa safari ya kutembea pamoja. Historia hiyo ni ile inayosimulia juu ya kurudishwa kwa Wakoptiki wa Kimisri kwa  sehemu ya masalio ya Mtakatifu Marko, anayeheshimika kama mwanzilishi wa Kanisa la Kiorthodox la kikoptik  ililoibwa mnamo 828 na kupelekwa Venezia nchini Italia. Kwa hiyo ishara ya Papa Montini yaani Papa Paulo VI, ilitoa uhai mpya kwa ajili ya uhusiano wa kiekumeni na masalia ambayo yamekuwa kwenye altare ndani ya Kanisa kuu la Kikoptic huko Cairo iliashiria hatua ya kwanza kati ya tarehe  9 na 13 Mei 1973, iliyoletwa kwenye mkutano kati ya Paul VI na Shenouda III, ambayo ilifikia kilele  tarehe 10 Mei kwa kutiwa saini kwa Azimio la pamoja.

Kitabu cha kumbukumbu

Miaka hamsini baadaye, walifuat waanzilishi wawili wa umoja, Papa Fransisko na Patriaki wa sasa wa Kikoptic Tawadros II, walitaka kukutana jijini Roma kushiriki maadhimisho na zaidi ya yote kumshukuru Mungu kwa kukumbuka hatua zilizochukuliwa na umbali ambapo tayari wamesafiri, ambayo mara nyingi ni muhimu zaidi kuliko tunavyofikiria. Wote wawili wanathibitisha hilo kwa kutia sahihi kwa pamoja utangulizi wa kitabu juu ya sherehe kilichochapishwa na Jumba la Uchapishaji la Vatican kwa niaba ya Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja, wa Kikirsot yenye mada, Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi la kikoptic. Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mkutano kati ya Papa Paulo VI na Papa Shenouda III (1973-2023), ambacho kitatokea tarehe 10 Mei.

Hatua za Kiekumeni

Katika kitabu hicho  ambacho kina nyaraka kuu zinazoshuhudia kukaribiana kati ya Makanisa mawili kuanzia Vatican II, Francisko na Tawadros II wanaangalia hatua muhimu ya mkutano huo wa kwanza, ambao ulifanyika miaka elfu na mia tano baadaye kati ya Askofu wa Roma na Papa wa Kanisa la Kikoptiki-Kiorthodox, kukumbuka hatua mbalimbali za mfululizo za kiekumeni, tangu kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Kimataifa na kazi yake  iliyoanza chini ya upapa wa Yohane Paulo II na Papa Shenouda III mwenyewe, hadi kufika mwaka 2003 katika msingi wa mazungumzo ya kitaalimungu kati ya Kanisa Katoliki na familia nzima ya Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki, majadiliano ambayo tayari yametoa hati muhimu zinazotoa ushuhuda wa uelewa unaokua kati ya Makanisa yetu, kwa mujibu wa ndondoo za kitabu.

Tuna muda gani wa kusafiri pamoja?

Maadhimisho ya miaka 40 ya utiaji saini wa kihistoria, yaliyoadhimishwa mwaka 2013 mwanzoni mwa upapa wa Papa Francisko, pia yalipelekea kuzaliwa kwa “Siku ya Urafiki kati ya Wakopti na Wakatoliki, ambayo tangu wakati huo imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka na Makanisa hayo mawili kila tarehe 10 Mei. Na  Jumatano tarehe 10 Mei kwa hiyo ni maadhimisho ya miaka 50, ambapo katika fursa hiyo  Patriaki Tawadros II atakuwa kwenye katkesi ya Papa  katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ili kufunga sio tu lengo lakini hata zaidi, kushiriki kuwa  na subira kwa afya kwa umoja mioyoni mwetu. ” ambayo huendelea kutufanya tujiulize: 'Quanta est nobis via' yaani tunapaswa kusafiri muda gani?”, ndivyo inasomeka katika utangulizi wa kitabu hicho. Kwa hiyo “upendo wa kindugu na urafiki unaounganisha Makanisa yetu  uendelee kukua hadi siku yenye baraka na inayotakikana ambayo tutaweza kuadhimisha pamoja kwenye madhabahu moja na kupokea kutoka kikombe kimoja, kwa sababu ulimwengu unaamini,” wanahitimisha Papa Francisko na Patriaki Tawadros II.

Maadhimisho ya Miaka 50 ya mkutano wa papa Montini na Shenouda III
09 May 2023, 16:29