Tafuta

2023.05.22 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia na Papa. 2023.05.22 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia na Papa.  (Vatican Media)

Papa azungumza na CEI kuhusu changamoto za leo za Kanisa na dunia

Takriban saa tatu za maswali na majibu kati ya Papa Francisko na Maaskofu wa Italia,waliokuwa kwenye Ukumbi Mpya wa Sinodi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 77.Miongoni mwa mada,kama ilivyoripotiwa na baadhi ya maaskofu kando ya mkutano huo ni:amani,fedha,mazingira,itikadi,huduma ya maaskofu na mapadre,upendo kwa maskini na wakimbizi.

Na Angella Rwezaula- Vatican

Vijana na miito, fedha na itikadi, huduma ya mapadre na seminari, amani, mazingira na makini na upendo. Mwisho ni sifa ya Kanisa la Italia ambalo ameonyesha heshima kubwa kwake. Yalikuwa ni mazungumzo ya wazi na tulivu mchana wa leo tarehe 22 Mei, kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Maaskofu zaidi ya 200 wa Baraza la Maaskofu wa Italia, waliokusanyika kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 77 mjini Vatican. Papa alifungua kazi ya mkutano wa machipuko ya maaskofu, unaoanza leo hadi tarehe 25 Mei katika Ukumbi Mpya wa Sinodi, yenye mada "Kusikiliza yale ambayo Roho anayaambia Makanisa. Hatua kuelekea utambuzi”.

Papa na CEI
Papa na CEI

Mazungumzo ya Papa na maaskofu wa mikoa yote ya Kaskazini, Kusini na Kati ya Italia yalichukua takriban saa tatu, ambayo yalianza mapema kwa muda wa sala ya pamoja na kwa salamu ya Papa kwa maaskofu wa maeneo yaliyoathiriwa na dhoruba huko Emilia-Romagna, Jumatatu alasiri tarehe 22 Mei 2023. Mkutano mzima, nyuma ya milango iliyofungwa, kisha uliingiliwa  kama kawaida katika hafla hizo  na maswali (takriban kumi na tano alasiri hii) na majibu. Miongoni mwa mada kuu, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya maaskofu pembezoni mwa mkutano, ni kupungua kwa miito, seminari na uwezekano wa kuunganishwa kwao. Mada, ya mwisho, pia iliyohutubiwa na Papa katika katekesi ya mwishoni mwa Machi iliyopita na maaskofu wa Baraza la Maaskofu la Calabrian.  Walizingatia pia huduma ya mapadre, ambao, kama kawaida, Papa aliwataka maaskofu waoneshe ukaribu.

Shemasi na Injili
Shemasi na Injili

Katika mkutano huo kulikuwa na kumbukumbu ya amani, katika Ukraine na katika dunia, uharaka ambao unahusu kila mtu, kisha kwa itikadi za wakati wetu, kisha matatizo mbalimbali ya kiutamaduni na suala la fedha, ambayo mara nyingi huwakilisha shida kwa Kanisa. Katikati pia matatizo ya mazingira ambayo mabadiliko ya mawazo ni muhimu. Mtindo mpya" pia inahitajika kwa njia ya sinodi inayohusisha Kanisa la mabara matano: mada ilikuwa katikati ya maswali. Pamoja na hili pia mwaliko wa kuzingatia umaskini, wa zamani na mpya, na zaidi ya yote tusiache upendo ushindwe. Hasa juu ya kipengele cha hisani, Papa alionesha heshima yake kwa Baraza la Maaskofu wa Italia, ambalo limehusika kwa miaka mingi katika kuwakaribisha wahamiaji na wakimbizi.

Na kwa usahihi juu ya mada ya wahamiaji, Papa Francisko, mwishoni mwa mkutano huo, alimpatia kila askofu wa CEI kitabu kiitwacho “Fratellino”, kitabu ambacho kinasimulia maisha ya mhamiaji Ibrahima Balde kwa uwazi na wakati mwingine mbaya  kilichaondikwa na  mshairi Amets Arzallus Antia. Ni kisa cha kijana kutoka Guinea ambaye aliondoka nchini mwake kwenda kumtafuta kaka yake mdogo, ambaye naye aliondoka kufika Ulaya. Lengo halikufikiwa kamwe. Mwandishi anaripoti majanga  aliojionea mwenyewe kuwanza kuvuka jangwa, biashara haramu ya binadamu, kifungo, mateso, safari za baharini, na kifo. Papa Francisko amekuwa akinukuu kitabu, kilichochapishwa nchini Italia na Feltrinelli, mara kadhaa, katika baadhi ya mikutano ya waandishi wa habari akiwa na  ndege inayorudi kutoka ziara zake za kitume, na katika baadhi ya mkutano.  La mwisho, lile la wakimbizi waliofika Ulaya kupitia mpango wa pamoja wa Mtakatifu Egidio, Makanisa ya Kiinjili, Meza ya Waldensia na Kanisa la Italia, lilipokelewa mjini Vatican  tarehe 18 Machi 2023. Papa alifafanua kijitabu hicho ambacho kinaelezea janga lake lote kama Njia ya Msalaba  wa kaka  dada wengi duniani kote.

Papa na Maaskofu wanaotoka katika maeneo yaliyokubwa na mafuriko na dhoruba
Papa na Maaskofu wanaotoka katika maeneo yaliyokubwa na mafuriko na dhoruba

Kando ya Mkutano huo, Baba Mtakatifu Francisko aliwasalimia maaskofu wa Mkoa wa  Emilia-Romagna, waliokumbwa na mafuriko yasiyoisha siku za hivi karibuni. Baada ya kusikia habari kuhusu watu wanavyopitia na kujifunza juu ya ishara nyingi za mshikamano zilizowekwa, Papa aliomba kupeleka ushiriki wake kwa jamii kwa kuhakikisha maombi ya kibinafsi. Alikuwa ni Kardinali Matteo Zuppi, rais wa  Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na askofu mkuu wa Bologna, ambaye mwanzoni mwa mkutano alielezea kile kilichotokea na dhoruba, hali mbalimbali ngumu zilizowapata watu na ishara nyingi za mshikamano na msaada.

Maaskofu Italia waanza mkutano wao
Maaskofu Italia waanza mkutano wao

Hatimaye Kardinali, Zuppi pamoja na makamu rais wa Ceer, Askofu Mkuu  Lorenzo Ghizzoni, wa Jimbo Kuu katoliki la Ravenna-Cervia,Askofu  Giovanni Mosciatti, wa Imola, Askofu  Livio Corazza, wa Forlì-Bertinoro, na Askofu Mario Toso, wa Faenza -Modigliana , walipata fursa ya kusalimiana na Papa binafsi na kutoa shukrani kwake"kwa ujumbe wake wa mshikamano katika siku za hivi karibuni. Katika dokezo, maaskofu walisisitiza kwamba wamekaribisha kichocheo cha Papa kwa ajili ya kutafakari zaidi juu ya heshima kwa Uumbaji na utunzaji  wa nyumba yetu ya pamoja. "Tulimkumbushakwamba watu wa Romagna ni wastahimilivu lakini majaribu yanajirudia mara kwa mara na kwamba tunahitaji maombi na ukaribu wake”, Walisema maaskofi hao.

Papa alizungumza nao kindugu
Papa alizungumza nao kindugu

Kuhusu mazungumzo ya Papa na maaskofu nyuma ya milango iliyofungwa, katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu, Askofu Giuseppe Baturi, pia aliripoti maelezo, akizungumza kwenye Televisheni ya Maaskofu (TV2000) ya mkutano muhimu kwa sababu unawasiliana na matatizo ya nchi na Kanisa.  Papa alisisitiza uharaka wa msukumo mpya wa uinjilishaji unaopitia kwa ushuhuda wa kuaminika... Maaskofu wanaitwa kuwa na huruma kwa mwanadamu, kumtunza hasa katika hali ya shida na mahitaji. Ulikuwa ni mkutano ambao ulitutia moyo kuendelea katika njia hii ambayo inapata katika safari ya sinodi njia adhimu ya majadiliano na kazi.

Papa na Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI)
23 May 2023, 16:01