Papa atakuwa#NotAlone,Mkutano wa kimataifa juu ya Udugu wa kibinadamu
Vatican News
Mkutano wa Kimataifa kuhusu Udugu wa Kibinadamu, unaoitwa(#notalone) yaani ‘Si peke yake’ utafanyika mbele ya Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 10 Juni 2023 saa kumi 10.00 jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican. Katika uwanja huo pia kutakuwa na washindi 30 wa Tuzo ya Nobel na maelfu ya vijana kutoka pande zote za dunia. Tukio hilo limeandaliwa na Mfuko wa Vatican wa ‘Fratelli tutti’, kwa ushirikiano na Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Baraza la Kipapa la Kuhamasisma huduma ya Maendeleo ya Binadamu, pamoja na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.
Kumbatio kubwa la vijana katika uwanja wa Mt. Petro
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Mfuko huo, “Mpango huo, uliochochewa na waraka wa Fratelli tutti, utahusisha watu kutoka ulimwenguni kote ili kuhamasisha na kukuza pamoja utamaduni wa udugu na amani na kuhimiza kujitolea kibinafsi katika chaguzi na mazoea ya fidia, mazungumzo na msamaha, kuondokana na upweke na kutengwa kunakonyima utu wa binadamu”. Tukio hilo hasa wanabainisha kwamba "litaona ushiriki wa uwakilishi wa kimataifa wa vijana ambao, mwisho wa siku, watashikana mikono, kwa mkumbatio mkubwa nguzo za Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambayo ni alama ya mkumbatio wa Kanisa la Ulimwengu".
Kujitolea kwa udugu wa kibinadamu
Siku, iliyofikiriwa kama mchakato na uzoefu wa kujenga udugu, itagawanywa katika nyakati mbili. Kwanza asubuhi baadhi ya vikundi vitakutana ili kushiriki njia za ushirika ambazo zitaelezwa kwa ufupi wakati wa mkutano wa jioni. Washindi wa Tuzo ya Nobel ambao hasa wamejiunga na mpango huo watakutana na kila mmoja na watu binafsi kutoka katika nyanja ya sayansi, utamaduni, sheria na mashirika ya kimataifa ili kuandaa waraka unaotaka kujitolea kwa ajili ya udugu wa kibinadamu, na kuwasilishwa kwa Papa Francisko katika Uwanja wa Mtakatifu Petro pamoja na Baba Mtakatifu, kwa watu wote duniani wanaojisikia wito wa kuchukua hatua za wito wa kujenga urafiki wa kijamii na dhana ya udugu, haki na amani. Mkutano huo utaoneshwa mbashara na televisheni na Vyombo vya Habari vya Vatican na, katika majukwa mbali mbali, kwenye tovuti Mfuko wa Fratelli Tutti (www.fondazionefratellitutti.org) na kwenye Facebook na YouTube chaneli za Mfuko wa Fratelli tutti.