Tafuta

Uwanja wa Mtakatifu Petro na mji wa Vatican. Uwanja wa Mtakatifu Petro na mji wa Vatican. 

Papa apyaisha Katiba ya Serikali ya Mji wa Vatican

Papa Francisko amepyaisha sheria mpya msingi ambayo inachukua nafasi ya ile ya mwaka 2000 “kwa ajili ya kijibu mahitaji ya nyakati zetu na kwa ajili ya kuruhusu shughuli za Kimataifa zinazohusiana na Vatican hata kwa ajili ya serikali.Tume ya Kipapa inapanuka na ambayo sasa itaundwa sio tu na makadinali bali hata walei.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa ajili ya kujibu mahitaji ya nyakati zetu kwa ajili ya kuruhusu shughuli za kitaasisi zinazohusiana na shughuli za kimataifa zinazotendwa na Makao ya Kitume, kwa kuupyaisha mahitahiji ambayo katika mantiki hiyo maalum yanahitajika, Baba Mtakatifu tarehe 13 Mei 2023,  katika Kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Fatima, amenzisha Sheria Msingi kwa ajili ya Serika ya Mji wa Vatican.Kwa maana hiyo Papa anapyaishwa hiyo “Katiba ya Mji wa Vatican inayochukua nafasi ya ile ya  tarehe 26 Novemba 2000 ya Mtakatifu Yohane Paulo II na ambayo ilikuwa inafuata ile iliyochapishwa mnamo tarehe 7 Juni 1929 na Papa Pio XI, kwa kutaka  “kuitikia mahitaji ya siku zetu na kufanya kazi katika hali zinazotokana na ahadi za kimataifa zilizofanywa na Kiti cha Kitume pamoja na mahitaji mapya ambayo kipengele hiki kinahusiana”.

Mageuzi hayo mapya  kwa hiyo ambayo yanalingana na mfumo wa mageuzi mengi yaliyofanywa katika miaka hii kumi ya upapa. Kwa hakika, Sheria inachukua na kukamilisha masasisho ya udhibiti ambayo tayari yametolewa na wasifu wa kitaasisi ambao umefanywa katika kazi Serikalini pamoja na marekebisho ya Sheria ya Vyanzo vya Sheria, Sheria ya Serikali ya Nchi na Sheria ya Mfumo wa Mahakama.

Kama katika Katiba ya 2000, Papa anathibitisha ukamilifu wa mamlaka ya serikali ya Papa ambayo inajumuisha mamlaka ya kutunga sheria, ya utendaji na ya mahakama. Pia iliyothibitishwa ilikuwa upekee na uhuru wa mfumo wa sheria wa Vatican, tofauti na ule wa Curia Romana uwezekane. Uwezo wa Serikali juu ya maeneo ya ziada ya eneo unathibitishwa, au tuseme utumiaji wa mamlaka yoyote juu ya eneo, iliyofafanuliwa na Mkataba wa Laterano, na katika majengo na katika maeneo ambayo taasisi za Vatican na Makao makuu ya Vatican, zinafanya kazi na zinatumika, chini ya sheria za kimataifa, dhamana za kibinafsi na za kiutendaji na kinga”.

Papa pia anathibitisha kazi ya kutunga sheria ya Tume ya Kipapa ya mji wa Vatican, ambayo hadi sasa ilikuwa inaudnwa na Kardinali rais (ambaye pia ni mwenyekiti) na makadinali wengine. Kwa Sheria mpya ya Msingi  huu moja ya mambo mapya ambapo  haitakuwa hivyo kwa sababu, pamoja na makadinali, wajumbe wengine walioteuliwa na Papa kwa muda wa miaka mitano pia wataingia kwenye Tume hiyo. Kwa hivyo walei wanaume na wanawake wanaweza pia kushiriki katika hilo.

Jambo lingine jipya muhimu linahusu udhibiti mkali na wa kina zaidi wa bajeti ya kuzuia na ya mashauriano ambayo hujadiliwa kila mwaka na Tume ya Kipapa, kwa kuzingatia kanuni za uhasibu na kwa vitendo vyenye nguvu ya sheria. Tume hiyo huamua juu ya mpango wa fedha wa miaka mitatu kwa kuwasilisha matendo haya moja kwa moja kwa idhini ya Papa. Bajeti lazima ihakikishe usawa wa mapato na matumizi na ihamasishwe na kanuni za uwazi, ukweli na usawa.

13 May 2023, 14:08