Tafuta

2023.05.26 Mahojiani ya Papa Francisko na Televisheni ya  'Telemundo'. 2023.05.26 Mahojiani ya Papa Francisko na Televisheni ya 'Telemundo'. 

Papa:amani itapatikana wakati Urussi na Ukraine zitakapoweza kuzungumza

Papa Francisko katika mazungumzo na Telemundo tarehe 25 Mei,kabla ya tukio la Scholas Occurrentes alikabiliana na mada ya wahamiaji wanaoondoka kwa sababu ya ya mahitaji,masuala utoaji mimba na useja ambao,alisemahayana uhusiano na unyanyasaji.Alieleza kuwa huwa anaomba sala kwa sababu waamini wanapomuombea mchungaji ni kana kwamba amevaa silaha.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Amani itapatikana siku watakapoweza kuzungumza baina yao au kupitia kwa wengine. Papa anaangalia janga ambalo limekuwa likifanyika nchini Ukraine kwa zaidi ya mwaka mmoja na, katika mahojiano na Telemundo, mtandao wa televisheni wa Marekani wa lugha ya Kihispania, uliofanyika tarehe 25  Mei 2023,  anaonesha nini kinaweza kuwa suluhisho la mzozo huo kwamba ni  mazungumzo.  Mazungumzo hayo na mwandishi wa habari Julio Vaqueiro yalifanyika tarehe 25 MeI,katika chumba cha Taasisi ya Augustinianum mjini Roma, mita chache kutoka Vatican, ambako Baba Mtakatifu Francisko alikutana na mameya wa Amerika ya Kusini na Ulaya walioshiriki katika mkutano wa mada ya "elimu ya mazingira na Scholas Occurentes. Ni Vaqueiro mwenyewe aliyesimamia mkutano huo. Hata hivyo kabla kwanza alifanya , mahojiano na Papa kuhusu mada za vita, masuala ya utoaji mimba na useja, afya yake, wahamiaji wanaoacha ardhi yao “kwa lazima”, sala ya waamini ambayo ni kama “silaha”.

Mkutano na Zelensky

Swali moja linahusu mkutano wa hivi karibuni  na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na maneno yaliyotolewa kwa vyombo vya habari kwamba hahitaji wasuluhishi. Papa  Francisko  alifafanua kuwa “Hii haikuwa sauti ya mazungumzo, na akisisitiza kwamba Zelensky “alimwomba fadhila kubwa sana na hiyo ni kuwatunza watoto waliopelekwa Urussi”. “Hawana ndoto ya upatanishi sana, kwa sababu kiukweli kizuizi cha Ukraine ni kikubwa sana, Ulaya yote na  Marekani kwa hivyo wana nguvu kubwa sana. Kinachomsababishia maumivu makali ni kujaribu kuwarudisha watoto Ukraine ameeleza, Papa “Ili kupata amani, unafikiri Urussi inapaswa kurudisha maeneo hayo? aliuliza mhoji. Jibu la Papa “Ni tatizo la kisiasa.”

Wahamiaji wanaokimbia kwa sababu ya ulazima

Tatizo lingine pia zito kwa Papa ni suala la uhamiaji ambalo anasisitiza haja ya mkakati ambao unaweza kukuza maendeleo na uendelevu wa nchi ambazo watu hukimbia Afrika, kwanza kabisa: “Wakati mmoja mwanamke, mwanasiasa mkubwa, alisema kwamba tatizo la uhamiaji wa Waafrika lazima litatuliwe huko  Afrika, kwa kuisaidia Afrika. Lakini kwa bahati mbaya Afrika ni mtumwa wa watu wasio na fahamu, kwa sababu Afrika inanyonywa. Msaada huo unafaa kutumika katika kuinusuru na kuifanya iwe huru”, alisema Papa.

Kitabu cha ndugu mdogo

Mawazo yaligeukia Sudan Kusini, iliyotembelewa hivi karibuni mwezi Februari uliopita, na watu wa ajabu ambao wamejipanga upya hivi karibuni.  Kwa hiyo Papa alishutumu kwamba: "Mamlaka ya kigeni mara moja yanaweka viwanda vyao huko, na sio kuifanya nchi kukua, lakini kuichukua, kuipora. Na kutoka hapo ndio chanzo cha  uhamiaji wote”. Katika muktadha huo Papa Francisko alitaja kitabu  cha “Ndugu Mdogo”, alichowapatia maaskofu wa Italia (CEI) jijini  Vatican Jumatatu tarehe 24 Mei. Kitabu hicho kinasimulia maisha ya mvulana ambaye aliondoka nchini Guinea kutafuta kaka yake na alichukua miaka mitatu kufika Hispania, akipitia utumwa, kifungo na mateso.  Kwa hiyo Papa alimshauri mwandishi huyo kukisoma ambapo ataona "majanga ya muhamiaji katika pwani ya Libya."

Uzoefu wa wahamiaji, bendera ya wawekezaji

“Kuhama ni kufa kidogo,” alisema mwandishi huyo wa habari, akimnukuu mkurugenzi wa Mexico Alejandro González Iñárritu. Papa Francisko alithibitisha: "Daima, kwa sababu mtu huacha ardhi yake mwenyewe". Papa alitoa mfano wake mwenyewe na familia yake kuwa: “Nilizaliwa Buenos Aires, lakini baba yangu alikuwa mhamiaji, tayari alikuwa mhasibu katika Benki ya Italia alipokwenda huko". Kwa hiyo hata asa, kama Papa ambaye anatoka Argentina (nchi ya wahamiaji na ambaye ameishi Roma kwa miaka kumi, anaendelea kuwa mhamiaji kidogo kwa sababu alisema: “Unaacha kitu kila wakati. Kinywaji cha Argentina “mate  unayojitengeneza kwa thermos kama hii, sio sawa na mate ambayo mama yako, au shangazi yako au bibi yako anakupatia, iliyotengenezwa muda huo. Ni kitu kingine. Unakosa hewa ya mahali ulipozaliwa.” Baba Mtakatifu (Papa Bergoglio) huku akinukuu shairi zuri sana la Nino Costa wa Piemonte, kuhusu kabila lao, alisema kuwa alisimulia hatima ya mhamiaji anayekwenda Amerika, ambapo alipata pesa nyingi lakini mwishowe alikufa mahali pasipojulikana. Kwa hiyo Papa aliongeza kusema: “ Mhamiaji anaweza kuwa tajiri na kufanya vizuri, au anaweza kuishia kuteseka vibaya ikiwa hatakaribishwa.”

Kutoa  mimba na useja

Mahojiano hayo pia yanataja masuala ya utoaji mimba na useja. Katika sehemu ya  kwanza, Papa alitaja mafunzo ya kiinitete, na ambacho tayari kwa mwezi mmoja baada ya mimba "yule aliye ndani ya tumbo la uzazi ni kiumbe hai. Kisha aliuliza swali Papa: “Je, ni halali kumuondoa kiumbe hai ili kutatua tatizo? Je, ni halali kuajiri muaji ili kutatua tatizo?”

Na kuhusu suala la useja wa kipadre na uhusiano unaodaiwa kuwa na unyanyasaji wa watoto katika Kanisa, Papa Francisko alijibu kwa kuripoti takwimu kwamba asilimia 32%, katika nchi nyingine 36% ya dhuluma hufanyika katika familia, mjomba, babu na wote walioolewa au na majirani. Baada ya hapo ni katika  kumbi za matamasha, baada ya hapo mashuleni…”. Kwa hiyo suala hilo halina uhusiano wowote na suala la useja", akiwa na maana kwamba unyanyasi unatokea kila sehemu.

Afya

Katika mazungumzo hayo hapakukosekana kutaja matatizo yake ya afya na goti. Papa alisema: “Kabla ni singeweza kutembea. Sasa ninaweza kutembea tena”, alitabasamu na kusema kwamba walimwambia iwapo wangesubiri "kwa masaa machache zaidi ingekuwa mbaya zaidi. Lakini ndani ya siku nne nilikuwa nje.”

Maombi kama silaha

Papa vile vile alieleza ni kwa nini anahitimisha kila hotuba ya Mkutano wowote ule  huku akiomba  wamwombee kwamba: “Wakati fulani watu hawatambui uwezo walio nao katika kuwaombea wachungaji wao. Na maombi ya waamini hufanya miujiza, kiukweli, hufanya miujiza. Kwa  mchungaji yeyote, awe paroko, askofu au mchungaji yeyote, ni kana kwamba anatetewa, amevalishwa silaha, amevaa silaha, kwa maombi ya waamini,”.

Mageuzi

Hatimaye, muhtasari wa haraka wa mageuzi yaliyofanywa katika miaka hii kumi ya upapa. Kwa uhalisia, Papa alieleza, si chochote zaidi ya kile ambacho makadinali waliomba katika mikutano ya kabla ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Papa kwamba : “mfumo wa kiuchumi, sheria mpya wa serikali ya Vatican, utunzaji wa kichungaji wa huduma ya Vatican. Na jukumu la wanawake. Kwa siku zijazo, hata hivyo, alisema anahisi bado anapaswa kufanya kila kitu. “Inachekesha, unapoendelea unagundua kuwa unakosa kila kitu”. Lengo moja kwa hakika ni kuondoa ukasisi ukasisi.  “Ukleri ni upotovu… Kama wewe ni kasisi, wewe si mchungaji. Mimi huwa ninawaambia maaskofu, mapadre na mimi mwenyewe tuwe wachungaji.”

 

29 May 2023, 10:17