Mazungumzo ya Papa na waandishi wa habari katika ndege:ishara za ubinadamu zinasaidia
Vatican News
Jitihada za Vatican katika kuwezesha kurudi nyumbani kwa watoto wa Kiukraine waliopelekwa Urussi wakati wa vita, amani, mawasiliano na Urussi na mazungumzo ya kiekumene, kwa kutaja afya yake baada ya kulazwa hospitalini Gemelli, Juma kabla ya Dominika ya Matawi. Na kurudi kwa mabaki ya masalia ya Parthenon hadi Ugiriki, ambao ni mfano kwa ishara mpya za siku zijazo kama hizo. Ni mada zilizoibuka wakati wa mazungumzo ya Baba Mtakatifu Francisko na waandishi wa habari katika ndege iliyokuwa inamrudishi jijini Roma kutoka katika ziara yake ya 41 ya kitume nchini Hungaria breve dialogo durante il volo,(unaweza kupata hapo mazungumzo hayo wakati wa safari) aliyoanza Ijumaa tarehe 28-30 Aptili 2023.
Ifuatayo ni nakala ya mahojiano ya Papa Francisko na waandishi wa habari kwenye safari ya ndege ya kurudi kutoka Hungaria: Antal Hubai (Rtl Klub)
Baba Mtakatifu, tunajua kwamba umekuwa na uzoefu mbalimbali wa kibinafsi na Wahungaria katika kipindi cha maisha yako: je, maono yako ya Wahungaria yamebadilika baada ya kukutana na wewe katika siku za hizi?
Ndiyo, kiukweli nilikuwa na uzoefu katika miaka ya 1960 nilipokuwa ninasoma nchini Chile, Wajesuiti wengi wa Hungaria, iliwabidi kwenda huko kwa sababu walifukuzwa kutoka Hungaria. Kisha nikabaki rafiki wa karibu wa Masista wa Hungaria wa Maria Ward, ambao walikuwa na shule umbali wa kilomita 20 kutoka Buenos Aires. Nilitembelea mara mbili kwa mwezi na nikafanya kama Padre wa kikanisa maalum. Kisha pia nikiwa na jamii ya Wahungaria ya watu walei Kihungaria wa Buenos Aires ambao walifanya kazi katika chuo cha Hungaria na hivyo hapo niliwatambua vema. Lugha sikuielewa ila nilielewa maneno mawili goulash na tokaj! Ilikuwa ni uzoefu mzuri na nilikuwa nashikwa na uchungu wa wale kuwa mkimbizi, kutoweza kurudi nyumbani na Masista wa Maria Ward waliobaki pale walikuwa wamefichwa kwenye vyumba ili utawala usiwachukue. Baadaye nilielezwa historia nzima kwa karibu zaidi ili kumshawishi Kardinali Mindszenty mwema kufika Roma na pia nilipata kujua shauku hiyo ya 1956 na kukata tamaa baadaye. Zaidi au chini ya hiayo
... lakini je, maoni yako kuhusu Wahungaria yamebadilika tangu wakati huo?
Hapana, haijabadilika: labda imetajirishwa, imetajirishwa kwa maana ya kwamba Wahungaria ambao niliwajua wana utamaduni mkubwa, utamaduni mkubwa; hata wale ambao hawakuwa wa tabaka la juu la kijamii, hata wale wa kawaida walikuwa na utamaduni wa hali ya juu sana. Kwa kawaida walizungumza Kijerumani au Kiingereza, kwa sababu Kihungaria hakizungumzwi nje ya Hungaria, ni Mbinguni pekee peke yake kinachozungumzwa kwa sababu wanasema inachukua milele kujifunza lugha ya kihungaria(alicheka). Na hilo halijabadilika, kinyume chake: Nimeona mtindo nilioujua.
Eliana Ruggiero (AGI)
Baba Mtakatifu, umezindua wito wa kufungua - kufungua tena - milango ya ubinafsi wetu kwa maskini, kwa wahamiaji, kwa wale ambao hawana utaratibu. Katika mkutano wako na waziri mkuu wa Hungaria Orbán, ulimwomba afungue tena mipaka ya njia ya Balkan ambayo alifunga? Halafu, katika siku hizi pia amekutana na Mkuu Hilarion. Je, Hilarion na Orbán mwenyewe wanaweza kuwa njia za kufungua kuelekea Moscow ili kuharakisha mchakato wa amani kwa Ukraine au kufanya mkutano kati yako na Rais Putin uwezekane? Asante.
Ninaamini kuwa amani daima hufanywa kwa kufungua mikondo,kamwe amani haiwezi kufanywa kwa kufungwa. Ninaalika kila mtu kufungua mahusiano, mikondo ya urafiki… Hii si rahisi. Hotuba ile ile ambayo kwa ujumla nimefanya, nimefanya na Orbán na nimeifanya kidogo kila mahali. Kuhusu uhamiaji: Nadhani ni tatizo ambalo Ulaya lazima ijikite nayo, kwa sababu kuna nchi tano ambazo zinateseka zaidi: Cyprus, Ugiriki, Malta, Italia, Hispania, kwa sababu ni nchi za Mediterania na wengi wanafika huko. Na ikiwa Ulaya haitasimamia hili, la usambazaji wa haki wa wahamiaji, tatizo litakuwa tu kwa nchi hizi. Ninaamini kwamba Ulaya lazima ijisikie kuwa ni Umoja wa Ulaya hata mbele ya hali hii. Kuna tatizo lingine linalohusiana na uhamaji, nalo ni kiwango cha kuzaliwa. Kuna nchi kama Italia na Uhispania ambazo… hazina watoto. Mwaka jana nilizungumza katika mkutano wa familia kuhusu hili na hivi karibuni nimeona kuwa serikali na serikali zingine pia wanazungumza juu yake. Umri wa wastani nchini Italia ni 46, kwa Uhispania ni kubwa zaidi na kuna vijiji vidogo vilivyo jangwa.
Mpango wa uhamiaji, lakini ambao umeendelezwa vyema na mfano ambao baadhi ya nchi zimekuwa nao wakati wa uhamiaji – ninafikiria, kwa mfano, Sweden wakati wa udikteta wa Amerika ya Kusini, inaweza pia kusaidia nchi hizi kiwango ambacho zina uzazi mdogo. Kisha, mwisho, ni nini cha mwisho? Ndio, Hilarion: Hilarion ni mtu ninayemheshimu sana, na tumekuwa na uhusiano mzuri kila wakati. Na alikuwa mkarimu kuja kuniona, kisha akaenda Misa na nikamwona hapo pia, kwenye uwanja wa ndege. Hilarion ni mtu mwenye akili ambaye unaweza kuongea naye, na mahusiano haya yanahitaji kudumishwa, kwa sababu tulizungumza juu ya uekumene, ninapenda hili, sipendi hili, lazima tunyooshe mkono na kila mtu, hata kupokea mkono. Nilizungumza na Patriaki Kirill mara moja tu tangu vita kuanza, dakika 40 kwa njia ya zoom, kisha kupitia Anthony, ambaye yuko katika nafasi ya Hilarion sasa, ambaye anakuja kuniona: yeye ni askofu ambaye alikuwa paroko, Roma na anajua mazingira vizuri, na mimi huwa ninawasiliana na Kirill kupitia yeye. Mkutano ambao tulipaswa kufanya huko Yerusalemu mnamo Julai au Juni mwaka jana unasubiri, lakini ulisitishwa kwa sababu ya vita: huo itabidi ufanyike. Na kisha, na Warussi nina uhusiano mzuri na balozi ambaye sasa anaondoka, balozi wa Vatican kwa miaka saba, yeye ni mtu mkuu, mtu comme il faut. Mtu makini, mwenye utamaduni, mwenye msimamo sana. Uhusiano na Warussi hasa ni kwa balozi huyo. Sijui kama nimesema kila kitu. Ilikuwa hivyo? Au nilikula kitu?
... ikiwa Hilarion na pia Orbán wangeweza kwa namna fulani kuharakisha mchakato wa amani nchini Ukraine na pia kuwezesha mkutano kati yako na Putin, ikiwa wanaweza kuchukua hatua - katika alama za nukuu - kama wasuluhishi...
Unaweza kufikiria kuwa katika mkutano huu hatukuzungumza tu juu ya ‘Cappuccetto Rosso’,yaana hadithi za kitoto sivyo? Tulizungumza juu ya mambo haya yote. Tunazungumza juu ya hili kwa sababu kila mtu anavutiwa na njia ya amani. Mimi niko tayari. Niko tayari kufanya chochote kinachohitajika ambacho kinapaswa kufanywa. Pia, utume unaendelea sasa, lakini bado haujaonekana hadharani. Wacha tuone jinsi ... nitasema itakapokuwa ya hadharani.
Aura Maria Vistas Miguel (Rádio Renascença)
Baba Mtakatifu, kituo kinachofuata ni Lisbon. Unajisikiaje kuhusu afya? Kwa sababu tulishikwa na mshangao ulipokwenda hospitali: kuna wengine walisema umezimia. Kwa hivyo unahisi nguvu ya kutembelea maelfu ya vijana katika siku hizo za Agosti huko Lisbon? Je, ungependa kumwalika kijana wa Kiukraine na kijana Mrussi kwenye Siku ya vijana WYD kama ishara ya amani pia kwa vizazi vipya?
Kwanza kabisa afya. Nilichokuwa nacho ni ugonjwa wa nguvu mwisho mwa Katekesi ya Jumatano, sikujisikia kula chakula cha mchana, nilijilaza kwa muda, sikuzimia, lakini ndio kulikuwa na homa kali, homa kali na saa tisa alasiri daktari alinipeleka hospitali mara moja: pneumonia kali na yenye nguvu, katika sehemu ya chini ya mapafu. Namshukuru Mungu ninaweza kusema, kwa kiasi kwamba kiungo, mwili, uliitikia vizuri matibabu. Asante Mungu. Hiki ndicho nilichokipata. Kisha Lisbon: siku moja kabla ya kuondoka nilizungumza na Monsinyo Américo (monsinyo Américo Manuel Alves Aguiar, askofu msaidizi wa Lisbon na rais wa Mfuko wa Siku ya Vijana (WYD 2023) ambaye alikuja kuona jinsi mambo yalivyo… Na ndio nitaenda, nitaenda, nitaenda na natumai kufanikiwa. Na unaona kwamba si sawa na miaka miwili iliyopita, lakini kwa fimbo, sasa ni bora zaidi, lakini kwa sasa safari haijafutwa. Halafu kuna safari ya Marseilles, halafu kuna safari ya kwenda Mongolia, halafu kuna moja ya mwisho sikumbuki wapi ... Mpango bado unanifanya niendelee, tuone!
... na mkutano na vijana wa Urusi na Ukraine?
Américo ana jambo fulani akilini, anatayarisha kitu, aliniambia. Anaitayarisha vyema!
Nicole Winfield (Associated Press)
Baba Mtakatifu, nilitaka kukuuliza jambo tofauti kidogo: hivi karibuni ulifanya ishara ya nguvu sana ya kiekumene, ukitoa vipande vitatu vya sanamu za Parthenon kwa Ugiriki kwa niaba ya Makumbusho ya Vatican. Ishara hii pia ilikuwa na mwangwi nje ya ulimwengu wa Kiorthodox, kwa sababu makumbusho mengi ya Magharibi yanajadili urejeshaji wa vitu vilivyopatikana wakati wa ukoloni, kama kitendo cha haki kwa watu hawa. Nilitaka kukuuliza ikiwa uko tayari kwa ishara zingine za kurejesha. Ninafikiria, kwa mfano, kuhusu watu wa kiasili na vikundi vya Canada ambao wameomba kurejeshwa kwa vitu kutoka katika makusanyo ya Vatican kama sehemu ya mchakato wa fidia kwa uharibifu uliotokea wakati wa ukoloni...
Lakini hii, kwanza kabisa, ni amri ya saba: ikiwa umeiba, lazima urudishe! Lakini, kuna historia nzima. Wakati mwingine vita na ukoloni husababisha kufanya maamuzi haya kuchukua mambo mazuri ya wengine. Hii ilikuwa ishara sahihi, ilibidi ifanyike: Parthenon, kutoa kitu. Na kama Wamisri watakuja kesho kuuliza obelisk, tutafanya nini? Lakini hapo lazima hufanywe utambuzi, kwa hali yoyote. Na kisha urejeshaji wa vitu vya asili, hiyo inaendelea, na Canada, angalau tulikubali kuifanya. Sasa nitauliza hili linakuwaje. Lakini uzoefu na watu wa asili wa Canada ulikuwa na matunda sana. Hata huko Marekani Wajesuit wanafanya kitu, na kundi hilo la watu wa asili huko Marekani. Mkuu wa shirika aliniambia siku iliyopita. Lakini turudi kwenye kurejeshewa pesa. Kwa kiwango ambacho inaweza kurudishwa, kwamba ni muhimu, na kwamba ni ishara, kwamba ni bora kuifanya, bora zaidi. Wakati mwingine haiwezekani, hakuna uwezekano wa kisiasa au uwezekano halisi au halisi. Lakini kwa kiwango ambacho unaweza kurudisha, tafadhali wafanya, hii ni nzuri kwa kila mtu. Sio kuzoea kuweka mkono kwenye mifuko ya watu wengine!
Eva Fernandez (Radio COPE)
Waziri mkuu wa Ukraine ameomba msaada wake kuwarejesha watoto hao waliopelekwa kwa nguvu nchini Urussi. Unafikiri unaweza kumsaidia?
Nafikiri hivyo kwa sababu Vatican ilifanya kazi kama mpatanishi katika baadhi ya hali za kubadilishana wafungwa, na kupitia kwa ubalozi hili lilikwenda vizuri, nadhani hilo linaweza kwenda vyema pia. Ni muhimu, angalau Vatican iko tayari kufanya hivyo kwa sababu ni sawa, ni jambo sahihi na lazima tusaidie, kusaidia ili hii sio casus belli, lakini kesi ya kibinadamu. Kwanza ni tatizo la ubinadamu badala ya tatizo utengenezaji wa silaha za vita au uhamisho wa kivita (deportation). Ishara zote za kibinadamu husaidia, kinyume chake ishara za ukatili hazisaidii. Lazima tufanye kila linalowezekana kibinadamu. Pia ninafikiri, na ninataka kusema, juu ya wanawake wanaokuja katika nchi zetu: Italia, Hispania, Poland, Hungaria, wanawake wengi wanaokuja na watoto wao na waume ambao wamekufa au wanapigana vita. Ni kweli shauku inasaidiwa kwa wakati huu, lakini msipoteze shauku ya kufanya hivyo kwa sababu shauku inaposhindikana, wanawake hawa huachwa bila ulinzi, na hatari ya kuangukia mikononi mwa mbweha ambao kila wakati huzunguka kutafuta hilo. Tuwe makini tusipoteze mwelekeo huo wa usaidizi tulio nao kwa wakimbizi. Hii fanyike kwa wote. Asante.