Tafuta

Maadhimisho ya Sinodi yawekwa chini ya maombezi ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa Maadhimisho ya Sinodi yawekwa chini ya maombezi ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa 

Maadhimisho ya Sinodi Chini ya Ulinzi na Tunza ya Bikira Maria

Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika Sikukuu ya Bikira Maria kumtembelea Elizabethi, Madhabahu ya Bikira Maria sehemu mbalimbali za ulimwengu yanasali kwa ajili ya kuombea maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu. Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa kwa njia ya ulinzi na tunza yake ya kimama alisindikize Kanisa katika maandalizi na hatimaye, maadhimisho ya Sinodi hii hapo mwezi Oktoba 2023: Umoja, Ushiriki na Utume!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya Pentekoste kwa mwaka 2023 amesema, Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu yananogeshwa na kauli mbiu “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume”, hii ni safari ya maisha ya kiroho kadiri ya Roho Mtakatifu, fursa makini ya kujenga utamaduni wa kumsikiliza Roho Mtakatifu, kwani katika shida na magumu ya historia ya Kanisa, Roho Mtakatifu ndiye nguzo na moyo wa ujenzi wa Kanisa la Kisinodi, chachu makini ya uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda wa imani tendaji. Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa ndiye anayetoa maana ya imani, maadili na shughuli za kitume, vinginevyo mambo yote haya yangekuwa ni mafundisho yasiokuwa na msingi, wajibu na shughuli za kichungaji zingekuwa ni kazi kama zilivyo kazi nyinginezo.

Maadhimisho ya Sinodi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria
Maadhimisho ya Sinodi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria

Ni katika Roho Mtakatifu imani inakuwa ni sehemu ya maisha, upendo wa Mungu unatawala na matumaini yanazaliwa upya. Roho Mtakatifu awe ni kiini cha maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu, na anao umuhimu wa pekee katika ulimwengu mamboleo, kumbe waamini wanapaswa kumwita kila siku wakisema, “Njoo Roho Mtakatifu.” Huu ni mwaliko kwa waamini kutembea katika mshikamanano, kwani Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa Siku ile ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja, ndiyo njia pekee ya kuadhimisha Sinodi na kuendelea kulipyaisha Kanisa, huku Roho Mtakatifu akipewa kipaumbele cha kwanza katika maisha na utume wa Kanisa kwa ajili ya ujenzi wa amani na utulivu ndani ya Kanisa. Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu yananogeshwa na kauli mbiu “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume”, Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika Sikukuu ya Bikira Maria kumtembelea Elizabethi, Madhabahu ya Bikira Maria sehemu mbalimbali za ulimwengu yanasali kwa ajili ya kuombea maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu. Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa kwa njia ya ulinzi na tunza yake ya kimama alisindikize Kanisa katika maandalizi na hatimaye, maadhimisho ya Sinodi hii hapo mwezi Oktoba 2023.

Bikira Maria na Sinodi

 

31 May 2023, 16:23