Tafuta

Mwaka huu wa 2023, ni kumbukizi ya miaka 650 tangu “Ufunuo wa Upendo wa Kimungu” wa Juliana wa Norwich ulipotokea. Mwaka huu wa 2023, ni kumbukizi ya miaka 650 tangu “Ufunuo wa Upendo wa Kimungu” wa Juliana wa Norwich ulipotokea. 

Juliana wa Norwich Kumbukizi ya Miaka 650 ya Ufunuo wa Upendo wa Kimungu

Mwaka huu wa 2023, ni kumbukizi ya miaka 650 tangu “Ufunuo wa Upendo wa Kimungu” wa Juliana wa Norwich ulipotokea, hili ni tukio la kiekumene, linalowakusanya waamini wa Makanisa mbalimbali ili kusherehekea tukio hili la Ufunuo wa upendo wa Kimungu. Juliana wa Norwich anakumbukwa sana kutokana na moyo wake wa ukarimu na upendo kwa wote waliokuwa wanatafuta ushauri wa kiroho na kutaka kutiwa moyo, kielelezo cha sadaka na majitoleo kwa wengine.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Julian wa Norwich, anayejulikana pia kama Juliana wa Norwich, “Lady Julian, Dame Julian au Mama Julian,” alikuwa mtangazaji wa Lugha ya Kiingereza, Zama za Kati. Maandishi yake, ambayo sasa yanajulikana kama “Revelations of Divine Love”, ni kazi za mapema zaidi za Lugha ya Kiingereza kuandikwa na mwanamke, ingawa inawezekana kwamba baadhi ya kazi zisizojulikana zinaweza kuwa na waandishi wa kike. Mwaka huu wa 2023, ni kumbukizi ya miaka 650 tangu “Ufunuo wa Upendo wa Kimungu” wa Juliana wa Norwich ulipotokea, hili ni tukio la kiekumene, linalowakusanya waamini wa Makanisa mbalimbali ili kusherehekea tukio hili la Ufunuo wa upendo wa Kimungu. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe aliomwandikia Askofu Peter Collins wa Jimbo Katoliki la East Anglia, anazungumzia kuhusu utamaduani wa Kikristo unaotambuliwa na kusherehekewa, kutokana na mvuto wake wa kimama, unyenyekevu na ufahamu wake wa kina wa kitaalimungu, ni ukumbusho mzuri wa kiimani unaokita mizizi yake katika upendo wa Mungu na utakatifu wa maisha uliomwilishwa katika huduma ya ukarimu kwa maskini na wahitaji zaidi, ili kujibu kilio cha watu wapweke katika ulimwengu ambamo umesheheni mambo mengi.

Juliana wa Norwich kumbukizi ya miaka 650 ua ufunuo wa upendo
Juliana wa Norwich kumbukizi ya miaka 650 ua ufunuo wa upendo

Jambo la msingi ni ufunuo wa ukweli unaofumbata maisha ya mkristo na mfuasi, lakini hiki ni kiini cha jamii inayosimikwa katika msingi wa jamii inayosimikwa katika haki na udugu. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Juliana wa Norwich, anakumbukwa sana kutokana na moyo wake wa ukarimu na upendo kwa wale wote waliotafuta ushauri wa kiroho na kutaka kutiwa moyo. Utayari huu ni kielelezo cha sadaka na majitoleo kwa wengine, wanaotengwa na kuhisi upweke kutoka kwenye Mataifa tajiri zaidi ulimwenguni. Kuhusiana na jambo hili, ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, Wakristo watahamasika na kutiwa moyo kutafuta kwa uaminifu, kwa shangwe na furaha zaidi kielelezo cha Kristo Yesu ambaye alikuja “si kutumikiwa bali kutumikia” Mt 20:28. Ujumbe wa huruma na upendo wa Mungu uliofunuliwa kwa Juliana wa Noriwich ni muhimu sana katika ulimwengu mamboleo, kwani alifundishwa kwa namna ya pekee kwa neema ya Mungu na kwamba, yote yatakwenda kama yalivyopangwa. Ni sala ya Baba Mtakatifu kwa wale wote wanaokumbana na changamoto ya: vita, ukosefu wa haki, athari za kiikolojia na umaskini wa maisha ya kiroho wafarijike na kutiwa nguvu na maneno ya hekima inayobubujika kutoka katika huruma na upendo. Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko amewapatia washiriki wote baraka zake za kitume!

Ufunuo wa upendo
16 May 2023, 17:05