Tafuta

Misa wakati wa ya Dominika ya Pasaka katika Uwanja wa Mtakatifu Petro uliopambwa vizuri maua Misa wakati wa ya Dominika ya Pasaka katika Uwanja wa Mtakatifu Petro uliopambwa vizuri maua  (Vatican Media)

Misa ya Pasaka 2023:Uwanja ulijaa watu katika Misa ya Papa!

Katika sherehe iliyoongozwa na Papa Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro,uliojaa watu wapatao 45,000,tangazo la Ufufuko wa Kristo lilisikika.Maelfu ya maua maridadi yalipamba uwanja wa Kanisa,kutoka Uholanzi na Slovenia na kutunzwa na Huduma ya Bustani na Mazingira ya Vatican.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Picha ya Dominika  ya  Pasaka imeoneshwa na Papa Francisko, mrithi wa Mtakatifu Petro, ameiheshimu Picha ya Kristo Mfufuka, katika Uwanja wa Kanisa kuu la Vatican, kwa kukumbusha kile kinachosimuliwa katika Injili ya Yohane, inayomwelezea Petro kuwa ni shuhuda  wa ufufuko wa Yesu. Waamini wameimba ushuhuda huo kwamba amfufuka na kweli alimtokea Simoni Petro.  

Maua mazuri kuonesha uhai wa mpya kutoka kwa Yesu
Maua mazuri kuonesha uhai wa mpya kutoka kwa Yesu

Dominika ya Pasaka tarehe 9 Aprili 2023, waamini wapatao 45,000 waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro hatimaye waliangazwa na jua na joto, ambapo wakashiriki Misa Takatifu Pasaka kumtukuza  Mwokozi, hasa baada ya kufunguliwa na Shemasi  Picha nzuri sana ya Kristo mfalme aliyeketi katika kiti cha enzi.

Ufupisho wa maadhimisho

Baadaye Papa Fransisko aliwanyunyiza maji baraka yaliyo barikiwa katika mkesha wa Pasaka yaani  Usiku Mtakatifu, akikumbusha kwamba "Furaha ya tangazo la Ufufuko wa Bwana hutujia kutoka katika mkesha wa Pasaka. Tukiwa tumegeuzwa sura na mwanga wa Mfufuka, na katika ushirika na wanafunzi wote wa Kristo, chini ya ishara ya maji, tunaadhimisha Ubatizo wetu, kushiriki katika upya wa maisha katika karamu ya Ekaristi".

Misa ya Pasaka katika Uwanaja wa Mtakatifu Petro
Misa ya Pasaka katika Uwanaja wa Mtakatifu Petro

Katika sala iliyofungua sherehe iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Fransisko akiwa na Makardinali 32, Maaskofu 15 na mapadre wakonselebtanti zaidi ya 300, Baba Mtakatifu alimwomba Mungu Baba  Mungu hivi: “Ee Baba, ambaye siku hii ya leo, kwa njia ya Mwana wako wa pekee, ulishinda mauti nawe umetufungulia njia ya uzima wa milele, utujalie sisi tunaoadhimisha Ufufuko wa Bwana, kuzaliwa upya katika nuru ya uzima, tukifanywa upya na Roho wako”.

Misa Takatifu ya Pasaka
Misa Takatifu ya Pasaka

Katika sala za waamini, msaada wa Bwana umeombwa kwa Kiingereza kama ifuatavyo: Amani, zawadi ya Bwana Mfufuka na matarajio ya watu, ishangilie kelele za silaha na chuki inayopanda kifo na mataifa yote ili kupata ustaarabu mpya unaotegemea 'Upendo'. Na kwa Kiarabu: wagonjwa, maskini na watu wapweke waadhimishe fumbo la Pasaka kwa faraja, na, kwa upendo wa ndugu, wapate huruma ya Mungu. Baba Mtakatifu kabala ya Baraka ya Urbi et Orbi, Fransisko alizungka kwa muda mrefu katika kigari kupitia sekta za mraba wa uwanja hadi  kupitia njia ya Conciliazione kuwabariki na kuwasalimu waamini wengi waliohudhuria.

Mapadre na maaskofu katika misa ya Pasaka
Mapadre na maaskofu katika misa ya Pasaka

Kama kawaida, ya utamaduni wa kupamba maua ya  pasaka njano na nyeupe inashinda, ikimaanisha rangi za uwakilishi wa Jiji la Vaticani. Maua yamunda sura iliyojaa ishara kwa maadhimisho ya Pasaka, ambayo daima inawakilisha mwanzo mpya, tumaini jipya, na maisha mapya. Kanisa kuu  na mlango wa Kanisa hili  hulipambwa kwa kwa ua  lililotengenezwa na waridi elfu sita, maua 500 ya Anthurium, Delphiniums 500 katika rangi 3, chrysanthemums ya zambarau 500 za multiflora. Katikati ya mapambo ya maua, azaleas zaidi ya 100 za maua ya ukubwa tofauti na ivy 125 za kunyongwa zinasimama.

Wakati wa Misa, karibu watu 45,000 wameudhuria
09 April 2023, 12:38