Papa:viongozi wa kidini na jukumu la kisiasa kwa ajili ya amani!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Papa Francisko ameandika barua kwa Ayatollah Mkuu wa Washia Ali Al-Sistani ambayo imetolewa katika Ofisi za vyombo vya habari Vatican, tarehe 14 Machi 2023. Katika barua hiyo Baba Mtakatifu anarudia kuzindua kwa upya hitaji la ushirikiano kati ya madhehebu yote kwa ajili ya kuishi pamoja kwa amani katika ulimwengu uliojaa migogoro mingi.
Papa katika barua hiyo anaandika kwamba: “Ninayo furaha tena kuwa na ufursa ya kuelekezea wewe baada ya mkutano wetu miaka miwili iliyopita huko Najaf nchini Iraq ambayo kama nilivyosema nikienda Iraq, ilifanya roho yangu vizuri. Ilikuwa hatua muhimu katika safari ya mazungumzo ya kidini na maelewano kati ya watu. Tangu wakati huo Papa anahifadhi kwa shukrani mazungumza ya kidugu ya kushirikisana kiroho na kimwili katika mada kubwa ya mshikamano, amani na ulinzi wa walio dhaifu zaidi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Ufalme wake kwa ajili ya wale ambao waliteseka kwa kuhifadhi utakatifu wa maisha na umuhimu wa umoja wa Watu wa Iraq.
Baab Mtakatifu anandika kwamba “Ushirikiano na urafiki kati ya waamini wa dini tofauti ni muhimu kwa ajili ya kukuza, si tu kupongezana lakini hasa yale maelewano ambayo yanachangia wema wa ubinadamu na kama ilivyo historia ya sasa ya Iraq inavyotufundisha”. Kwa hiyo Papa anabinisha kwamba “Jumuiya zetu zanaweza na lazima ziwe mahali muafaka wa umoja na ishara ya kuishi kwa amani ambao wote wanamwomba Muumba wa wote kwa ajili ya wakati ujao wa umoja duniani”.
Papa anasema kuwa “sote tunasadikishwa kwamba kuheshimu utu na haki za kila mtu na kila jumuiya, hususan uhuru wa dini, mawazo na kujieleza, ni chanzo cha utulivu wa kibinafsi na kijamii na wa maelewano kati ya watu. Kwa hiyo, ni jukumu letu pia viongozi wa dini kuwahimiza wale walio na majukumu katika jumuiya za kiraia kufanya kazi ya kuthibitisha utamaduni unaozingatia haki na amani, kuendeleza vitendo vya kisiasa vinavyolinda haki za msingi za kila mtu. Kwa hakika, ni muhimu kwamba familia ya binadamu igundue tena maana ya udugu na kukubalika kwa pande zote, kama jibu madhubuti kwa changamoto za leo.
Msisitizo wa Papa Francisko katika barua hiyo anabainisha kwamba: “wanaume na wanawake wa madhehebu mbalimbali, wakitembea katika mapatano kuelekea kwa Mungu, wanaitwa “kukutana katika nafasi kubwa sana ya maadili ya pamoja ya kiroho, ya kibinadamu na ya kijamii, na kuwekeza hili katika uenezaji wa wema wa juu zaidi wa maadili, unaoombwa na dini hizo (hati ya Udugu kibinadamu kwa ajili ya amai ulimwengu na kushi kwa Pamoja,4 Februari 2019). Katika barua yake iliyotiwa saini tarehe 28 Februari 2023, Papa Francisko anahitimishwa kwa matashi mema kwamba “kwa pamoja na wakristo, na waislamu, inawezekana daima kuwa mashuhuda wa ukweli, upendo na wa matumaini katika ulimwengu wenye alama ya migogoro mingi na hivyo kuhitaji huruma na uponyeshaji.” Anainua sala zake kwa Mungu Mwenyezi, kwa ajili yake na jumuiya nzima pendwa ya Iraq.