Papa:uwanja wa elimu jamii zinahitajika hoja zinazofaa na thabiti,zenye msingi wa imani!
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 23 Machi 2023 amekutana mjini Vatican na washiriki wa Mkutano uliohamasishwa na Chuo Kikuuu cha Alfonsian jijini Roma ambao wamekutana wakiwa mwishoni mwa mkutano wao kuhusu mada ya umuhimu wa pendekezo la Maadili la Alphonsian na katika mkesha wa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Taasisi yao ya Kipapa, itakayoadhimisha mnamo tarehe 9 Februari mwaka 2023. Amemshukuru Mkuu wa Chuo kwa maneno yake ya salamu, Msimamizi Mkuu, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Laterano, walimu, viongozi na wanafunzi, shukrani kwa huduma ya malezi wanayotoa kwa Kanisa katika uwanja wa taalimungu ya maadili. Papa aliwasalimia Maprofesa wengi waliostaafu, ambao kwa kazi zao wameacha chapa kwa taasisi hiyo ya Alphonsian na Kanisa na wanafunzi wengi wa zamani ambao walipata mafunzo pamoja nao na wanaendelea kutoa mchango wao kwa watu wa Mungu kwa huduma hii muhimu ya mafunzo!
Mtaguso wa II wa Vatican unathibitisha kwamba taalimungu maadili, inayolishwa na Maandiko Matakatifu, lazima iwasaidie waamini kuelewa ukuu wa wito wao wa kuleta upendo wa Kristo ulimwenguni (taz.Hati ya Optatam totius,16). Hatimaye, kila pendekezo la kitaalimungu-maadili, lina msingi huu: Upendo wa Mungu ni mwongozo wetu, mwongozo wa uchaguzi wetu binafsi na wa safari yetu ya kuwepo. “Ukiwa mwaminifu kwa mapokeo ya Alphonsian, unajaribu kutoa pendekezo la maisha ya Kikristo ambalo, kwa kuzingatia mahitaji ya tafakari ya kitaalimungu, sio, hata hivyo, maadili baridi, maadili ya dawati, papa ameongeza ktoa mfano wa wale ambao wanajidai kuwa wasomi na pia enzi za zamani ambapo walikuwa wakikatazwa kutona hata kitabu cha Häring, “Sheria ya Kristo”: kwa sababu ilisadikika kuwa cha uzushi bila maadili lakini shukrani kwa Mungu kwamba yameisha, na kwamba ilikuwa dawati baridi ya maadili.”
Kutoka kwao Papa amewaomba pendekezo linalojibu utambuzi wa kichungaji unaodaiwa upendo wa huruma, unaolenga kuelewa, kusamehe, kusindikiza na zaidi ya yote kuunganisha (taz. Amoris laetitia, 312). Kuwa kikanisa kunaonesha hii: kuunganisha. Sambamba na kazi ya Mtakatifu Alphonsianus, ulianza Mkutano wao kwa kutafakari juu ya dhamiri na nguvu ya malezi yake. Hii ni mada muhimu. Kwa hakika, katika mabadiliko magumu na ya haraka ya nyakati tunazopitia, ni watu tu walio na dhamiri iliyokomaa wataweza kutekeleza uwakilishi wa kiinjili wenye afya katika huduma ya kaka na dada zao katika jamii. Baada ya yote, dhamiri iko juu ya mahali popote ambapo kila mtu yuko peke yake na Mungu, ambaye sauti yake inasikika katika urafiki (Gaudium et spes, 16). Neno analosema si lake, bali linatokana na Neno lile lile la Muumba, ambaye alifanyika mwili ili awe pamoja na wanadamu. Na ni katika shule yake, katika shule ya Neno Laonekanian katika Mwili, ambapo kila mmoja anajifunza mazungumzo na wengine, akikuza shauku ya udugu wa ulimwengu wote, inayojikita katika utambuzi wa hadhi isiyoweza kukiukwa ya kila mtu (taz. Fratelli tutti; 8; Gaudium et spes, 16).
Pia ulizingatia baadhi ya masuala ya kibiolojia. Katika uwanja huu Papa amesema ni ngumu! kwa hiyo amewaalika kukuza uvumilivu wa kusikiliza na majadiliano, kama ilivyopendekezwa na Mtakatifu Alphonsianus kwa hali za migogoro. Wasiogope na wasikilize. Itakuwa msingi kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa kawaida, ambayo kutambua na kuhakikisha heshima kwa utakatifu wa kila maisha, katika kila hali. Ni kwa njia hii tu itawezekana kufafanua, katika uwanja wa elimu ya jamii, hoja zinazofaa na thabiti, zenye msingi wa imani, zinazofaa kwa dhamiri za watu wazima na zinazowajibika na zenye uwezo wa kuhamasisha mjadala wa kijamii na kisiasa. Ni muhimu kuepusha mienendo mikali ya ubaguzi, kawaida zaidi ya mjadala wa vyombo vya habari kuliko utafiti wa kisayansi na kiaalimungu wenye afya na rutuba: badala yake tumia kanuni, iliyooneshwa kila mara na Mtakatifu Alphonsius, ya kupitia vyombo vya habari, ambayo si ya kidiplomasia.
Sehemu nyingine ya mkutano wao ilishughulikia maswali ya maadili ya kijamii. Katika eneo hili pia, kuna haja ya tafakari thabiti leo hii. Mgogoro wa kimazingira, mpito wa kiikolojia, vita, mfumo wa kifedha wenye uwezo wa kuathiri maisha ya watu hadi kufikia hatua ya kuunda watumwa wapya, changamoto ya kujenga udugu kati ya watu na kati ya watu: mada hizi lazima Papa amesisitiza kwamba zituchochee kufanya utafiti na mazungumzo. “Bwana ndiye mwisho wa historia” (Gaudium et spes, 45) na jamii ya wanadamu, iliyofanywa upya katika Kristo, imekusudiwa kukua kama familia ya Mungu (Gs 40). Hili ndilo lengo la kazi yetu! Kwa hivyo, na tujaribu kwa unyenyekevu na busara kuingia katika muundo tata wa jamii tunamoishi, ili kupata kujua mienendo yake vizuri na kupendekeza kwa wanaume na wanawake wa wakati wetu njia zinazofaa za kukomaa katika mwelekeo huu (taz. Gaudium 26).
Papa amesisitiza umuhimu wa kutembea na watu katika hali ya maadili waliyo nayo. Kutembea nao na kutafuta njia ya kutatua shida zao, lakini kutembea, sio kukaa kama madaktari ambao, kwa kidole chao, wanalaani bila wasiwasi. Katika miaka ya hivi karibuni amekumbusha tulivyo kabiliana na masuala mazito ya kimaadili kama vile uhamiaji na watoto wachanga; leo hii tunaona udharura wa kuongeza mengine, kama vile faida iliyojilimbikizia mikononi mwa wachache na mgawanyiko wa mamlaka ya kimataifa. Pia tunakaribisha changamoto hizi kwa ujasiri, tayari “kueleza tumaini lililo ndani yetu” (rej. 1 Pt 3:14).
Mwishowe, Papa Francisko amesema kuwa, Kanisa linatazamia Chuo cha Kipapa cha Alphonsianus kujua jinsi ya kupatanisha ukakamavu na ukaribu wa kisayansi na watu watakatifu waaminifu wa Mungu, ukaribu na watu wa Mungu, ili kutoa majibu thabiti ya matatizo halisi, kusindikiza na kutunga mapendekezo ya maadili ya mwanadamu, makini na kuokoa ukweli na kwa manufaa ya watu. Na Mtakatifu Alphonsus alikuwa muumbaji wa maisha ya kiadili na alitoa mapendekezo kadhaa kwa njia hiyo Roho Mtakatifu awasaidie kuwa waelimishaji wa dhamiri, waalimu wa tumaini linalofungua mioyo na kuelekeza kwa Mungu. Amewabariki kutoka moyoni mwake amewashukuru sana tena kwa kazi yao. Na vile vile kuwaomba wasali kwa ajili yake.