Tafuta

2023.03.27 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano wa "Minerva Dialogues" ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. 2023.03.27 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano wa "Minerva Dialogues" ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:jitihada ya uwajibikaji wa teknolojia ikabiliane kwa thamani za kidini!

Hatuwezi kuruhusu kanuni za kanuni kupunguza au kuweka masharti ya heshima kwa utu,wala kuwatenga katika huruma,upole,msamaha na zaidi ya yote,uwazi kwa matumaini ya mabadiliko ya mtu.Ni katika hotuba ya Papa wakati amekutana mjini Vatican na washiriki wa Mkutano uitwao “Minerva Dialogues”ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 27 Machi 2023, amekutana mjini Vatican na washiriki wa Mkutano uitwao “Minerva Dialogues” ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Katika hotuba yake amewakaribisha wote Roma katika tukio la kila mwaka. Mkutano huo umewaleta pamoja wataalamu wa ulimwengu wa teknolojia, wanasayansi, wahandisi, wakuu wa makampuni, wanasheria, wanafalsafa pamoja na wawakilishi wa Kanisa, maafisa wa Curia Romana, Wataalimungu na wanamaadili, kwa lengo la kukuza utambuzi mkuu na kuzingatia muktadha wa kijamii na kiutamaduni wa teknolojia ya kidijitali kwa namna ya pekee ya akili bandia.

Mkutano wa 'Minevra Dialogues'
Mkutano wa 'Minevra Dialogues'

Baba Mtakatifu amewapongeza sana katika mchakato wa safari ya mazungumzo, ambayo kwa miaka ya mwisho imeruhusu kushirishana michango na maono kwa kufanya kuwa tunu ya hekima kwa wengine. Uwepo wao unashuhudia jitihada ya kuhakikisha makabiliano  stahiki na jumuishi kwa ngazi ya ulimwengu juu ya jitihada ya uwajibikaji wa teknolojia hizi na makabiliano ya watu kwa thamani za kidini. Papa anaamini kuwa mazungumzo kati ya waamini na wasio amini kuhusu masuala msingi  ya maadili, ya sayansi na sasa na juu ya utafiti wa maana ya maisha, unaweza kuwa njia ya ujenzi wa amani na kwa ajili ya maendeleo fungamani ya binadamu.

Teknolojia ni msaada mkubwa kwa ubinadamu. Tufikirie idadi ngapi ya maendeleo katika nyanja ya madawa, uhandisi na mawasialiano (Laudato si, 102). Na wakati tunatambua faida za sayansi na ufundi tunaona ndani yake jaribio la ubunifu wa kuwa mwanadamu na  tunu yake kubwa ya wito wa kushiriki uwajibikaji kwa matendo ya uumbaji wa Mungu (Laudato si, 131). Baba Mtakatifu katika mtazamo huo anaamini kuwa maendeleo ya akili bandia na mafunzo ya kujitegemea yameweza kuongeza nguvu ya kuchangia manufaa ya wakati ujao wa ubinadamu. Aidha anao uhakika lakini kwanga nguvu hiyo kwamba utakamilika tu ikiwa utakuwa na utashi wa dhati kwa upande wa wale ambao wanaendeleza teknolojia kwa ajili ya kutenda kwa namna adili, na uwajibikaji. Inawatia moyo wengi wanaofanya kazi katika nyanja hiyo ili kuhakikisha kuwa teknolojia inajikita awali ya yote juu mtu  na  yenye msingi wa maadili katika kuandaa na hatima yake ya wema.

Papa na washiriki wa Mkutano wa Minevra Dialogues
Papa na washiriki wa Mkutano wa Minevra Dialogues

Ni furaha ya Papa kwamba imeonekana maana ya michakato ya maendeleo ambayo inaheshimu thamani za ujumuishaji, uwazi, usalama, usawa, faragha na kuaminiana. Kwa hiyo anakubaliana hata juhudi za mashirika ya kimataifa katika kuweka kanuni za teknolojia hizo ili ziweze kuhamasisha maendeleo ya dhati, yaani ya kuchangia kuacha ulimwengu ulio bora na wa usawa wa maisha ya juu fungamani

Ni mazungumzo jumuhishi tu ambayo mtu anatafuta pamoja na ukweli yanaweza kufanya itokee maana ya kweli ya kukubaliana; na hiyo inawezakana kuibuka ikiwa inashirikishwa na kuamini kuwa katika ukweli wenyewe, wa kuwa binadamu na katika jamii… kuna safu za muungano  wa msingi ambao unasaidia maendeleo yao na kuishi kwao. (Ft 212). Thamani ya kimsingi ambayo ni lazima tuitambue na kuikuza ni ile ya hadhi ya mtu (taz. ibid., 213). “Kwa  hiyo Papa ameawaalika, katika mashauri yao, kufanya utu wa ndani wa kila mwanamume na mwanamke kuwa kigezo muhimu katika kutathmini teknolojia zinazoibuka, ambazo zinafichua chanya zao za kimaadili kwa kiasi kwamba zinasaidia kudhihirisha heshima hii na kuongeza udhihirisho wake, hata kidogo, viwango vya maisha ya mwanadamu. Wasiwasi wa Papa ni kwamba hadi sasa inaonekana ushauri ambao teknolojia za kidijitali zimehudumia kuongezeka kwa ukosefu wa usawa duniani.

Mkutano wa Minevra Dialogues
Mkutano wa Minevra Dialogues

Sio tofauti tu za utajiri wa vitu, ambapo licha ya kuwa muhimu lakini shinikizo la kisiasa na kijamii. Papa ameomba kujiuliza: Je taasisi zetu za kitaifa na kimataifa zina uweze wa kuzingatia makampuni ya kiteknolojia wahusika wa muktadha wa kijamii na kiutamaduni kwa uzalishaji wao? Kuna hatari hata ya kuongezea kwa ukosefu wa usawa ambao unaweza kuhaidia maana yetu ya mshikamano wa kibinadamu na kijamii? Tunaweza kupoteza maana ya hitimisho la kushirikisha? Kiukweli matarajio yetu ni kwamba ukuaji wa ubunifu kisayansi na kiteknoloia vinasindikiza pakubwa ukosefu wa usawa na ujumuishaji kijamii (Taz. Videomessaggio alla Conferenza TED a Vancouver, 26 Aprile 2017).

Muktadha wa hadhi ya binadamu uliosukana inatulazimisha kujua na kuheshimu kwa kuwa thamani msingi wa binadamu hauwezi kupimwa na ugumu wa takwimu. Katika michakato ya maamuzi kijamii na kiuchumi, lazima kuwa makini katika kuamini hukumu za vipindi ambazo zinajishughulisa na takwimu zilizokusanywa, mara nyingi kwa siri, kuhusu watu binafsi na sifa zao na tabia za zamani. Hasa kwa vile tabia ya mtu ya zamani isitumike kumnyima fursa ya kubadilika, kukua na kuchangia katika jamii. Hatuwezi kuruhusu kanuni za kanuni kupunguza au kuweka masharti ya heshima kwa utu, wala kuwatenga huruma, huruma, msamaha na zaidi ya yote, uwazi kwa matumaini ya mabadiliko ya mtu.

Hotuba ya Papa kuhusu mkutano wa teknolojia hasa akili bandia
27 March 2023, 17:22