Papa kwa Wabudha:Uongofu kiikolojia ni wito ili kubadili tabia mbaya kwa mustakabali wa dunia
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi 19 Januari 2023, amekutana mjini Vatican na Wawakilishi wa Kibudha kutoka Kambodia, ambapo amewakaribishwa kwa shangawe na pia wawakilishi wa jamii ya kiraia ya Kambodia. Ni furaha yake kwa ziara huyo ambayo inashangaza mshikamano wa urafiki wa kudumu kama viongozi wa kidini wenye bidii ya kuboresha ushirikiano wa kidini, chombo muhimu wa jamii ambao unaruhusu watu kuishi kwa amani kama kaka na dada, waliopatanishwa kati yao na katika mazingira wanamoishi. Katika wakati ambao familia ya kibinadamu na katika sayari yetu inajikuta mbele ya hatari kubwa, wao walichagua kwa fursa ya uongofu wa kiikolojia, kama mada ya mkutano wao. Hii kweli ni ishara halisi ya kukuza hisi na wasi wasi kwa ajili ya ustawi wa Dunia, Nyumba yetu ya pamoja na kwa ajili ya michango muhimu ambayo inahuishwa na imani za kidini na tamaduni za kiroho, wanaweza kutoa mchango muhimu katika Nchi kwenye Mchakato wa uponyaji wa kidini na kujenga upya uchumi, baada ya mgogoro wa kijamii na kisiasa kwa miaka kumi ya mwisho.
Umaskini na ukosefu wa heshima kwa hadhi ya watu wanaosukumizwa pembezoni husababisha mateso mengi na kukatisha tamaa katika wakati wetu huu; kwa hivyo lazima zilinganishwe na michakato iliyounganishwa ambayo inakuza ufahamu wa udhaifu mkubwa wa mantiki yetu ya mazingira. Ni haraka kutafuta, kwa njia ya mazungumzo katika ngazi zote, masuluhisho yaliyounganishwa kwa kuzingatia heshima ya utegemezi wa kimsingi kati ya familia ya binadamu na asili. Kwa sababu hiyo, kwa kufuata njia iliyofuatiliwa na watangulizi wake, Papa amesisitiza jinsi alivyoendelea kuhimiza utunzaji kwa nyumba yetu ya pamoja, utunzaji ambao pia ni wito wa kuheshimu. “Kuheshimu uumbaji, heshima kwa wengine, kujiheshimu na kuheshimu ulimwengu na kazi nzima ya Muumba” (Hotuba kwa mkutano kuhusu “Imani na sayansi kueleka COP26, 4 Oktoba 2021). Lakini hii haiwezi kutokea bila mabadiliko ya moyo, mabadiliko ya maono na mabadiliko ya tabia.
Uongofu wa kiikolojia unajitokeza wakati kuna utambuzi wa mizizi ya kibindamu katika mgogoro wa sasa wa mazingira; Ikiwa kuna toba ya kweli ambayo inapeleka upole pole au kusimamisha tabia za itikadi na kutenda madhara na kutoheshimu uumbaji na wakati watu wamejitolea kukuza mifano ya maendeleo ambayo huponya majeraha ya uchoyo, kwa utafutaji wa kupindukia wa faida za kifedha, kwa ukosefu wa mshikamano wa mazingira. Uongofu wa kiikolojia unatazamia mabadiliko katika mateso binafsi na yale ambayo yanaukumba ulimwengu, na hivyo ni kuitwa kuwa na utambuzi ambao ni mchango wa kila mtu anaoweza kuutoa. Uongofu huo unatualika kubadilika, kubadili tabia mbaya ili kuweza kutoa, kuunda na kutenda pamoja katika utambuzi wa mustakabali wenye haki na usawa. Mazungumzo yanaonesha utajiri mkubwa ambao kwa kila tamaduni za kidini unatoa kusaidia juhudi za kukuza uwajibikaji wa kiikolojia.
Kwa kufuata misingi ambayo Budha aliacha kama urithi wa wafuasi wake (Pratimoksa), miongoni mwa mazoezi yanayoitwa “metta”, yanayojikita kutodhuru viumbe (rej. Metta Sutta sn 1.8), na kwa kuishi mtindo wa maisha rahisi, Wabudha wanaweza kupata tabia ya huruma ya kuelekea viumbe, ikiwa ni pamoja na dunia, na mazingira wanamoishi. Kwa upande wao, kama Wakristo watimize uwajibikaji wao wa kiikolojia wakati, wanakuwa kama walinzi waliokabidhiwa, walinde kazi ya uumbaji, kazi ambayo Mungu alimkabidhi binadamu, kwa sababu, waweze kuilima na kuilinda, (Mw 2,15; na Laudato si’) wakiwa watunzaji wanaotegemewa, wanalinda uumbaji, ambayo Mungu amewakabidhi kuikuza na kuitunza (rej. Mwa 2:15; Laudato si', 95; 217). Papa amewashukuru tena kwa ziara yao, iliyothaminiwa sana, na anatuamini kwamba kukaa kwao Roma kutapendeza na kutajirisha. Pia anao uhakika kuwa mkutano na wakuu wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini utatoa fursa ya kuchunguza njia zaidi za kuendeleza ubadilishaji wa maoni kuhusu ikolojia kupitia mipango inayofanywa na majadiliano ya Wabuddha na Wakristo nchini Kambodia na katika eneo zima. Juu yao na wakazi wa nchi yao pendwa amewabariki kwa baraka ya Mbinguni.