Papa katika ndege,wamesali kwa ajili ya wale waliokufa wakivuka Sahara
Na Angella Rwezaula – Vatican
Ukimya na sala kama ule wa kutaka kubembeleza maisha ya mateso na watu waliokata tamaa wakati wakitafuta fursa mpya. Papa Francisko alisema alirudia kuonesha uchungu na huruma wakati akizungumza na waandishi wa habari Jumanne tarehe 31 Januari 2023 asubuhi katika safari ya ndege ya kutoka Roma kwenda Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kituo cha kwanza katika ziara yake ya 40 ya kitume ambayo pia itampeleka nchini Sudan Kusini. Akizama Chini rangi za jangwa na jua, hakusahau kuwa na kumbukumbu ya maisha watu wengi waliozikwa ndani ya mchanga huo au kutombea kwa uzito na uchovu, kiu na vurugu.
Papa amesema kwa wakati huu tukiwa tunavuka Sahara tufikirie, kwa ukimya, maombi kwa watu wote ambao, katika harakati za kutafuta ustawi kidogo, uhuru kidogo, wamevuka na hawajafanikiwa. Wagonjwa wengi wanaofika Mediterania baada ya kuvuka jangwa na kuwekwa katika kambi za mateso na kuteseka huko. Tuwaombee watu hao wote.
Papa ameondoa kwa hija ya amani nchini Congo na Sudan Kusini
Kabla ya maombi hayo ya kimya na mazito hata hivyo Papa Francisko kama kawaida yake aliwahutubia waandishi wa habari waliokuwepo, takriban 75 kutoka nchi 12, wawili kati yao wakiwa Waafrika na kuwashukuru kwa kuandamana naye katika safari hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa mwaka mmoja. Papa akiendelea amesema “Ni safari nzuri, ningetamani kwenda Goma, lakini kwa sababu ya vita huwezi kwenda huko. Itakuwa Kinshasa na Juba tu, tukiwa huko tutafanya kila kitu. Asante kwa kuwa hapa pamoja nami tukiwa wote, asante kwa kazi yenu nzuri sana inasaidia sana maana inawapatia watu wanaopenda picha za safari, mawazo, tafakari yenu ya safari, asante sana”, alisema Papa.
Aidha Papa Francisko ameelezea masikitiko yake kwa kutofanya mzunguko wa kawaida wa kusalimiana nao hivyo amesema: “Lakini leo siwezi”, kwa hiyo Papa Francisko alibaki kwenye kiti chake na kusema “ninahisi aibu kidogo kuona kila mtu anakuja hapa, hivyo tunaweza kusalimiana kwa mbali”. Papaakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa waliomsindikiza katika safari hiyo, mwandishi wa habari Eva Fernandez wa Radio Cope, mtangazaji wa Baraza la Maaskofu wa Hispania, alitoa kipande cha mwamba wa Kiwu ambao wanachomoa coltan na kumweleza Papa Francisko kwamba kwa kila kilo kilo moja. Watu wawili wanakufa. Kisha kipande cha lava kutoka kwenye volkano ya Nyiragongo, karibu kilomita 12 kaskazini mwa jiji la Goma, ambalo husababisha mikasa.