Tafuta

Papa anasubiriwa kwa shauku kubwa huko DRC. Papa anasubiriwa kwa shauku kubwa huko DRC.  (AFP or licensors)

Hija ya Kitume:Ujumbe wa Papa kwa Watu wa DRC na Sudan Kusini

“Ni muda mrefu ninasubiri kutembelea Nchi hizi mbili ambazo zimo ndani ya moyo wangu ambapo ninatarajia kwenda kama muhujaji wa amani na upatanisho.Ardhi zilizoko katikati ya Bara kubwa la Kiafrikia,zimejaribiwa kwa muda mrefu na mizozo."Ni maneno ya Papa kwa Watu wa Congo DRC na Sudan Kusini akiomba kusindikizwa kwa sala.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 29 Januari 2023, Baba Mtakatifu Francisko amewaeleza waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, jinsi ambavyo tarehe 31 Januari 2023 ataondoka kwenda ziara ya Kitume katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Sudan Kusini. Kwa njia hiyo wakati anashukuru Mamlaka ya raia na Maaskofu mahalia kwa mwaliko huo na kwa ajili ya maandalizi ya ziara hizo, anawasalimia kwa upendo watu wapendwa ambao wanamsubiri.

Kanisa Kuu la Notre Dame huko Kinshasa DRC linaonesha mabango ya kumkaribisha Papa
Kanisa Kuu la Notre Dame huko Kinshasa DRC linaonesha mabango ya kumkaribisha Papa

Papa Francisko akiendelea amesema kuwa: “Ni muda mrefu ninasubiri kutembelea Nchi hizo mbili ambazo zimo ndano ya moyo wangu kwa namna ya pekee na ambapo ninatarajia kwenda kama muhujaji wa amani na upatanisho. Ardhi zile, zilizko katikati ya Bara kubwa la Kiafrikia, zimejaribiwa kwa muda mrefu na mizozo: Mfano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inateseka hasa huko Mashariki mwa nchi na mivutano ya kisilaha na kwa unyonyaji; wakati huo  huo Suda Kusini, inasumbuliwa kwa miaka na vita, hawaoni saa kwamba vurugu hizo kuisha ambazo zimesaabisha watu wengi kuishi wamerundikana na hali ngumu sana”.

Mabango ya picha ya Papa katika maandalizi ya kumpokea huko Kinshasa DRC
Mabango ya picha ya Papa katika maandalizi ya kumpokea huko Kinshasa DRC

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema kwamba kwa upande wa Sudan Kusini atafika huko pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbary na Msimamizo wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland kwa njia hiyo wataishi hivyo pamoja kama ndugu katika uhujaji wa kiekumene wa amani, ili kumuomba Mungu kusitisha vizingiti kwa watu  ili kuweza kuishi kwa maridhiano. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewaomba waamini wote na watu wa Mungu wamsindikize katika ziara hiyo ya kitume  kwa sala.

Maandalizi  ya sala kambambe ya kumpokea Papa
Maandalizi ya sala kambambe ya kumpokea Papa

Ziara ya Kitume ya Papa ni kuanzia tarehe 31 Januari  hadi 5 Februari 

Ikumbukwe Ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu anatarajia kuondoka tarehe 31 Janauri kuelekea nchini Congo DRC hadi tarehe 2 Februari. Na kuanzia tarehe hiyo 2 ataondoka kwenda Nchini Sudan Kusuni, kama yeye alivyosema, ni shauku ya muda mrefu kuatembea wana wa Mungu ambao kwa muda mrefu wameteseka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana 29 Januari 2023
29 January 2023, 13:41