Tafuta

Watanzania waungana na Papa Francisko kwa sala ya Malaika wa Bwana kumshukuru Mungu kwa Miaka 61 ya Uhuru; Miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Mwalimu JK. Nyerere na Miaka 25 ya kifo cha Kardinali Rugambwa Watanzania waungana na Papa Francisko kwa sala ya Malaika wa Bwana kumshukuru Mungu kwa Miaka 61 ya Uhuru; Miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Mwalimu JK. Nyerere na Miaka 25 ya kifo cha Kardinali Rugambwa  #SistersProject

Watanzania Waungana na Papa Francisko Kwa Sala ya Malaika wa Bwana Kumshukuru Mungu

Papa Francisko ameungana na watanzania kumshukuru Mungu kwa Tanzania kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 61 tangu Tanzania Bara ilipojipatia uhuru wake. Miaka 25 tangu Kardinali Laurien Rugambwa alipofariki dunia pamoja na baadhi ya watawa kufunga nadhiri zao za daima. Hili ni tukio ambalo limeacha chapa ya kudumu katika akili na nyoyo za watanzania wengi! Yaani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 11 Desemba 2022 ameikumbuka na kuiombea Jumuiya ya waamini wa Kanisa Katoliki wanaoishi nchini Italia ambao, walikuwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kumshukuru na kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani, kwa Tanzania kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 61 tangu Tanzania Bara ilipojipatia uhuru wake. Miaka 25 tangu Kardinali Laurien Rugambwa alipofariki dunia pamoja na baadhi ya watawa kufunga nadhiri zao za daima. Hili ni tukio ambalo limeacha chapa ya kudumu katika akili na nyoyo za watu wa Mungu kutoka Tanzania. Familia ya Mungu nchini Tanzania kwa namna ya pekee kwa mwezi Desemba, inamshukuru Mungu kwa watoto wake wanne wa Shirika la Masista wa Collegine wa Familia Takatifu “Collegine Sister’s of the Holy Family” kwa kuweka nadhiri za daima katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu mkuu Alessandro Damiano wa Jimbo kuu la Agrigento lililoko kusini mwa Italia. Hawa ni Sr. Getrude Tully, kutoka Parokia ya Mtakatifu Paulo Mtume, Jimbo Katoliki la Iringa. Sr. Maria Mwigune kutoka Parokia ya Mtakatifu Augustino Temboni, Jimbo kuu la Dar es Salaam. Sr. Catherine Mgina kutoka Nyakipambo, Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mungu, Jimbo Katoliki la Iringa pamoja na Sr Eufrasia Msigwa kutoka Lugenge, Parokia ya Mtakatifu Henriki, Jimbo Katoliki la Njombe.

Masita wa Collegine walioweka nadhiri zao za daima hivi karibuni
Masita wa Collegine walioweka nadhiri zao za daima hivi karibuni

Itakumbukwa kwamba, Familia ya Mungu nchini Tanzania tarehe 9 Desemba 2022 imeadhimisha kumbukizi ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara; Miaka 100 tangu alipozaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Muasisi wa Taifa la Tanzania na Miaka 25 tangu alipofariki dunia Kardinali Laurien Rugambwa hapo tarehe 8 Desemba 1997, akiwa na umri wa miaka 80; Mwafrika wa kwanza kutangazwa kuwa Kardinali na hivyo kushiriki katika maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ambamo alitoa hotuba 15 zenye mvuto na mashiko; matendo mkuu ya Mungu. Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 8 Novemba 1984 alichapisha Waraka unaojulikana kama “Tot Tantaeque” yaani “Bikira Maria ameidhinishwa kuwa Msimamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Hili ni ombi lililotolewa kwa wakati huo na Askofu Antony Petro Mayala “23 Aprili 1940 hadi tarehe 19 Agosti 2009” aliyekuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, kuomba ili Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili aweze kuwa msimamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia familia ya Mungu nafasi ya kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa zawadi ya uhuru, siku moja tu, baada ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili. Mtakatifu Yohane Paulo II, alikazia umuhimu wa watu wa Mungu nchini Tanzania, kuomba ulinzi na tunza ya Bikira Maria, huku wakisukumwa kwa namna ya pekee na uchaji kwa Mwenyezi Mungu na Ibada kwa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili.

Watanzania wakiwa wameungana na Papa Francisko kumshukuru Mungu
Watanzania wakiwa wameungana na Papa Francisko kumshukuru Mungu

Ni matumaini ya Mtakatifu Yohane Paulo II kwamba, kwa ulinzi, tunza na maombi ya ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili atazidisha upendo, ari na mwamko mkubwa wa mshikamano kwa familia ya Mungu nchini Tanzania. Ni katika muktadha huu, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mkutano wake mkuu wa mwaka uliofanyika Juni 2016 liliamua kwamba, kuanzia sasa Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili itakuwa inaadhimishwa kitaifa nchini Tanzania ifikapo tarehe 9 Desemba. Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa katika barua yake kwa ajili ya tukio hili alisema, uamuzi huu ni utekelezaji wa zawadi iliyotolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1984 kwa kuiweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya ulinzi na maombezi ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili. Kumbe, kwa mara ya kwanza, katika historia ya Tanzania, Siku kuu ya Bikira Maria mkingiwa Dhambi ya Asili kitaifa nchini Tanzania iliadhimishwa rasmi tarehe 9 Desemba 2016. Hii ni nafasi ya kuombea familia ya Mungu nchini Tanzania ili iweze kudumisha misingi ya haki, amani, upendo, umoja na mshikamano wa kitaifa, nguzo msingi ambazo daima zimewatambulisha watanzania katika Jumuiya ya Kimataifa.

Kumbukizi ya miaka 100 tangu azaliwe Mwl. JK. Nyerere 2022
Kumbukizi ya miaka 100 tangu azaliwe Mwl. JK. Nyerere 2022

Ilikuwa ni wakati wa mkesha wa uhuru wa Tanganyika kunako mwaka 1961, Mtakatifu Yohane wa XXIII alipotunga sala maalum kwa ajili ya kuiombea Tanzania ili uhuru wake uwawezesha watanzania kuishi maisha mema zaidi kadiri iwastahilivyo watoto wa Mungu. Aliwaombea viongozi wa Serikali na watunga sera na sheria ziwe ni kwa ajili ya mafao ya wengi. Aliwaombea Watanzania paji la imani, hekima, ukweli na uaminifu kwa Amri za Mungu. Aliwaombea upendo wa Kimungu ili kujenga na kudumisha umoja na mshikamano wa kitaifa ili kushinda: utengano, ushindani, ukabila, utaifa ili watanzania wote waweze kuwa ndugu wamoja na katika Fumbo la Utatu Mtakatifu. Mtakatifu Yohane XXIII aliombea amani na maridhiano kati ya Tanzania na majirani zake; viongozi wa Serikali ili waweze kutimiza wajibu wao kama inavyostahili; raia kujipatia maisha bora zaidi na hatimaye, waweze kuwa ni raia katika Ufalme wa mbinguni milele na milele!

Mtakatifu Yohane Paulo II: 8 Novemba 1984 B.Maria Mlinzi wa Tanzania
Mtakatifu Yohane Paulo II: 8 Novemba 1984 B.Maria Mlinzi wa Tanzania

IOANNES PAULUS PP. II: LITTERAE APOSTOLICAE. TOT TANTAEQUE BEATA VIRGO IMMACULATA PATRONA CONFIRMATUR REI PUBLICAE TANZANIENSIS

Ad perpetuam rei memoriam. – Tot tantaeque sunt difficultates, pericula, discrimina, in quibus Christifideles versantur, ut ad aeternam illorum salutem non modo oporteat omnia humanae prudentiae quaerere praesidia, sed etiam superum opem implorare, maxime beatissimae Virginis Mariae, Christi Matris amabilissimae filiorumque Patronae sollicitare. Qua re, cum Venerabilis Frater Antonius Mayala, Episcopus Musomensis, idemque Coetus Episcoporum Tanzaniae Praeses, ab hac Petri Sede petierit, etiam fidelium nomine, ut beatissima Virgo Maria ab Immaculata Conceptione, Patrona apud Deum totius Rei publicae Tanzaniensis confirmaretur (nempe ad normam «Instructionis de Calendariis particularibus atque Officiorum et Missarum Propriis recognoscendis», n. 30): in Eam enim fideles summa pietate ferri, in Eiusque die festo sollemnem recuperatae patrice libertatis celebrationem fieri; Nos re bene considerata, comperto praeterea sive electionem, sive Episcopi adprobationem ad statas leges facta esse, libenter in Venerabilis Fratris, cuius mentionem fecimus, sententiam discedimus. Quapropter, iis probatis quae Sacra Congregatio pro Cultu Divino de negotio gesserit, factis olim a Nobis potestatibus, placet B. M. V. sine originis labe conceptam, caelestem esse et haberi Tanzaniae Rei publicae Patronam, certa spe fore ut tum christiana plebs pietatem in Virginem augeat, tum beatissima caelorum Regina amoris ac dilectionis dona multiplicet. Quae vero iura, privilegia, facultates confirmationem hanc consequantur, haec libenter facimus et concedimus. Contrariis nihil obstantibus.

Datum Romae, apud Sanctum Petrum, sub anulo Piscatoris, die VIII mensis Novembris, anno MDCCCCLXXXIIII, Pontificatus Nostri septimo.

AUGUSTINUS Card. CASAROLI, a publicis Ecclesiae negotiis.

Papa Tanzania

 

11 December 2022, 15:15