Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Bahrein:changamoto halisi ni kumpenda adui

Katika Misa ya Papa,Jumamosi Novemba 5,iliyoadhimishwa katika Uwanja wa Taifa wa Bahrain mahubiri yamejikita na mada kuhusu amani na haki,na kwamba nguvu ya Yesu ni upendo kwa wote hata maadui,anavunja minyororo ya ubaya na kujenga ulimwengu wa udugu.Uhusiano jjumuiya na kidugu ukuzwe kila mahali.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu wakati wa  misa Takatifu  ambayo imejikita na mada ya Amani na Haki katika uwanja wa Kitaifa wa Bahrein Jumamosi tarehe 5 Novemba 2022 katika ziara yake ya Kitume ya 39 ya kuwa nje ya nchi na nchi ya 58 kutembelea akiwa kama Papa. Akianza mahubiri yake kwa kuongoza na masomo yaliyosomwa, Baba Mtakatifu  Francisko amesema kuhusu Masiha ambaye Mungu atafanya kuchomoza  kwamba  nabii Isaya anasema kuwa uwezo wake utanea, na amani haitakuwa na mwisho [Is 9,6]. Hii utafikiri ni kinyume katika hali ya sasa ya ulimwengu, kiukweli mara nyingi tunaona kwamba kadiri ya kutafuta madaraka, ndivyo hata amani inakuwa hatarini. Kinyume chake nabii anatoa tangazo maalumu jipya kwamba Masiha anayekuja ni mwenye nguvu, lakini sio kwa namna ya kuongozwa na vita na kutawala wengine, badala yake ni Mfalme wa Amani [Is, 9,5] kama Yule anayepatanisha wanadamu na Mungu na kati yao.  Ukuu wa nguvu yake hausaidiwi na nguvu za vurugu, lakini za wadhaifu wa upendo. Na tazama nguvu ya Mungu ni upendo.  Papa amesisitiza kuwa hata kwa wote Yeye aliwekeza nguvu yake, ya uwepo wa upendo, wa kupenda kwa niaba ya jina lake la  kupenda kama Yeye alivyopenda. Je kwa namna gani? Pasipo masharti. Si kwa sababu mambo yanapokwenda vizuri na kuhisi kupenda, daima, si kwa mtazamo wa rafiki zetu tu na walio karibu bali  kwa wote hata maadui.

Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba
Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba

Kupenda daima na kupenda wote ndiyo suala la kutafakari juu yake, alisema Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri hayo. Akitazama Injili iliyosomwa kutoka Matayo 5,38- 48,  Papa alisema Neno la Yesu linawaalika kupenda daima yaani kubaki daima katika upendo wake, kuukuza na kufanyia mazoezi katika kila hali ambazo wanaishi. Lakini lazima kuwa na umakini juu ya Mtazamo wa dhati wa  Yesu, Yeye hasemi kwamba itakuwa rahisi na wala kupendekeza upendo wa kihisia tu na kimapenzi, kama vile katika mahusiano ya kibinadamu,  katika wakati wa mgogoro na kati ya watu utafikiri hakuna sababu za vizingiti. Yesu si wa hasira, Yeye  ni wa kweli. Yeye anazungumza wazi kuhusu mabaya na maadui [Mt 5, 38-43]. Yeye anajua kuwa ndani ya uhusiano zinatoka kila siku mapambano kati ya upendo na chuki na hata kila siku ndani mwa kila mtu, panajiwakilisha mapingamizi kati ya mwanga na giza,  kati ya mapendekezo na shauku ya wema na yale ya udhaifu wa dhambi ambao mara nyingi unakuja juu na kutuburuza katika matendo ya ubaya.

Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba
Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba

Hata ikiwa wakati mwingine tunafanya uzoefu, licha ya jitihada za ukarimu, daima hatupokei wema ambao tulitegemea, badala yake wakati mwingine bila kueleweka tunapokea ubaya. Na tena anaona na kuteseka kwa kuona nyakati zetu katika sehemu nyingi za dunia ambamo mazoezi ya nguvu ambazo zinamwilishwa na kuongezeka vurugu na katika nafasi binafsi kwa kuweka ufinyu kwa nchi  zile nyingine na kupendekeza utawala huku kwa kuweka vizuizi vya uhuru msingi na kukanyaga wadhaifu. Kwa maana hiyo Yesu anasema kuna migogoro, mikandamizo na uadui. Mbele ya hayo yote swali muhimu la kujiuliza ni jinsi gani ya kufanya tunapojikuta tunaishi katika hali kama hiyo? Pendekezo la Yesu ni la ajabu, kavu na la kushangaza. Yeye aliwaomba mitume wake wawe na ujasiri wa kuthubutu kwa kile  ambacho utafikiri ni uwazi wa kupoteza. Aliwaomba daima wabaki waaminifu, katika upendo, licha ya yote na mbele ya ubaya na adui.  Tendo la kibinadamu kirahisi ni la kimisumari,  jicho kwa jicho, na jino kwa jino, kwa  maana ya  kile chenye kufanya haki kwa kutumia  silaha ile ile ya ubaya tulioupokea. Yesu anadiriki kupendekeza jambo jingine jipya, tofauti na lisilofikiriwa, msibishane na mtu mbaya bali mtu akikupiga shavu la kulia umwelekezee pia jingine [Mt 5,39].

Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba
Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba

Baba Mtakatifu kwa kusisitiza zaidi amesema tazama ni kitu gani Bwana anaomba, kutoota kwa hasira ulimwengu unaohuishwa na udugu, bali kujitahidi kuanzia na sisi wenyewe, kuanza kuishi kwa dhati na ujasiri wa kidugu duniani, kwa kuhifadhi katika wema hata tunapopokea ubaya kwa kutuvunja matamanio ya kulipiza visasi, kuzuia vurugu, kuondoa moyo wa kijeshi. Mtume Paulo anatoa mwangwi anapoandika  kuwa msiache mshindwe na ubaya bali mshinde ubaya kwa wema [Rm 12,21]. Kwa njia hiyo mwaliko wa Yesu hautazami awali ya yote masuala makubwa ya binadamu, bali hali halisi ya kina katika maisha yetu. Uhusiano wetu katika familia, uhusiano wetu katika jumuiya ya kikristo, uhusiano ambao tunaukuza katika hali halisi tunayofanya kazi na katika jamii tunayojikuta nayo.  Kutakuwa na migogoro, vipindi vya mivutano, kukinzana, mitazamo tofauti lakini anayefuatilia Mfalme wa amani daima lazima aombwe amani. Haiwezekani kuwa na amani ikiwa neno baya linajibiwa kwa  neno baya zaidi, ikiwa kofi linajibiwa na kofi njingine, badala yake inatakiwa kuzuia, kuvunja mnyororo wa ubaya,  kuvunja tamanio la vurugu, kuacha kukuza hisia za kiburi, kumaliza tabia za kulalamika na kujililia. Inahitaji kubaki katika upendo na daima ni njia ya Yesu kwa ajili ya kutoa utukufu kwa Mungu wa Mbingu na kujenga amani duniani. Kupenda daima!

Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba
Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba

Baba Mtakatifu Francisko akizungumza juu ya mantiki ya pili kuhusu kupenda wote alisema inawezekana kutia juhudi katika upendo lakini haitoshi ikiwa ni kubaki katika mantiki finyu ya wale ambao tunapokea upendo kwao, kwa marafiki na  wale tunaofanana nao. Hata katika muktadha huo mwalikoo wa Yesu unashangaza kwa sababu unapanua mipaka ya sheria na  maana. Tayari upendo wa jirani, aliye karibu hata kama ni  sababu na ni ngumu. Kwa kawaida  ni kile ambacho Jumuiya au watu wanatafuta kufanya ili kuhifadhi amani za binafsi. Na ikiwa tuko katika sehemu moja ya familia au taifa lile  ikiwa wana mawazo sawa na ladha sawa, ikiwa wana imani sawa ni kawaida kutatua na kusaidia na kupendana. Lakini ni kitu gani kinatokea ikiwa wa mbali anatukaribia, ikiwa ni mgeni tofauti  au imani tufauti anakuwa karibu na nyumba yetu? Baba Mtakatifu amebainisha jinsi ambavyo ardhi  hiyo daima ni sura hai ya kuishi kwa utofauti, katika ulimwengu wetu ambao diama umezidi kuongeza uhamiaji wa wat una mawazo mengi, tabia na tamaduni.

Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba
Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba

Kwa maana hiyo ni muhimu kukaribisha uchochezi huu wa Yesu akisema ikiwa mnawapenda wale ambao wanapenda mnapata tuzo gani? Je watoza ushuru hawafanyi vile? [Mt 5, 46]. Changamoto ya kweli ili kuwa wana wa Bwana na kujenga ulimwengu wa Ndugu ni kujifunza kupenda wote hata adui. Mmesikia kwamba imenewa, Umpenda jirani yako na Umchukie adui yako, lakini mimi ninawaambia Wapendeni adui zenu  waombeeni wanaowaudhi [Mt 5, 43-44]. Hii kiukweli maana ya kuchagua kutokuwa na adui, kutoona mwengine  kama kizingiti za kushinda, lakini kama kaka na dada wa kupenda. Kupenda adui ni kubeba ardhi ambayo ni kioo na  kufanya kushuka katika dunia ule mtazamo na moyo wa Baba ambaye hafanyi utofauti, habagui bali yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki [ Mt 5,45].

Misa Takatifu huko Bahraine
Misa Takatifu huko Bahraine

Baba Mtakatifu Francisko amesema nguvu ya  Yesu ni kupenda na Yesu anatupatia uwezo wa kupenda hivyo kwa namna ambayo sisi tulivyo binadamu. Lakini uwezo unaofanana hauwezi kuwa tunda la jitihada zetu tu, awali ya yote ni neema. Neema ambayo lazima kuiomba bila kuchoka:” Wewe Yesu unayenipenda, nifundishe kupenda kama wewe. Yesu, Wewe ambaye unanisamehe, nifundishe kusamehe kama wewe. Utume Roho wako juu yangu, Roho wa upendo. Baba Mtakatifu ameongeza kuwa ni lazima kuomba hilo kwa maana mara nyingi Bwana amepelekewa umakini wa maombi mengi japokuwa hilo ni muhimu kwa wakristo, kujua kupenda kama Kristo mwenyewe. Kupenda ni zawadi kubwa sana inayopokelewa wakati inapoachwa nafasi kwa  Bwana katika sala, wakati wa kupokea Uwepo wake katika Neno lake na kubadilika na katika mapenzi  ya unyenyekevu kwenye  Mkate uliomegeka. Kwa namna hiyo taratibu zinaanguka kuta ambazo zilikuwa ngumu ndani ya moyo na kupokea furaha ya kutumiza matendo ya huruma  kwa kuelekea wengine. Kwa maana hiyo inawezekana kujua kuwa maisha ya heri yanapitia kwenye heri na ni pale inapowezekana kugeuka kuwa wahudumu wa amani [Mt 5,9].

Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba
Misa Takatifu huko Bahrain 5 Novemba

Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu amependa kuwashukuru kwa ushuhuda wao wa upole na unyenyekevu wa kidugu, kwa ajili ya kuwa mbegu ya upendo na amani kwa ardhi ile. Ni changamoto ambayo Injili inawakabidhi kila siku katika jumuiya zao za kikristo na kwa kila mmoja wao. Na wote waliofika kuadhimisha sherehe hiyo kutoka katika nchi Nne za Usimamizi wa Kitume huko Uarabuni Kaskazini yaani Bahrein, Kuwait, Qatar  South Arabia  ikiwa ni pamoja na nchi nyingine za Ghuba kama ilivyo hata maeneo mengine madogo ambapo amesema amewapelekea upendo na ukaribu wa Kanisa la Ulimwengu ambalo linawatazama na kuwakumbatia, linawatakia mema na kuwatia moyo. Bikira Mtakatifu Mama Yetu wa Arabia awasindikize katika njia na kuwalinda daima katika upendo kwa wote.

Mahburi ya Papa katika huko Bahrain 5 Novemba 2022
05 November 2022, 09:16