Tafuta

Matera, Italia: Kanisa Kuu la Mji wa Matera Matera, Italia: Kanisa Kuu la Mji wa Matera  

Papa:kuna mabadiliko ya ziara huko Matera.Kard.Zuppi:jitihada kwa raia ni kwa Mkristo!

Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia anamshukuru Papa Francisko kwa mabadiliko yaliyofanywa ya kuweza kuwapo huko Matera DominikaSeptemba 25 kwa ajili ya kuhitimisha Kongamano la 27 la Ekaristi Kitaifa.Siku ambayo kiukweli nchini Italia wanapiga kura ya uchaguzi wa kisiasa ambapo Kardinali amesema kuwa haki ni jukumu la raia wote wakiwa ni pamoja na wakristo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, Kardinali Matteo Zuppi, ametoa maoni yake juu ya mabadiliko ya ziara  ya Dominika 25 Septemba 2022. Kwa mujibu wa ofisi ya Vyombo vya habari Vatican mnamo 6 Septemba kuwa kardinali amesema: “Tunamshukuru sana Baba Mtakatifu kwa nia yake kubwa ya kupeleka mbele muda wa ziara yake ya kichungaji huko Matera katika hitimisho la Kongamano la Ekaristi Takatifu la Kitaifa la 27, katika siku muhimu sana kwa nchi yetu, iliyoitwa kubuni mustakabali wake kwa njia ya kura”.

Ratiba ya awali na mpya

Katika ratiba ya tarehe 8 Julai iliyopita, ilikuwa inaonesha ratiba  juu ya liadhimisha misa saa 4.00 kamili  na baadaye  kutembele kurudi Vatican iliyokuwa impangwa  saa 6.30.  Kwa mujibu wa ratiba mpya , baada ya kutua Papa Francisko atakaribishwa muda wa saa 2.45 asubuhi katika Uwanja wa Manispaa uitwao XXI Settembre, ambapo saa 9.00 ataongoza Misa itakayofungwa kwa sala ya Malaika wa Bwana. Misa inatarajiwa kumalizika saa  5.00, ambapo Papa Francisko ataaga mamlaka itakayokuwa imekaribisha, baadaye  atakwenda  kwa gari hadi  kiwanja cha Shule ya Riadha ili kuondoka mapema, saa 5.15 asubuhi  kurudi Vatican  mida ya  6.45 mchana.

Kanisa ni kwa ajili ya uhuru wa dhamiri

Akikumbuksha juu ya jitihada kwa raia  kwamba ni sehemu muhimu ya maisha ya Kikristo, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia( CEI) amesisitiza kwamba “kupiga kura ni haki na wajibu wa raia wote. Kanisa ni kwa ajili ya uhuru wa dhamiri, hakika si kwa ajili ya uhuru wa kutojali”. Kwa njia hiyo  Kardinali Zupi anatoa shukrani kwa Papa Francisko kwa ishara yake ya tahadhari ambayo itawawezesha wajumbe wa majimbo yote ya Italia waliopo Matera kurejea miji yao kwa ajili ya mafao ya muda wa kuweza kupiga kura”.

07 September 2022, 17:44